Thursday, November 11, 2010

YAH: USHAURI KUHUSU KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI

Dear Dr.Slaa

Natumaini haujambo na pole udharimu wa CCM dhidi ya kura zako na wagombea ubunge wabunge wa chadema.Mimi nimesikitika sana na matukio ya kifisadi yaliyofanywa na CCM na wagombea wake naamini Mwenyezi Mungu atatuonyesha njia iliyo nyooka kuelekea ukombozi wa taifa hili.

Hata hivyo hatuwezi kubeza hata mafanikio tuliyopata ya chama chetu hasa kwa kuweza kupata viti 22 bungeni na pia kupata Halmashauri kadhaa ambazo zitaongozwa na chadema. Na tunategemea hatutalala tutaendelea kupambana hadi kieleweke.

Leo ninaomba kutoa ushauri wangu kuhusu uteuzi wa kiongozi wa kambi ya upinzania ambaye kwa hakika anatarajiwa kutoka chadema.Ushauri wangu kwako Dr.ni kwamba ingekuwa busara zaidi kama chama kitaacha nafasi hiyo kwa wabunge wapya lakini wenye uzoefu kazini, tunaamini kuwa kama chama kitaangalia kiongozi kwa kutoa nafasi ya kwanza kwa wabunge waliotoka mikoa ambayo kwa mara ya kwanza imetoa wabunge kupitia chadema.

1. Mkoa wa shinyanga umeongoza kwa kutoa wabunge wengi wa upinzani kupitia chadema ni bora wananchi wangepewa motisha kwa chama kuteua kiongozi wa kambi ya upinzani kutoka huko.mapendekezo ni Prof.Kahigi ateuliwe kuongoza kwani ni msomi na mzoefu katika masuala ya kiutawala. Hii itaamsha chachu ya upinzani mkoani shinyanga

2. Mkoa wa Mwanza umeweza kutoa wabunge watatu wa chadema kwa mara ya kwanza kama ilivyo kwa shinyanga ni changamoto kwa chadema kuhakikisha kuwa wanazingatia uteuzi kwa kuangalia the big two(shinyanga na mwanza) interms of population, ni mikoa yenye wakazi zaidi ya milioni 7.Mheshimiwa wenje ameonyesha kuwa ni mpiganaji wa kweli hasa kwa kuweza kusimama kidete na kumwangusha kigogo aliyetumia vibaya madaraka kutaka kumwangusha WENJE.

3. mKOA WA SINGIDA UNA HISTORIA YA AINA YAKE KWANI KWAMARA YA KWANZA umeweza kutoa mbunge wa upinzani kwa tiketi ya chadema.Ni vema Tundu LISSU akapewa nafasi ya kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kupitia chadema

Nimeamua kutoa mapendekezo haya ili kukifanya chama kiwe na damu changa katika uongozi bungeni Chadema wasiangalie vigogo ndani ya chadema kuwa ndiyo wagombee nafasi, ni vema wakaangalia wabunge wapya ili kuweza kupata changamoto mpya na kuweza kuibua vipaji vipya lazima chama kiwe kama ACADEMY YA KUTOA VINGOZI WAPYA KILA WAKATI KISITEGEMEE VIGOGO KILA WAKATI inabidi chadema wawaenzi wanchi waliowaletea wabunge wapya kuliko kuendelea kukumbatia wazamani

Natumaini Dr.slaa ATAZINGATIA USHAURI HUU ILI kukiimarisha chama na pia kuepuka migogoro

0 comments:

Post a Comment