Wednesday, August 18, 2010

hassan yahaya hussein ajitosa kinyang'anyiro cha kiti cha udiwani kata ya Mzimuni, Magomeni,

Wednesday, August 18, 2010
yanga oye! nyaipiga simba 3-1 kutwaa ngao ya hisani
Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom TAnzania Ephraim MAfuru wakimkabidhi ngao ya hisani nahodha wa Yanga Fred Mbuna baada ya vijana hao wa Jangwani kuwatungua Wekundu wa Msimbazi, Simba, bao 3-1 jioni hii neshno hapa Dar katika mchezo wa ngao ya hisani. Dakika 90 ngoma ilikuwa droo 0-0 ndipo ikaja mikwaju ya penati ambapo Yanga walitia kimiani mitatu na kipa wa Simba Ally Mustafa Barthez aliokoa mbili. Simba walikosa mikwaju mitatu, moja walopaisha na kipa wa Yanga Yao Berko toka Ghana akafuta moja
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Davies Mosha akijidai na ngao ya hisani ambayo vijana wake wameipata kwa kuwafunga watani wa jadi 3-1

Yanga Imara - Daima mbele, nyuma mwiko
aiayayayaaaaaaa yayayayayaaaaaaaa

Mashabiki wa Sima wanadai
ati mgonjwa kaanza kunywa uji....
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
wadau wa sekta ya habari wakutana kujadili uchaguzi mkuu 2010 leo
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO akiongea na wadau wa sekta habari leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa kujadili mwongozo wa maadili ya vyombo vya habari katika kutoa taarifa za uchaguzi mkuu 2010. Pamoja na mambo mengine amewataka kuheshimu Uhuru wa vyombo vya habari uliopo nchini kwa kuepuka kuandika habari za uchochezi na matumizi ya lugha zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani.Bw. Deogratias Mushi mdau katika sekta ya habari akiongoza majadiliano ya mkutano wa wadau wa sekta habari kujadili mwongozo wa maadili ya vyombo vya habari katika kutoa taarifa za uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwezi Octoba, 2010 leo jijini Dar es salaam.Wadau wa sekta ya habari nchini wakipiga kura kupitisha baadhi ya maamuzi yatakayozingatiwa na vyombo vya habari kama mwongozo wa maadili kwa vyombo vya habari katika kutoa taarifa za uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwezi Octoba 2010.Baadhi ya wadau wa sekta ya habari wakichangia masuala mbalimbali kuhusu Mwongozo wa maadili ya vyombo vya habari katika kutoa habari za uchaguzi mkuu wa 2010 leo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kutoa habari zisizopendelea upande wowote ,zenye ukweli na zenye kujali uchunguzi wa hoja.

(Picha na Aron Msigwa -Globu ya Jamii)
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
JK na Dr Bilal wasaini tamko la kisheria kuthibitisha usahihi wa taarifa katika fomu za ugombea Urais,pia atoa Hati idhini kwa vyuo vikuu nchini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Mwenza Dr. Mohamed Gharib Bilal wakisaini tamko la Kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizozitoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Jaji Mkuu Agostino Ramadhani akishuhudia.Tamko hilo lilisainiwa leo asubuhi na kukabidhiwa ofisini kwa Jaji Mkuu jijini Dar es Salaam.Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Jaji Mkuu Agostino Ramadhani tamko la kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizotoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ofisini kwa Jaji mkuu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Anayeshuhudia kulia ni mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekabidhi Hati ya Idhini(University charter) kwa baadhi ya vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu hapa nchini.Pichani Rais Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Chuo Cha Mtakatifu Agustino Mwanza Mhashamu Askofu Aloyce Balina hati Idhini kwa chuo kishiriki cha Bugando Weill Medical College kilichopo jijini Mwanza.
(Picha na Freddy Maro)
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
mtoto andrea anaomba msaada wa gharama za matibabu
Andrea akiwa kitandani pake

Mtoto Andrea Kipangula ni mtoto yatima kati ya watoto wanaosaidiwa vifaa vya shule na TAWLAE kwa msaada wa USAID/AED/ AGSP.

Ana miaka 10 (kumi) na anasoma darasa la nne (4) katika shule ya Kibao, wilaya ya Mufindi, kwa sasa, kwa masaa anayoweza kumudu anasoma shule ya msingi ya Makuburi, wilaya ya Kinondoni.

Mtoto huyu ana tatizo la kutopata choo kwa muda mrefu kwa vile njia yake ya haja kubwa inahitilafu. Madaktari wamemfanyia upasuaji mara saba hosipitali ya rufaa ya Muhimbili ili kurekebisha hali yake.
Kwa sasa imebidi atumie utumbo mkubwa kutolea choo ambao upo nje ya tumbo lake, hali ni ngumu kwa mtoto huyu.

Bibi yake ambaye ni mzee sana pamoja na shangazi yake ambaye ni mjane, hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na maisha.
Wale watakaopenda kusaidia kwa njia ya benki,

tafadhali weka katika akaunti namba
0121030000838
ya NBC Samora Branch Dar-es-salaam,
ukishaweka tuarifu kupitia simu namba
0754-360215, 0754-360215, 0754-360215
au +255(22)2700085, +255(22)2700085, +255(22)2700085,
au fax pay in slip ya benki kwenye namba +255(22)2700090 +255(22)2700090 +255(22)2700090
Vinginevyo tuletee msaada kwenye ofisi zetu zilizopo
MARI-MIKOCHENI
Plot namba 24 “b”
Sam Nujoma Road
kuelekea kiwanda cha Cocacola,

Tafadhali tunaomba msaada wako ili kumsaidia mtoto Andrea.
Aksante.
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
balozi peter kallaghe aongea na bongo celebrity
Balozi Peter A. Kallaghe

Miezi michache iliyopita, Rais Jakaya Kikwete, alifanya mabadiliko na teuzi kadhaa za mabalozi wetu katika nchi mbalimbali. Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na yale ya kumhamisha Balozi Peter A.Kallaghe kutoka nchini Canada kwenda kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Uingereza.

Wakati akijiandaa kuondoka nchini Canada kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Uingereza,BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano maalum utakayoyasoma hivi punde.

Balozi Peter Kallaghe anaelekea nchini Uingereza kuchukua nafasi iliyoachwa na Balozi Mwanaidi Maajar ambaye amehamishiwa nchini Marekani. Fuatana nasi katika mahojiano haya:
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
tangazo la mhadhara Leeds Agosti 21, 2010
Asaalam Aleykum Kaka Michuzi na Wadau
wote wa Globu ya Jamii popote pale duniani

Kwanza nawaombea Ramadhani Mubaraka wote waliojaaliwa kufunga na ambao hawakujaaliwa.
Sisi ndugu zenu wa hapa Leeds, U.K tumeandaa muhadhara rasmi kwa ajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na pia futari ya pamoja siku ya tarehe 21.08.2010;
Muhadhara utafanyika katika ukumbi wa Intercontinental Mill 3, uliopo Mabgate Mill,
Macaulay street,
LS9 7BZ,
LEEDS;
Kuanzia saa 7.00 mchana hadi
saa 12.00jioni (13.00pm - 18.00pm).

WAHADHIR ni Ustaadhi SALUM HATIB kutoka LONDON na wenzake.

Futari ya pamoja itakuwa katika ukumbi wa Ebor Garden kuanzia saa 2.00 usiku hadi saa 4.00 usiku

Kwa upendo mkubwa na moyo mkunjufu Leeds Swahihi Community inawakaribisha WADAU WOTE kwenye MUHADHARA na FUTARI
Ima ima msikose wake kwa waume, hasa wewe kaka MICHUZI

Waandaaji ni : LEEDS SWAHILI COMMUNITY

Allah atujaalie Ibada kamilifu, Upendo, Afya, Ushirikiano na Subra katika kila lenye Kheri dunia na Akhera, Inshaalah! ;
Allah aijalie GLOBO yetu hii iwe ya kheri na kiunganisho cha upendo. Inshaalah !

Asalaam Aleykum, Wabirah Tawfiq

M/kiti; Aran Rashid na wajumbe Sheikh Mahir Mzishi na Ust. Ridhiwan
© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
ankal aibuka na libeneke la michuzipost.com
Asalaam Aleikhum Wadau,

Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya la www.michuzipost.com
ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa.

Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia kuboresha libeneke hili.

Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu kwa muda wote huu.

Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la www.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamii itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa mapana na undani zaidi.

Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii inavyojionesha: http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments.

Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea kama kawa.

Libeneke hili jipya la www.michuzipost.com limewezekana kwa ushauri na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw. Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke hili.


Muhidin Issa Michuzi
Mkurugenzi
Michuzi Post Ltd.

© Michuzi | Wednesday, August 18, 2010 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 10
hassan yahaya hussein ajitosa kinyang'anyiro cha kiti cha udiwani kata ya Mzimuni, Magomeni, jijini Dar
Hassan Yahaya Hussein (pichani) anawania Udiwani kata ya Mzimuni jijini Dar kupitia tiketi ya CHADEMA. Hivi tunavyoongea ameshateuliwa na kuchukua fomu za Tume ya Uchaguzi, amejaza na jana amezirejesha tayari. Anaomba kura yako ewe mkazi wa kata ya Mzimuni ili afanye kile anachotaja kuwa mabadiliko makubwa kwenye kata hiyo yenye wakazi wengi na rasilimali kibao. Hassan ni mwanae mkubwa Sheikh Yahya Hussein, mnajibu na mwanazuoni maarufu nchini na afrika mashariki na kati.

0 comments:

Post a Comment