Saturday, October 2, 2010

TAMWA yaonya wagombea wanawake wasinyanyaswe

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya , amesema wagombea wanaume ambao wanatoa lugha za matusi kwa wagombea wanadhihirisha kuwa hawana hoja wala sera za maendeleo na hawafai kuwa viongozi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana, Nkya alisema baadhi ya wanaume ambao wanaona wagombea wanawake ni tishio kwao, hivyo wanatafuta mbinu chafu za kuwachafulia ikiwa ni pamoja na kejeli na kuwadhalilisha kwa matusi.

Alisema wanawake kadhaa wanaogombea ubunge majimboni wamelalamikia baadhi ya wanaume wapinzani wao kwamba wamekuwa wakiwatukana na kuwakejeli baada ya kubaini kuwa wagombea hao wanawake wanakubalika katika majimbo yao.

Aliyataja majimbo ambayo wagombea wanaume wamelalamikiwa kutumia lugha za matusi dhidi ya wagombea wanawake ni pamoja na jimbo la Kawe (Dar es Salaam) na Kwimba (Mwanza) na kubainisha kuwa Sheria ya adhabu ya mwaka 2002, kifungu cha 89 kifungu kidogo cha kwanza (a), kinasema kuwa mtu yeyote akitoa lugha ya matusi kwa mtu mwingine ni kosa na adhabu yake ni miezi sita jela.

Hata hivyo, alieleza kuwa miongoni mwa sifa hizo ni uadilifu ( si fisadi), maono, dhamira, ubunifu, upeo wa mambo, ufahamu wa matatizo ya wananchi na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi na kutetea maslahi yao na taifa lao, jumla ya wanawake 190 wanagombea ubunge majimboni mwaka huu.

TANZANIA DAIMA

0 comments:

Post a Comment