Sunday, October 24, 2010

Kataa Ujumbe wa uchochezi kwa chadema

Kataa Ujumbe wa uchochezi kwa chadema

Ndugu zangu

Saa hii nimepata ujumbe toka namba 25565906805 unaosema

CHADEMA WAMETEKELEZA AHADI YA KUMWAGA DAMU , JUZI WAMEMUUWA NDUGU WA MGOMBEA WA CCM MASWA . MJUMBE WA KAMPENI WA SLAA AMEKAMATWA
TUWAKATAE CHADEMA WAMWAGAJI DAMU .

Ndugu yangu ukipata ujumbe kama huu usisambaze kwa wenzako au kwa mtu wowote kusambaza ni kosa na utaweza kushitakiwa kwa kutumia kifaa chako cha mawasiliano kwa ajili ya kutuma taarifa za uchochezi au za uchonganishi katika jamii

Tuzidi kufanya kampeni kwa amani , upendo na utulivu hata katika kupiga kura tutumie nafasi hiyo kwa amani na upendo pia .

0 comments:

Post a Comment