Monday, October 4, 2010

KAMPENI KWA NJIA YA SIMU/MTANDAO

Kampeni kwa njia ya Simu /Mtandao
Kuna Watu wamekuwa wanajaribu kuufananisha Uchaguzi wa 2010 na ule wa mwaka 1995, wamekuwa wakijaribu kulinganisha Umaarufu alionao nao Dr. Slaa na Umaarufu aliokuwa nao Augustino Lyatonga Mrema alipokuwa anagombea Urais Kupitia NCCR-Mageuzi. Watu hao wanadiriki kutumia ufanano wa Umaarufu huo hata kujaribu kutabiri eti Dr. Slaa ataanguka kama alivyoanguka Mrema 1995.

Watu hao wamejivika upofu wa Kufananisha watu hao wawili huku wakikwepa ama kwa makusudi ama kwa kutojua Tofauti ya Kimazingira kati ya Mwaka 1995 na mwaka 2010

Kuna mambo ambayo inabidi yaangaliwe kabla ya kufananisha hali ilivyokuwa 1995 na 2010

Mwaka 1995 technolojia ya habari haikuwa imeenea sana kama 2010, Sasa hivi karibu kila Mzazi kijijini mwenye mtoto Mjini anatumia simu ya Mkononi. Nimekuwa nikifuatailia kura za mtandaoni ambazo zimekuwa zikimpa Ushindi mkubwa Dr. Slaa dhidi ya Wapinzani wake.

Japokuwa Baadhi ya Watu wamekuwa wakiziponda polls hizi ila kwa mtu makini hawezi kuzipuuzia hata kidogo na hata Wapinzani wa Dr. Slaa hawawezi kuzipuuzia hata kidogo kwa sababu wanatambua ni Ujumbe gani unaotolewa

Baadhi ya Watu wanaweza kuja hapa na kutoa Hoja kwamba ni Watanzania wangapi wana access na internet? Watanzania Wangapi wanajua FOS ? Hizi ni Hoja Mfu zinazofanana na Mgombea mmoja wa Urais aliyena kwamba kura 350000 ni ndogo sana kwake bila kuangalia ni watu wangapi wako nyuma ya hao watu 350,000

Ndugu Wazalendo wapenda Mabadiliko leo nina Ujumbe Muhimu sana kwenu

Wanaweza kutubeza kwa Uchache wetu, wanaweza kutubeza eti hatupigi kura, Wanaweza kutubeza eti kwamba sisi ni watu wa kulalamika kwenye Mitandao, wanaweza kutubeza kwamba tunaota ndoto za mchana

Lakini Ukweli ni Kwamba

Sisi tuna Wazazi, tuna Wadogo zetu na kaka Zetu na hata Ndugu zetu wale wanaobezwa kwa kukosa huduma hii ya Mtandao, Lakini ndugu zetu hawa asilimia kubwa wana Simu za Mikononi

Sasa wote wapenda mabadiliko, wataopiga kura na ambao hawatapiga kura kwa sababu yeyote Nyanyua Simu yako Mpigie Shangazi yako, mama yako, bibi yako, babu yako, kaka yako dada yako, mjomba wako Mwambie tunahitaji mabadiliko.
Ingia kwenye email yako peleka ujumbe huu kwa watu wengi zaidi ingia kwenye facebook yako na blogu zako weka ujumbe huu utume usambae dunia nzima kwa watanzania wote

PAMOJA NA UCHACHE WETU TWAWEZA KULETA MABADILIKO, PLAY YOUR PART

0 comments:

Post a Comment