Thursday, August 12, 2010

Dkt Slaa apitishwa kwa 99.2%

MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo umempitisha rasmi kwa asilimia 99.2, Dkt. Willibrod Slaa kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Wakipiga kura za NDIYO au HAPANA kwa kunyoosha mkono, wajumbe 752 kati ya 758 walisema NDIYO Dkt. Slaa abebe bendera ya chama chao katika mbio za kwenda ikulu, sita walisema HAPANA, baada ya kuulizwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe.

“Niko tayari kwa moyo wangu wote, kwa akili yangu yote na kwa nafsi yangu kamili kuwatumikia Watanzania, kadri matakwa ya Mungu yatakavyokuwa,” alisema Dkt. Slaa baada ya kupitishwa.

RSM

0 comments:

Post a Comment