Matokeo yaanza kutangazwa - ZANZIBAR/PEMBA |
TUME YA UCHAGUZI IMEBORONGA
Tuandikie marafikiwachadema@gmail.com
Zifuatazo ni mbinu zitakazotumika kuiba kura kesho na zimeanza kutumika mkoani Shinyanga!!!
1.0 Mabalozi wote wa nyumba 10 na viongozi wa serekali za mitaa wanaitwa, wanapewa karatasi 2 za kupigia kura zilizo na vema tayari kwa mgombea wa kijani. Karatasi moja ni ya mume na moja ni ya mke wake. Kesho kila mmoja atakapoingia chumba cha kupiga kura atatakiwa achukue karatasi ingine (ya awali atakuwa kaificha). Akisha piga kura, atadumbukiza kwenye sanduku karatasi zote mbili. Hivyo mjumbe mmoja atapiga kura 2 na mkewe/mumewe kura 2. Jumla 4
Chadema wafanyeje kudhibiti hali hii??? Waweke daftari ambalo kila anaeingia anaandika namba kuanzia 1 hadi mtu wa mwisho. Baada ya kuhesabu kura, zitakazozidi zitakuwa ni zile zilizochakachuliwa!!!!!
Kama itawezekana, kila mpiga kura akaguliwe idadi ya karatasi atakazotumbukiza kwenye sanduku la kupigia kura. Else, wawakague watu kabla hawajawapa karatasi za kupigia kura, kujiridhisha kwamba, hawana vibomu/videsa vya ziada.
Its serious vikao vinaendelea kutimiza azma ya kupiga kura kwa design hiyo, japo maeneo yaliyolengwa ni yale yenye upinzani wa kweli. Mf. Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Mwanza na Mara. DSM inaogopwa sababu ya mwamko na kusambaa kwa taarifa sababu ya teknologia!!
2. Mbinu ya pili ni kutoa karatasi za kupigia kura zisizo na muhuri sambamba na zenye muhuri wa tume ya uchaguzi, ambapo karatasi zisizokuwa na muhuri zitachukuliwa kuwa batili kwa sababu hazijapigwa muhuri wa NEC.
Chadema wafanye nini hapa!!! Kila mtu anapofika kupiga kura, mawakala wapitie kila karatasi anayopewa mpiga kura kuhakikisha kwamba karatasi anayopewa mpiga kura ina muhuri sahihi.
3. Kuchakachua kura zikiwa njiani kwenda kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo!!! Kwenye sheria za NEC na taratibu za internal control (Sarbanese Oxley Act), hapa kuna leakage. Hakuna anaeweza kuthibitisha kuto kuchakachuliwa kwa masanduku ya kura njiani kwakuwa mawakala hawana uwezo kusindikiza kura hizo!!!
Naomba kuwashirikisha mbinu hizo chafu kutokea Shinyanga!!! Hali si hali
Mungu awalinde na kuwabariki, awawezeshe nyote kupiga kura kwa umakini na kwa amani na kumpata Raisi wa kutuongoza kwa kipindi kijacho cha miaka mi tano mwenye hekima, akili, busara na hofu ya Mungu ndani yake!!!
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Said Mwema amewaomba wananchi kuwa na ushirikiano katika kukataa kushawishiwa ama kuhusishwa katika uvumi, fujo au vurugu zozote zinazoweza kuingiza nchi kwenye machafuko yasiyo ya maana yoyote.
Aidha Mkuu huyo , amesema kuwa amani na usalama na utulivu hapa nchini vitadumishwa wakati wote kabla na baada ya uchaguzi, kwa kuhakikisha kwamba sheria , kanuni na taratibu za nchi zinafuatwa ipasavyo.
“Tukumbuke kwamba vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa sheria, kabla na baada ya uchaguzi ni uhalifu.Sheria haina udhuru, inachukua mkondo wake mara moja endapo ukiukwaji umefanyika. Hivyo kutii sheria na taratibu za uchaguzi ni wajibu wa kila mpiga kura na kila mwananchi,” alisema Mwema.
Aliongeza kuwa baada ya kura kupigwa na zoezi hilo kufungwa rasmi, hatua inayofuata ni kuzichambua na kuzihesabu ili kupata matokeo, hivyo huo ndo wakati wananchi wanatakiwa kuwa na subira, kwa sababu zoezi hilo ni muhimu na linapaswa kuendeshwa kwa umakini wa hali ya juu ili, haki itendeke na kuepusha malalamiko.
Mkuu huyo alisema baada ya matokeo kutangazwa ni muhimu kutambua kwamba aliyeshinda ndiye aliyepigiwa kura nyingi na watu wengi.
“Wote tunawajibu wa kumkubali , kumtambua na kushirikiana naye ili kumsaidia kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa watu wote,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarouk Abdulwakil aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi au udini kuendelea kuwa na msukumo wa utaifa na kuacha maslahi binafsi ili amani, usalama na utulivu vidumu kabla ya baada ya uchaguzi.
Alisema wizara yake inawahakikishia wananchi kwamba nchi itakuwa katika hali ya amani, usalama na utulivu wakati wote huku, hivyo alisisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi .