Showing posts with label Washindi 2010. Show all posts
Showing posts with label Washindi 2010. Show all posts

Monday, November 15, 2010

Mbunge wa jimbo la Mbulu Mustapha Akonay




Mbunge wa jimbo la Mbulu Mustapha Akonay

Mbunge wa jimbo la Mbeya kwa chama cha CHADEMA,Mh.Joseph Mbilinyi

Mbunge wa jimbo la Mbeya kwa chama cha CHADEMA,Mh.Joseph Mbilinyi akila kiapo hivi karibuni ndani ya jengo la Bunge,wakati mchakato wa kuapishwa Wabunge wateule ukiendelea.Picha kwa hisani ya Richard Mwaikenda.

Wednesday, November 10, 2010

WABUNGE WATEULE VITI MAALUMU WA CHADEMA

Tume ya Uchaguzi imetangaza nafasi 104 ya wabunge wa viti maalumu kwa mgawanyo wake wa kuweza kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge. Hivyo baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo CCM imejizolea viti 65, CHADEMA kimepata viti 23 na CUF kimepewa viti 10.

Katika bunge lililopita kulikuwa na Viti maalumu 75 ambapo CCM ilikuwa ina viti 58, CUF viti 11 na CHADEMA viti 6. Viti vingine 6 vimeachwa wazi vikisubiri matokeo ya majimbo 7 ambayo uchaguzi wake haukufanyika.

Yafuatayo ni majina ya wanaopewa nafasi kutajwa kuwa wabunge wateule kutoka CHADEMA.

MAJINA YA WABUNGE WATEULE 23
WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NI:

Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza, Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.

Wengine ni Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha na Rachel Mashishanga.

Tuesday, November 2, 2010

WASHINDI WA UBUNGE CHADEMA 2010 - 2015

  1. Halima James Mdee -Kawe/Chadema
  2. Tundu Lissu - Singida Mashariki/Chadema
  3. Mustapha Quorro Akonaay- Mbulu/Chadema
  4. Israel Yohana -Karatu/Chadema
  5. John Mnyika -Ubungo/Chadema
  6. Silinde David -Mbozi Magharibi/Chadema
  7. Salvatory Naluyaga Machemuli-Ukerewe/Chadema
  8. Ole Sambu -Arumeru Magharibi/Chadema
  9. Joseph Mbilinyi -Mbeya Mjini/Chadema
  10. Philemon Ndesamburo Kiwelu-Moshi Mjini/Chadema
  11. Dk Antony Mbasa -Biharamulo Magharibi/Chadema
  12. Joseph Selasini -Rombo/Chadema
  13. Hezekiah Wenje -Nyamagana/Chadema
  14. Peter Msigwa -Iringa Mjini/Chadema
  15. Freeman Mbowe -Hai/Chadema
  16. Vincent Nyerere -Musoma Mjini/Chadema
  17. Godbless Lema -Arusha Mjini/Chadema
  18. Zitto Kabwe/C -Kigoma Kaskazini/Chadema
  19. Hayness Samson -Ilemela/Chadema
  20. John Shibuda -Maswa Magharibi/Chadema
  21. Meshack Opulukwa -Meatu/Chadema
  22. Sylvester Kasulimbayi Mhoja-Maswa Mashariki/Chadema
  23. Regia Mtema / Chadema
  24. Prof Mlambiti /Chadema

JOHN SHIBUDA - MASWA MAGHARIBI

Mh. John Magale Shibuda (pichani) na Silvester Kasulumbayi wametangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi kuwa wabunge wa maswa magharibi na mashariki kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu.

PETER MSIGWA - IRINGA MJINI


MGOMBEA wa chama cha Demokrasia na maendeleo ( Chadema) jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amevunja ngome ya CCM mkoa wa Iringa baada ya kuwabwaga vibaya wapinzani wake katika matokeo ya ubunge baada ya kujizolea kura 17742 dhidi ya kura 16916 alizopata mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Monica Mbega ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

ZITTO KABWE - KIGOMA KASKAZINI

Zitto Kabwe kwa tiketi ya CHADEMA amelitetea jimbo lake la Kigoma Kaskazini

GODBLESS LEMA - ARUSHA MJINI

Pichani ni Mbunge mteule wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Godbless Lema akiwa anaondoka katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge akiwa anasindikizwa na wanachi pamoja na wapambe wake. Mh. Lema amepata kura 56, 569 dhidi ya Dk. Batilda Burian wa CCM aliepata kura 37,460. Picha na Woinde Shizza

JOHN MNYIKA - UBUNGO

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hivi sasa ni kwamba Mgombea Ubunge kwa jimbo la Ubungo na Naibu katibu mkuu kupitia chama cha CHADEMA,Bwa.John Mnyika ametangazwa rasmi kuwa ndiye Mbunge mteule wa jimbo hilo.

FREEMAN MBOWE - CHADEMA HAI

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ameshinda uchaguzi Jimbo la Hai na kurejea bungeni tena kama mbunge baada ya kuwa nje kwa miaka mitano.