Monday, August 30, 2010

Dr Slaa atangaza sera yake

Kiongozi wa CHADEMA aahidi katiba mpya Tanzania iwapo atashinda

Nchini Tanzania,mchaka mchaka wa kampeni za uchaguzi umeanza kushika kasi navyo vyama vya kisiasa vikiianza safari ya kuwashawishi wananchi kuwachagua. Mwishoni mwa wiki chama tawala cha CCM,kilizindua rasmi kampeni zake. Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na maendeleo,CHADEMA kinatazamiwa kuzindua rasmi kampeni zake mwishoni wa juma hili mjini Dar es Salaam. Hivi karibuni baadhi ya vigogo wa chama cha CCM wamekiacha mkono na kuhamia chama cha CHADEMA kinachoonekana kupata nuru mpya.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam George Njogopa alibahatika kukutana na mgombea wa urais wa chama cha CHADEMA Dr Wilbrod Slaa aliyekuwa na mengi ya kuelezea.

Josephat Nyiro Charo

0 comments:

Post a Comment