Monday, October 11, 2010

Tunaosema tunamwunga mkono Dr. Slaa

Tunaosema tunamwunga mkono Dr. Slaa, hatumwungi kwa vile tunamfahamu au kwa vile tumefanya naye kazi, n.k. lakini tunamwunga mkono kutokana na mambo anayoyasimamia - kupiga vita rushwa, ufisadi, matumizi mazuri ya mapato ya serikali na ujasiri wake wa kuwavaa mafisadi bila woga. Halikadhalika, hatumchukii Kikwete kama yeye, lakini haturidhishwi na sera zake za uchumi kwa kushindwa kuhimili mfumko wa bei, kushindwa kulinda thamani ya shilingi, kuamini kuwa nchi yetu inaweza kuendelea kwa kuomba omba badala ya kujenga misingi ya uchumi, kufanya urafiki na mafisadi, kushindwa kusimamia matumizi sahihi ya makusanyo ya serikali, kuruhusu matumizi ya anasa kwa watendaji wa serikali yake, n.k. Wale wanaomwunga mkono watuambie kuwa si kweli kuwa mfumko wa bei umependa chini ya utawala wa Jk, shilingi haiporomoki, n.k. Mijadala yetu ikisimama katika misingi hiyo, itakuwa ni ya kujenga na kuelimishana.

0 comments:

Post a Comment