Wednesday, August 25, 2010

DR.SLAA:THE NEXT PRESIDENT?

Pichani ni Dr.Willbroad Peter Slaa akihutubia mamia ya wananchi waliokwenda kumsikiliza hivi karibuni mjini Arusha.

Hivi karibuni Dr.Slaa alitangazwa kuwa mgombea wa kiti cha Urais kwa kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambacho kwa muda sasa amekitumikia kama Katibu wake Mkuu.

Tangu ilipotangazwa kwamba Dr.Slaa sio tena candidate wa Ubunge bali Urais,kumekuwa na maoni tofauti tofauti.Kuna ambao wanasema Dr.Slaa asingethubutu kugombea Urais na badala yake angeendelea tu kugombea kiti chake cha Ubunge wa Karatu kwani nafasi ya kumshinda mgombea wa Chama Cha Mapinduzi-Jakaya Mrisho Kikwete ni ndogo sana.

Wanaounga mkono hoja hiyo wanasema,kwa sababu uwezekano wa Dr.Slaa kumshinda Kikwete ni mdogo,hiyo ina maana kule Bungeni kutakuwa kumepungukiwa na mbunge makini na ambaye kwa muda wa miaka mitano iliyopita,aliwapa tabu na challenge kubwa,wabunge na viongozi wa chama tawala cha CCM.

Kwa upande mwingine,wale wanaounga mkono uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Dr.Slaa katika kuwania Urais,wanasema ni kitu kizuri kwa ukuaji wa demokrasia na wanaamini kwamba Dr.Slaa atamshinda Jakaya Mrisho Kikwete na kwa maana hiyo he will become our next President.

Tungependa kupata maoni yako.Je,unakubaliana na wale wa kundi la kwanza au la pili? Will Dr.Slaa become our next President?

SOMA HABARI NYINGINE ZA DR SLAA CHINI

PESA ANAZO CHANGIWA DR SLAA ZA NINI?

Dr SLAA Mgombea Uraisi CHADEMA ?

KAULI MBIU YA DR SLAA

Maswali na Majibu – Mgombea Uraisi Dr W Slaa ...

Mapokezi ya Dr. Slaa Dar es Salaam Tarehe 07.08.2010

baadhi ya majibu ya dr slaa kuhusu maswali aliyoulizwa

Maoni - Mdahalo Wa Wagombea Uraisi Tanzania 2010


0 comments:

Post a Comment