Showing posts with label Mjue Dr Slaa. Show all posts
Showing posts with label Mjue Dr Slaa. Show all posts

Monday, October 11, 2010

Ziara ya Mgombea Urais wa CHADEMA-Dr.Willibrod Peter Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini

Ziara ya Mgombea Urais wa CHADEMA-Dr.Willibrod Peter Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini

Katika Kata Kumi za Jimbo la Kigoma Kaskazini

Tarehe:10-10-2010

Mkutano wa Kumi na Tatu wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kata ya Mwandiga

Mkutano wa Kumi na Tatu wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kata ya Mwandiga2

Mkutano wa Nne wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kata ya Mkigo-Kijiji cha Nyarubanda

Mkutano wa Pili wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kata ya Mwamgongo-Mapokezi

Mkutano wa Nne wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kata ya Mwamgongo

Mkutano wa Kwanza wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kuondoka Kagunga

Mkutano wa Kwanza wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Baada ya Mkutano-Kagunga

Mkutano wa Kwanza wa Dr.Slaa Jimbo la Kigoma Kaskazini-Kagunga-Baada ya Mkutano

Wednesday, October 6, 2010

Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Nimelala nimekesha, jambo nimefikira
Bongo nimezichemsha, sipati jibu sawia
Hivi kweli Umekwisha Uzalendo Tanzania?
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Ona walivyoziuza, rasilimali za mtanzania
Kwa kweli inashangaza, mikataba waloingia
Kisha tukiwauliza, hawana la kutwambia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Rushwa imekuwa ngao, kumdhulumu raia
Ubinafsi kwao nguo, vazi la kujivunia
Hizi ndizo sera zao, katu hawajui njia
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Wananchi amkeni, haki kujitafutia
Mtalala mpaka lini?, saa imeishawadia
Uwongo ukataeni Waache kuwatania
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mkipiga kura zenu, chagueni mwenye nia
Waonesheni wanenu, muelekeo na njia
Fanyeni vitu vyenu, tuiokoe Tanzania.
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Mchagueni Slaa, kiboko cha Mafisadi
Huyu bwana hana njaa, atatwanga wakaidi
Ni kiongozi shujaa, si mtumwa wa itikadi
Mchagueni Slaa, tuiponye Tanzania

Tuesday, September 28, 2010

MAMBO 10 KUHUSU DR W P SLAA

Dk. Willibrod Peter Slaa

1. Anachokisimamia

Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, umakini na uwajubikaji katikaü uongozi wan chi na utendaji serikalini.
Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzaniaü wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk. Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya DK. Slaa kielimu na Kitaaluma

Dk. Slaa ana shahada na atashahada zifuatazo.
Sharada ya Uzamivu (PhD) katika Sheriaü ya kanisa kutoka Chuo kikuu cha St. Urban, Rome.
Stashahada ya Theolojiaü kutoka Kipalapala Seminari.
Stashahada ya falsafa kutoka Kiboshoü Seminari.
Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa chaü Macho.


4. Mafanikio ya Dk . Slaa kikazi na kitaalamu

Dk. Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:
Mkurugenzi Mtendaji, Chama chaü Wasioona Tanzania, 1992 – 1998
Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzaniaü (TEC), 1985 – 1991
Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 19977ü – 1979 na 1982 – 1985
Padri wa Kanisa Katoliki kuanzia 1977 hadiü 1991

5. Vitabu alivyoandika

Utimilifu wa Msichana (1977)ü
ü Utimilifu wa Mvulana (1977)
Expediency and Exigency Liturgical Legislationü (1981)

6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk. Slaa anajua kuzungumza na kuandiak ligha nane za kimataifa zifuatazo:
Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk. Slaa Kisiasa

Dk. Slaa ana uzoefu wa musa mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo.

Mbunge wa karatu kwa miaka 15 kutoka 1995 hadi 2010

Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa
Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998 – 2002

Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuuü wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk. Slaa KItaifa na Kimataifa

Dk. Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo.

Mjumbe w akuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika,ü Carribean na Pcific-FU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996 – 2000.

Mjumbe kamatiü ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998ü hadi 2010

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge la SADC(Interü Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010.

Nibu kiongozi wa kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

Mwenyekiti Kamati ya Hesabu za SErikali za Mitaa, Bunge la Tanzania 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

Dk. Slaa amekuwa mbunge wa karatu kwa miaka 15 mfululizo.
Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye maafanikio makubwa ikiwamo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii, Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka 15 ya ubunge wa karatu kwa ajili ya taifa zima.

Ndiye katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijengaü CHADEMA kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kafsha za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.

10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa
Kuanzisha mchakato wa kuandikisha upya katiba nadni ya siku 100 baada ya kuunda serikali.



Kupambana naü kuwashughulikia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha
zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bore naü cha kisasa, chenye faida na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha na kuuza mazao mbalimbali.

Kuhakikisha kuwa kilaü mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika ngazi zote.

Kuanzishaü utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa umri 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya pensheni kwa wastaafu.

Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa misharara inapanda kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda

Saturday, September 25, 2010

CHAGUA DR SLAA - CHAGUA CHADEMA

Dk. Wilbroad Slaa




Mgombea wa ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Karatu,mchungaji Israel Yohana Natse akihutubia maelfu ya wananchi wa mjini Karatu.




Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.


Sunday, September 5, 2010

Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod Peter Slaa

Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Dk Willibrod Peter Slaa

Dk Willibrod Peter SLAA

1. Anachokisimamia

• Dk Slaa anasimamia maadili, uadilifu, uamakini na uwajibikaji katika uongozi wa nchi na utendaji serikalini.

• Dk. Slaa anaamini kuwa Watanzania wanaweza kuleta mabadiliko wanayoyataka wakipata uongozi bora na thabiti.

2. Kuzaliwa, elimu ya msingi na sekondari

Dk Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika Wilaya ya Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965. Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

3. Mafanikio ya Dk Slaa Kielimu na Kitaaluma

Dk Slaa ana shahada na stashahada zifuatazo

• Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome

• Stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari

• Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari

• Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho

4. Mafanikio ya Dk Slaa Kikazi na Kitaalamu

Dk Slaa amefanya kazi katika maeneo na sehemu mbalimbali. Baadhi ya nyadhifa alizoshika na kazi alizofanya ni hizi zifuatazo:

• Mkurugenzi Mtendaji, Chama cha Wasioona Tanzania, 1992-1998

• Katibu Mkuu, Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), 1985-1991

• Mkurugenzi wa Maendeleo (Jimbo Katoliki la Mbulu), 1977-1979 na 1982-1985.

• Padri wa Kanisa ikatoliki kuanzia 1977 hadi 1991.

5. Vitabu alivyoandika

• Utimilifu wa Msichana (1977)

• Utimilifu wa Mvulana (1977)

• Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981)


6. Ufasaha katika lugha nane (8)

Dk Slaa anajua kuzungumza na kuandika lugha nane za kimataifa zifuatazo: Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

7. Uzoefu wa Dk Slaa Kisiasa

Dk Slaa ana uzoefu wa muda mrefu katika shughuli za kisiasa. Baadhi ya nyadhifa alizoshika ni hizi zifuatazo:

• Mbunge wa Karatu kwa miaka 15, kutoka 1995 hadi 2010

• Katibu Mkuu wa CHADEMA, 2002 hadi sasa

• Makamu Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, 1998-2002

• Mjumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu wa CHADEMA kutoka 1995 hadi sasa

8. Uzoefu wa Dk Slaa Kitaifa na Kimataifa

Dk Slaa ana uzoefu mbalimbali kitaifa na kimataifa kama ifuatavyo

• Mjumbe wa kuwakilisha Bunge la Tanzania katika Bunge la Afrika, Carribean na Pacific-EU (ACP-EUC Joint Assembly), 1996-2000

• Mjumbe Kamati ya Uongozi (ACP-EU Joint Assembly)

• Mjumbe katika Bunge la SADC kutoka 1998 hadi 2010

• Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la SADC (Inter Parliamentary Cooperation and Capacity Building Committee) kutoka 1998 hadi 2010

• Naibu Kiongozi wa Kamati ya Upinzani Bungeni, 2006-2010

• Mwenyekiti, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Bunge la Tanzania, 2008-2010

9. Mafanikio kisiasa na kiutendaji

• Dk Slaa amekuwa mbunge wa Karatu kwa miaka 15 mfululizo. Karatu ni moja ya wilaya hapa nchini zenye mafanikio makubwa ikiwemo miundo mbinu bora, maji na huduma nyingine za kijamii. Dr. Slaa anataka kutumia uzoefu wake wa miaka

15 ya ubunge wa Karatu kwa ajili ya taifa zima.

• Ndiye Katibu Mkuu aliyefanikiwa zaidi kuijenga CHADEMA. Kwa kushirikiana na viongozi wengine ameweza kuipitisha CHADEMA katika changamoto mbalimbali na kukifanya kuwa chama kilicho tayari kushika uongozi wa taifa.

• Bila kujali vitisho vya watawala aliibua rasmi kashfa za ufisadi mbaya kuliko zote zilizowahi kutokea hapa nchini zikihusisha wizi wa fedha za umma katika Benki Kuu. Madai yake mazito Bungeni yalimlazimisha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini kutoroka nchini.


10. Baadhi ya vipaumbele vya Serikali itakayoundwa na Dk Slaa

• Kuanzisha mchakato wa kuandika upya Katiba ndani ya siku 100 baada ya kuunda serikali

• Kupambana na kuwashughulia mafisadi katika nafasi zote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha zote zilizoibwa zinarejeshwa na wahusika wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

• Kuhakikisha kuwa kilimo chetu kiwe bora na cha kisasa, chenye faida na kinachofikia viwango vya kimataifa katika kuvuna, kuhifadhi, kusafirisha na kuuza mazao mbalimbali.

• Kuhakikisha kuwa kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora katika ngazi zote.

• Kuanzisha utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote wenye umri wa miaka 60 na kuendelea nchi nzima na kurekebisha mfumo wa malipo ya pensheni kwa wastaafu

• Kuanzisha utaratibu mpya wa upandaji mishahara kwa watumishi wa umma na wa sekta binafsi utakaohakikisha kuwa mishahara inapanda kadri gharama za maisha na mfumuko wa bei unavyopanda.

Chagua Mabadiliko,

Mchague Dk Slaa ili arudishe tunu za taifa letu: Uzalendo, Maadili, Uadilifu na Umakini.

Dr. Slaa ni Mlei

Dr. Slaa ni Mlei

Dr. SlaaKwa muda mrefu sasa vyombo mbalimbali vya habari na watu binafsi wamekuwa wakieneza habari kuwa Dr. Willibrod Slaa ni Padre wa Kanisa Katoliki na kuwa kwa vile aliwahi kuwa Padre (Kuhani) ndani ya Kanisa hilo ina maana kuwa hadi leo hii yeye ni Padre kama walivyo mapadre wengine. Wengi wanaosema mambo haya wanaonesha kutokujua au hata kujaribu kujua mafundisho ya Kanisa Katoliki juu ya Upadre na jinsi gani mtu anaweza kuwa Padre na akauacha na kuwa Mlei kama Walei wengine.

Kanisa Katoliki linazo Sakramenti saba ambazo ni Ubatizo, Kipaimara, Komunio (Ekaristia), Upatanisho (Maungamo), Ndoa, Upadrisho (Ukuhani) na Mpako wa Wagonjwa. Sakramenti hizo saba zipo ambazo zinatolewa mara moja tu kwa mtu na nyingine ambazo zaweza kurudiwa. Tunaposema "kutolewa mara moja" maana yake ni kuwa mtu anapopatiwa uwezo na nguvu za kuanza kupokea neema za sakramenti hizo hilo hufanywa mara moja tu na hairudiwi tena (isipokuwa kama hakuna uhakika kuwa alishapokea mara hiyo ya kwanza). Hizi ni Ubatizo, Kipaimara na Upadrisho. Zingine ni zile ambazo mtu anapokea mara ya kwanza lakini katika maisha yake ya kila siku anarudia kupokea mara kwa mara kwa kadiri inavyohitajika. Hizi ni Ekaristia na Maungamamo japo nazo huanza kupewa mara moja tu na kutoka hapo ni kuendelea kuchota neema zake kwa taribu zinazotakiwa. Na zipo ambazo hufanywa upya kabisa kama vile hazijawahi kufanywa kabisa; hizi ni ndoa na mpako wa wagonjwa.

Siyo kusudio letu kuelezea Theolojia ya sakramenti hizo ila tunataka kuzungumzia hili ambalo linaonekana kuwashindwa watu kuelewa. Ni kweli Dr. Slaa alipewa Sakramenti ya Upadrisho ndani ya Kanisa Katoliki baada ya kumaliza maandalizi yake ya kazi hiyo. Upadre siyo kama kazi nyingine ambazo mtu "anasomea"; si sawa na Udaktari, Uwakili au Uhasibu. Upadre ni Sakramenti ya Ukuhani ambayo mtu anaandaliwa kuiingia na kuitumikia. Ndio maana kimsingi kabisa, hata mtu ambaye hajasomea kabisa mambo ya Theolojia na Filosofia anaweza akapewa Upadrisho. Lakini kwa miaka mia nyingi Makanisa (Mashariki na Magharibi) yamekuwa yakiwaandaa wale wanaotaka kuingia katika "Daraja Takatifu" kwa mafunzo maalum ya mambo ya dini, falsafa, utawala n.k Ukiondoa mafunzo ya Theolojia ya Katoliki mafunzo mengine ya Falsafa, utawala, au elimu nyingine yoyote ni sawa kabisa na mafunzo yanayotolewa katika vyuo vikuu vingine.

Mtu akishapata daraja ya Ushemasi na baadaye Upadre basi anakuwa ni "Kuhani Milele" na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kufanywa kuondoa daraja hilo. Hii huitwa "alama isiyofutika". Ni alama ile ile ambayo inapatikana katika Sakramenti ya Ubatizo na Kipaimara ambapo mtu akishabatizwa ubatizo wake hauwezi kurudiwa tena kwani alama hiyo ya neema haifutiki. Ni kwa sababu hiyo mtu ambaye ameshawahi kupata upadrisho ataendelea kuwa kuwa na alama hiyo milele.

Kuwa na daraja hilo katika nafsi haina maana mtu ni mhudumu wa altare tena yaani kuhani. Hivyo, mtu anaweza kuamua kuacha kabisa kazi ya upadre, akaamua kuasi, au akaamu kujiunga na dini nyingine au kutoamini kabisa uwepo wa Mungu, lakini ile alama haifutwi na milele anabakia nayo. Kwa maana hiyo, Padre wa Kikatoliki anaweza kuacha, kufukuzwa, kuachishwa kazi za kila siku za kutoa huduma ya Upadre lakini bado anabakia kuwa ni padre moyoni. Hivyo, mtu huyo aliyeacha hastahili kuitwa "Padre X" kwa maana ya mapadre ambao bado wako kwenye huduma. Ni sawa na Daktari aliyeacha kazi ya Udaktari au kufukuzwa Udaktari au Uwakili lakini bado mafunzo na uwezo wa kutoa huduma hiyo akawa bado anao japo haruhusiwi tena kufanya hivyo. Wapo watu ambao kutokana na mazoea wataendelea kumuita "Daktari" japo hafanyi tena huduma hiyo.

Jambo hili ni muhimu kulielewa. Mtu ambaye ameacha yeye mwenyewe upadre bila kurejeshewa hali yake ya ulei (yaani uumini wa kawaida) kwa mujibu wa taratibu za Kanisa basi mtu huyo bado ni Padre na haruhusiwi kupewa Sakramenti ya Ndoa. Hata hivyo, Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kumfanya mtu aliyewahi kuwa padre kurejeshwa kwenye hali ya ulei (yaani kuondolewa kabisa kazi na haki ya kufanya kazi za upadre na kuwa muumini wa kawaida kabisa). Mtu ambaye ameondolewa upadre kwa utaratibu wa Kanisa na kibali cha Vatikani anaondolewa haki na majukumu yote ya mapadre wengine isipokuwa mambo mawili tu yaani useja (celibacy) na kusikiliza maungamo ya mtu aliyekaribu na kifo.

Hilo la useja linahitaji kibali kingine kuondolewa ili aruhusiwe kuoa. Hata hivyo kwa vile padre ni padre milele basi mtu aliyewahi kuwa Padre anaweza kusikiliza maungamo na kutoa msamaha kwa mtu ambaye yuko katika hatari ya kifo tu.

Mfano mzuri wa kuelewa hili ni aliyekuwa Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro huko Paraguay. Askofu Lugo alitaka kuingia katika siasa kitu ambacho kinakatazwa na Kanuni za Kanisa Katoliki. Askofu Lugo aliomba Kanisa Katoliki limruhusu arejee katika hali ya Ulei ili aweze kushiriki katika siasa lakini Kanisa lilimkatalia lakini Lugo aliendelea kugombea na aliposhinda uchaguzi Mkuu wa Paraguay Kanisa Katoliki lilikubali kumuondolea Upadre wake na kumrejesha katika Ulei. Hivyo, Rais wa sasa wa Paraguay ni Askofu wa zamani wa Kanisa Katoliki ambaye alirejeshwa katika Ulei.

Hii ina maana ya kwamba, Dr. Slaa siyo tu ni mlei lakini anayo haki kama wakatoliki wengine walei kushiriki katika nafasi ya uongozi kwani hajavunja sheria yoyote ya Kanisa, wala hajaenda nje ya haki zake za kikatiba. Dr. Slaa sasa hivi ni muumini Mlei kama wengine na atakapoamua kupata sakramenti nyingine yoyote ya Kanisa ataweza kufanya hivyo kwa uamuzi wake yeye mwenyewe kwani alifuata taratibu za kanisa za kurejeshwa katika maisha ya mlei.

Hivyo, Dr. Slaa siyo mtumishi wa Kanisa Katoliki na siyo padre kwa maana ya kuwa anahaki na majukumu yote ya mapadre wengine. Yeye ni muumini Mlei ambaye kutokana na nafasi yake ya kuwa aliwahi kuwa padre anabakia na haki za waumini wengine walei ndani ya kanisa hilo na vile vile uwezo wa kusikiliza maungamano ya mtu aliye katika hatari ya kifo TU.

Thursday, August 26, 2010

Huyu Ndio Dr.Willibrod Peter Slaa

Jina la Dr.Willibrod Peter Slaa (pichani),Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Karatu, hivi sasa linaweza kuwa jina ambalo linatajwa zaidi kushinda lingine lolote katika anga za kisiasa nchini Tanzania.Wananchi wengi wanamuongelea kama kiongozi shujaa,aliye tayari kudiriki kufanya au kusema chochote katika kutetea maslahi ya wananchi hususani wale wanaoitwa “wa kawaida” na wenye hali duni za kimaisha.Angekuwa anaishi katika nchi za magharibi,Dr.Slaa angeitwa “whistleblower” nambari wani jina ambalo hupewa mtu anayeamua kuwa mkakamavu na kukemea mienendo mibaya na isiyofaa ya watu walioko kwenye madaraka fulani nk, potelea mbali kinachoweza kumtokea kutokana na ujasiri huo.

Kwanini jina la Dr.Wilbrod Slaa liwe vinywani mwa watanzania wengi hivi sasa?Jibu ni rahisi;ni kutokana na mchango wake katika kufichua “ufisadi” uliokuwa unafanyika katika Benki Kuu ya Tanzania(BOT) na mambo mengi mengineyo ambayo anahisi yanakwenda visivyo.

Ingawa umaarufu wa Dr.Slaa haujaanzia na suala la BOT,ni wazi kwamba sakata hili ndilo limefanya jina lake liwe miongoni mwa majina maarufu sio tu kutoka kambi ya upinzani bali katika anga za wanasiasa kote nchini Tanzania.

Lakini Dr.Slaa ni nani?Anatokea wapi?Wangapi wanafahamu alikuwa akifanya nini kabla hajaingia kwenye siasa? Tangu ameingia kwenye siasa amepata mafanikio gani? Anasemaje kuhusu sakata zima la BOT?Ameridhika na maamuzi yaliyochukuliwa na Rais Kikwete?Ana ujumbe gani kwa wananchi?Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo, hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano rasmi.Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Dr.Slaa karibu sana ndani ya www.bongocelebrity.com. Ni heshima kwetu kupata nafasi hii ya kufanya nawe mahojiano.Jambo la kwanza kabisa ambalo tunaamini wasomaji wetu wangependa kujua ni kuhusu historia yako. Je, unaweza kutueleza ulizaliwa wapi,lini,ukasomea wapi mpaka kufikia hadhi ya udaktari wa falsafa?

WS:Historia fupi, nilizaliwa Kwermusl, Mbulu, Tanzania, tarehe 29.10.1948.Lakini ili kukidhi haja ya swali hili zima,labda tuambatanishe CV au BIODATA yangu kama ifuatavyo;

CURICULUM VITAE(BIODATA)

Full Name: Willibord Peter Slaa.

Date and Place of Birth: 29.10.1948,Kwermusl,Mbulu,Tanzania.

EDUCATION:

PRIMARY: 1958-1961 Kwermusl

1962-1965 Karatu Middle School.

SECONDARY: 1966-1969 Dunguyi Seminary

1970-1971 Itaga Seminary

PHILOSOPHY:

1972-1973 Kibosho Seminary

THEOLOGY:

1974-1977 Kipalapala Seminary

1974-1976 Makerere University,Diploma,Theology

HIGHER EDUCATION:

1979-1981 Pontifical Urba University,Rome,JCD(summa cum laude)

1980-1980 ADV.Diploma-Socio-Political Studies,Koln,Germany(KAF)

1981-1981 St.Thomas Aquinas University,Rome,AD.Diploma Rural Development

1985-1985 London COR.College, Principles and Practice of Management Certificate.

WORK EXPERIENCE:

2000-Todate Member of Parliament(MP),Karatu

1995-2000 Member of Parliament(MP),Karatu.

1991-1995 Executive Director,Tanzania Society for The Blind.

1986-1991 Secretary General,Tanzania Episcopal Conference(TEC)

1982-1986 Development Director,Diocese of Mbulu

1982-1986 Vicar General,Diocese of Mbulu

1977-1979 Development Director,Diocese of Mbulu (Catholic Priest 1977-1991)

MEMBERSHIP IN LOCAL AND INTERNATIONAL BODIES

2006-Todate: Deputy Leader,Official Opposition, Parliament of Tanzania

2000- Todate: Vice President, Forum of African Parliamentarians on Education( FAPED)

2004-Todate: Secretary General,CHADEMA.

2001-Todate: Member,Special Education Committee,MOEC/SADC.

2000-Todate: Shadow Minister,Legal and Constitutional Affairs.

1998-2004 Vice Chairman,CHADEMA

1998-2003 Chairman, Inter-Parliamentary Forum (SADC-PF)

1996-2000 Member,ACP-EU Joint Parliamentary Assembly

1994-Todate: Chairman,Comprehensive Community Based Rehabilitation Tanzania (CCBRT)

1992-1995 Secretart,National Prevention of Blindness Programs,MOH

1992-1995 Director,SLS General Trading Co.Ltd

INTERNATIONAL CONFERENCES

Attended numerous national and international conferences and workshops,presented papers and facilitated in a number of them including,IPU,SADC-PF and CPA organized workshops and conferences.

Attended numerous short courses and seminars both within and outside the country.

BC: Wanasiasa wengi wanasema kwamba waliingia kwenye siasa baada ya kukerwa na mambo fulani fulani wanayokuwa wanahisi hayaendi sawa kijamii,kisiasa au kiuchumi.Kama maelezo hayo yanafanana na historia yako kwenye siasa,ni jambo au mambo gani yalikufanya uingie kwenye siasa?Na tangu umeingia umeweza kuleta mabadiliko gani mpaka hivi sasa?

WS: Niliingia kisisasa mwaka 1995, bila kuwa na nia kabisa ya kuingia kwenye uongozi hasa ubunge japo kwa nafasi mbalimbali nimeshiriki shughuli za Kisiasa huko nyuma. Nimekuwa Katibu wa TANU Youth League nikiwa Kipalapala Seminary, na kufungua matawi mengi ya TANU wakati huo. Nimekuwa Katibu wa Shina la CCM, Tawi la Mambo ya Nje, Rome wakati nasoma Rome, 1980-81.

Niliingia kugombea ubunge baada ya Wazee wa Karatu kunifuata Dar-Es-Salaam, wa vyama vyote vilivyokuwepo wakati ule-CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi. Nikaombwa nichague chama ninachokipenda, na kama ilivyokuwa kwa kila mmoja wakati ule nikaingia kupitia CCM. Nikashinda kwenye Kura za Maoni ndani ya CCM, lakini jina liliondolewa kimizengwe, kwa msingi kuwa “mimi si mwenzao”. Leo ninaelewa kilichomaanishwa, ni kweli kwa hali hii ya ufisadi mimi sikuwa mwenzao”. Sijutii kabisa, kuwa baada ya hapo niliingia Ubunge kupitia Chadema, nafasi pekee iliyokuwa wazi wakati huo. Sikuijua Chadema, sikuwa namfahamu Mzee Mtei, wala Katiba ya Chadema. Nadhani ni Mungu aliongoza hivyo kwa sababu anazofahamu mwenyewe, kwa wale wanaomwamini Mungu.

Jambo kubwa pekee lililokuwa linawakera Wananchi wa Karatu na kuja kuniomba ni : Maji. Karatu ni wilaya isiyo na mto hata mmoja wala maziwa yanayoweza kutumika na binadamu, japo tuna Lake Manyara upande wa Mashariki -Kusini na Lake Eyasi upande wa Magharibi. Wamekuwa wakiomba wapate miradi ya maji kwa miaka 30 lakini licha ya kuchangishwa mara kadhaa miradi hiyo ilishindikana kabisa. Kulikuwa pia na suala la Elimu hasa ya Sekondari na pia matatizo ya Huduma za Afya. Haya ndiyo mambo ya msingi kabisa waliyoomba kwangu wananchi wa Karatu wakitaka niwatangulie na kuwa wako tayari kufanya kazi nami katika hali na mali.

a) Nilipoingia tu, japo sikuwa na diwani, na mwenyekiti mmoja tu wa Kijiji kwa Tiket ya Chadema, na sikuwa na kitongoji hata kimoja, nilifanikiwa kupata msaada mkubwa wa maji kwa ajili ya mji wa Karatu na vijiji vitano vinavyoizunguka vya Ayalabe, Gongali, Gyekurum Arusha, Gyekurum Lambo, na Tloma kupitia shirika la MISEREOR la ujerumani kupitia Diocese of Mbulu, (Katoliki) ambao kwa muda mrefu nimekuwa nikifanya nao kazi na kujenga kuaminiana sana.

Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana, kwani mradi huo uliwekewa mizengwe ya kila aina, mbinu za kutaka kuukwamishwa kutumia Katibu Tarafa, Mtendaji wa Kata, watendaji wa Halmashauri.

Hata hivyo, baada ya mapambano makali, kwa kushirikiana na Wananchi na bila Serikali ( ya Wilaya) nilifanikiwa kukamilisha mradi huo mwaka 2000. Siku maji yalipotoka wananchi waliomba dua, walisherehekea, na kuamini kumbe inawezekana. Kuanzia siku hiyo nimeendelea na kutafuta mbinu mbalimbali kupata miradi ya maji kwa ajili ya Wilaya nzima, na hadi leo, vijiji 35 vimepata maji ya uhakika ya Bomba hadi ngazi ya Kitongoji. Kazi iliyobaki ni ya usambazaji hadi karibu na wananchi, kupeleka DP kwa ukaribu wa mita 400 au chini ya hapo kufuatana na sera ya maji ya nchi, na kuingiza maji ndani (Domestic). Pia tumefanya jitihada ya kujenga mabwawa kadhaa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.

b) Kutokana na maendeleo hayo ambayo yalionekana dhahiri, Wananchi wa Karatu waliichagua Chadema mwaka 2000 na kuifanya CCM kuwa chama cha Upinzani. Yaani Mwenyekiti wa Halmashauri na wenyeviti wa Kamati zote wanatoka Chadema, kutokana na uwingi wa Chadema. Pia katika uchaguzi uliofuata wa Serikali za mitaa 2004, Chadema sasa ina vijiji vingi na vitongoji vingi vinavyoongozwa na Chadema. Wazo hili la CCM kuwa chama cha Upinzani limekuwa gumu sana kueleweka na CCM na serikali yake, hivyo wameendelea kuhujumu Serikali ya mitaa inayoongozwa na Chadema, lakini kwa kuwa tumekuwa imara na tumeendelea kuwa karibuni na wananchi, majaribio hayo yote yameanguka kwenye mwamba wa jiwe.

c) Kwa upande wa Elimu, mwaka 2000 Wilaya ya Karatu ilikuwa na shule moja tu ya wananchi, yaani AWET Sekondari. Lakini kwa Ilani na sera nzuri ya Chadema, tunapoongea leo, Wilaya ya Karatu inayo shule za Sekondari 25, na 3 ziko kwenye hatua ya mbalimbali ya ujenzi. Wakati Sera ya CCM ni shule za Sekondari katika ngazi ya Kata, Sera na Ilani ya Chadema Karatu ni kuwa na Sekondari katika ngazi ya kijiji, kwa vile Kata nyingi bado ni kubwa na shule za kata ni za kutwa hivyo zinakuwa mateso kwa watoto wetu. Zaidi ya nusu ya vijiji tayari vina shule za vijiji za Sekondari. Chadema kwa hili imetoa changamoto kwa Serikali ya CCM. Isitoshe, mwaka huu, 2008 watoto wote wanaotakiwa kuingia Sekondari waliotimiza vigezo, wameingia Sekondari, na bado tuna nafasi tupu 800 yaani tuna madara 20 zaidi kuliko watoto. Kitaifa watoto waliofaulu ni asilimia 51 wakati Karatu waliofaulu ni 54. Tatizo la msingi ni kuwa Serikali kuu inasua sua katika kutekeleza majukumu yake, mathalan upatikanaji wa waalimu ni tatizo kubwa, vifaa vya elimu na hata vitabu.

d) Huduma za Afya nayo ni eneo moja ambapo Chadema tumeonyesha njia. Sera na Ilani ya Chadema ilikuwa kujenga zahanati kila kijiji. Hadi leo ni vijiji 5 tu bado havina zahanati, na vijiji vyote au vimekamilisha ujenzi au viko kwenye hatua ya kumalizia ujenzi. Kutokana na changamoto hiyo, Serikali ya CCM pia sasa imetangaza bila kuwa na sera hiyo ujenzi wa Zahanati katika ngazi ya Kijiji kwa nchi nzima. Tatizo hapa ni Madaktari na manesi ambao ni jukumu la Serikali Kuu na upatikanaji wa uhakika wa madawa.

e) Jambo ambalo mara nyingi linafanyiwa porojo ni kuondoa manyanyaso ambayo wananchi walikuwa wanayapata wakati wa mfumo wa chama kimoja. Chadema Karatu tulipiga vita unyanyasaji wa aina yeyote. Mathalan, michango mingi isiyo ya kisheria inakusanywa kwa mabavu na kuwaumiza wananchi wa chini. Chadema tulipiga marufuku hayo. Ndipo Serikali ya CCM bila kujiandaa ikafuta kabisa kilichoitwa kodi ya Maendeleo. Kwa bahati mbaya walikurupuka bila kuandaa na wala kufanya “alternatives”, na sasa Serikali za mitaa ziko kwenye hali ngumu kujiendesha, na pia kuanzisha dhana mpya ya watu kutolipa kodi ya aina yeyote kabisa.Chadema tulipopiga marufuku kodi za manyanyaso tulitafuta vianzio visivyo na athari kwa mwananchi wa kawaida, wala visivyo na athari kwa uchumi mpana.

f) Miundo mbinu na kilimo ni eneo muhimu ambalo tumeweka mkazo kwa lengo la kupiga vita umaskini kabisa miongoni mwa watu wetu. Mikakati yetu ya kilimo, na jitihada za kutafuta vianzio vyetu vya fedha nje ya vile vya Serikali Kuu imeongeza sana fanaka katika mipango yetu mbalimbali.

BC: Tukiwa hapo hapo kwenye suala la historia yako.Wengi tunatambua kwamba siku za nyuma kabla hujaingia kwenye siasa ulikuwa padre au ulisomea upadre. Unaweza kutueleza kwanini uliacha upadri na kuwa mwanasiasa? Ulifukuzwa au uliacha kwa hiari? Una mke na watoto. Je, kanisa lilikuruhusu kuoa?

WS: Ni kweli nimekuwa Padre wa Kanisa Katoliki. Nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu sana ndani ya Kanisa kuanzia Jimboni kwangu ambapo nimekuwa Makamu wa Askofu, na Mkurugenzi wa Maendeleo, lakini pia nimekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu toka 1985 hadi 1991. Ni kweli hayo maswali yanaulizwa mara nyingi, kwa bahati mbaya si wengi wanaofahamu taratibu za kisheria ndani ya Kanisa Katoliki. Niliondoka mimi mwenyewe katika Upadre bila kushinikizwa na yeyote, wala kufukuzwa, wala hata kupewa onyo. Ni kweli kuna mambo ambayo mimi niliyakataa na kwa dhamira yangu nisingeliweza kuendelea, lakini nadhani hayo ni binafsi zaidi, na si mahali pake kuyaeleza. Nimetoka kwa kibali cha Kanisa, kwa utaratibu wa kisheria wa Kanisa Katoliki, ndiyo maana mimi sina tatizo wala ugomvi wa aina yeyote na Kanisa Katoliki na ninashiriki katika shughuli mbalimbali za Kanisa.

Nina Mke na watoto wawili, Emiliana Slaa na Linus Slaa, japo sijafunga ndoa kikanisa kwa utaratibu wa kawaida wa Kanisa Katoliki, pamoja na kuwa sina kipingamizi chochote kufanya hivyo kikanisa, ni uamuzi wangu na wa mke wangu na familia yetu.

BC: Baada ya mkutano wako wa hadhara pale MwembeYanga jijini Dar-es-salaam Septemba mwaka jana,vyombo vya habari karibuni vyote vilihofia kuandika ulichokisema na pia kuweka bayana orodha ya majina uliyoyataja.Unadhani kwanini vyombo vya habari viliogopa kufanya hivyo? Na wewe binafsi ulijisikia vipi kuona hali hiyo? Tukio lile lilimaanisha nini kwako kuhusiana na suala zima la uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania?

WS: Nilijua kabisa kuwa vyombo vya Habari vinaogopa kuandika aina ya taarifa tuliyotoa na wenzangu pale Mwembe Yanga, hivyo sikushangaa. Nilifurahi sana nilipoona Gazeti dogo la Mwanahalisi, limethubutu, siyo tu kuandika majina na tuliyoeleza bali pia kuweka na picha yao. Tafsiri pekee ni kuwa vyombo vingi vilikosa ujasiri na uzalendo. Vilipenda kujilinda zaidi wasishitakiwe, wengine nao pia hawakuamini tuliyoyasema kama ni kweli na wala hawakwenda mbele zaidi kufanya utafiti wao kuthibitisha tulichosema. Hivyo, kuna mengi yanaweza kusemwa kuhusu vyombo vya habari na uhuru wa vyombo vya habari hapa Tanzania. Hali ni mbaya zaidi, unapokuta kuwa vyombo vingine vinamilikiwa na wanasiasa na hasa pale wamiliki wa vyombo hivyo wanapoguswa kwa namna moja au nyingine na tuhuma hizo.

Waandishi wa habari na vyombo vya habari ni muhimu sana katika ukombozi wa aina yeyote. Wanahitajiwa kuwa na ujasiri, kwani bila hivyo watakosa thubutu ya kwenda kwenye mstari wa mbele wa vita au mapambano kuripoti kinachojiri kama tulivyoona kwa waandishi wa CNN. Nampongeza sana Bwana Kubenea aliyejitosa, na kwa hakika ni shujaa wa kweli, na gazeti hilo dogo limeonyesha njia, naamini na mengine yatafuata njia.

BC: Baadhi ya wananchi,hususani kwenye kambi ya upinzani, wamekuwa wakihofia usalama wa maisha yako.Wengine wamekuwa wakitoa mapendekezo kwamba serikali haina budi kukupa ulinzi wa ziada. Je,wewe mwenyewe unahofia usalama wa maisha yako?Kama jibu ni hapana,kwanini?

WS: Ni kweli hisia hizo zipo na wengi wamenipa ushauri wa aina mbalimbali. Nawashukuru sana kwa kunipenda na kunijali. Hata hivyo, hatima ya yote, Usalama utatolewa tu na Mwenyezi Mungu. Tukumbuke kuwa John Kennedy ameuawa akiwa amezungukwa si tu na maaskari wa ulinzi bali pia na CIA na FBI. Wako waliokufa wamezungukwa na madaktari 30 au zaidi, lakini saa yao ilipofika waliondoka bila kuaga. Ninaacha Maisha yangu kwa Mwenyezi Mungu. Ninachukua tahadhari zote zinazoweza kuchukuliwa na binadamu, lakini kamwe sitaacha kufanya wajibu wangu, na kile ambacho dhamira yangu inataka nikifanye kwa kuhofia usalama na maisha yangu. Hatukuomba kuzaliwa na hatutaomba kuondoka humu duniani.

Kambi ya upinzani;kutoka kushoto kwenda kulia,Mwenyekiti wa TLP,Augustine Lyatonga Mrema,Mwenyekiti wa CUF,Prof.Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,James Mbatia na Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr.Willibrod Peter Slaa.Anayeonekana nyumba kwa mbali katikati ya Mrema na Lipumba ni Maalim Seif Hamad,Katibu Mkuu CUF.

BC: Watu wengi wamejitokeza hadharani na kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wa kutengua ajira ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu,Daudi Balali.Pamoja na hayo,kumeibuka maswali kadha wa kadha kuhusu maneno kama “utenguzi wa ajira” nk. Tungependa kukuuliza maswali mawili juu ya hili.Kwanza,kwa mtazamo wako,Raisi amefanya kile ambacho ulikitegemea?Pili nini hasa maana ya maneno haya (utenguzi wa ajira) kwa jinsi ulivyoelewa wewe na pia kisheria?

WS: Ni wazi kabisa, msimamo wangu unajulikana na umenukuliwa na magezeti kadhaa:

1) Sijaona kabisa sababu ya kupongeza hatua ya Rais.Kwanza muda uliochukuliwa ni mrefu sana. Jambo hili limejenga matabaka katika nchi yetu. Kwa sheria iliyoko leo, ukituhumiwa unakamatwa, unapelekwa polisi, unawekwa lock up-au unapata mdhamana ambao ni haki yako isipokuwa kwa makosa fulani fulani tu. Lakini kwa tuhuma ya uwizi mkubwa masharti yanajulikana, mathalan kuchukuliwa kwa Passport yako ili usiweze kutoroka, kuweka mdhamana wa mali isiyohamishika kwa kiwango kilichowekwa na sheria nakadhalika, na uchunguzi unafuata baadaye. Hii ndiyo sheria ilivyo leo ( Sheria inayoenda Bungeni inabadilisha kidogo hali hiyo, uchunguzi unatangulia kabla ya kukamatwa). Haya yote hayakufanyika kwa mtuhumiwa wa Mabilioni, tena yaliyothibitishwa na wakaguzi, lakini ameaachwa ana tamalaki tu. Hi si ishara nzuri na wala si utawala bora kutengeneza matabaka kati ya wananchi wake Rais.

2) Hatua ya “kutengua” maana yake Dr.Balali bado ni mfanyikazi wa Serikali, ila tu uteuzi wake au nafasi yake kama Gavana imeondolewa. Wala Rais hajasema kama amesimamishwa kazi au vipi. Angalau basi Balali alitakiwa kusimamishwa kazi Serikalini na wakati Tuhuma zake zinapelekwa mahakamani. Lakini hilo halikufanyika, na kwa msingi huo inawezekana kabisa Balali anaendelea kupokea mshahara kamili, kwa vile hajasimamishwa utumishi wake Serikalini. Isipokuwa kama tutaelezwa vinginevyo, kwa taarifa tuliyonayo Balali ni mtumishi wa Serikali kabla ya kuwa Gavana, na utumishi huo haujasimamishwa.

3) Sijaridhika kabisa na hatua ya Rais, kwa vile, Tuhuma dhidi ya Balali nilizotoa Mwembe Yanga zinaenda zaidi ya Kasma “Vote” moja ya EPA ndani ya BOT.Ziko votes nyingi na ubadhirifu umetapakaa kwingi, kwa mfano fedha zilizolipwa Alex Stewart aliyekuwa anapata 1.9% ya Royalty yetu -ambayo ni 3%. Huu ni mkataba wa ajabu na kama kweli ilifanyika kihalali basi hii ni biashara kichaa kwa maelezo yeyote yale. Suala la malipo kwa Kampuni ya Mwananchi Gold Co halijaelezwa na wala Rais hajalieleza Taifa hatua gani za ziada zinaendelea kuchukuliwa, suala DEEP Green Finance Co halijaelezwa popote ambapo fedha za Umma toka Hazina/BOT zaidi ya 20 Billioni zimepelekwa kusikojulikana, ila kuna ushahidi wa kimazingira kuwa zilipelekwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 kuisaidia CCM. Na mengine mengi tuliyoyasema Hizi zote ni fedha za Umma, na Rais hana mamlaka ya kuamua kutoa au kutotoa Taarifa kwa Umma. Ndiyo maana ninaendelea kushinikiza kuwa Tuhuma za Ubadhirifu bado mbichi na hatua zilizochukuliwa hazikidhi kabisa kwa kiwango chochote. Kwa bahati mbaya Watanzania wengi hawaelewi na hivyo wanaridhika tu na kidogo alichokifanya Rais. Tutampongeza Rais atakaposafisha uozo huu wote.

4) Rais alitakiwa kuwasimamisha vile vile wale wote waliohusika na uozo huu. Nimesema mara nyingi kuwa Balali si peke yake katika ubadhirifu na ufisadi huu. Wale wote wanatakiwa kuchukuliwa hatua.Tunaendelea kudai hawa wote wachukuliwe hatua akiwemo Gray Mgonja, ambaye pamoja na yote tuliyosema, anaendelea kuwa Mjumbe wa Bodi ya BOT kwa kofia yake ya kuwa Katibu Mkuu, Hazina. Ni muhimu Rais amwondoe, ili Katibu Mkuu mwingine aingie na kusaidiana na Gavana mpya kusaifisha nyumba. Vinginevyo tunatwanga maji kwenye kinu. Rais ameagiza Bodi ya BOT iwachukulie hatua wahusika wote, ni kweli hafahamu kuwa Gray Mgonja, aliyesaini nyaraka nyingi tu hahusiki kweli, hata kwa uzembe tu? Kama hajui basi tunatatizo kubwa zaidi kuliko tunavyofahamu na tunavyotaka kujiaminisha. Kwa hali hiyo basi ni dhahiri kuwa alilofanya Rais silo nililotegemea wala silo lililotegemewa na Watanzania wengi waelewa wa mambo.

BC: Hivi karibuni umekuwa ukilalamikia suala la serikali kutoiweka hadharani ripoti ya EPA kama ilivyowasilishwa serikalini na kampuni ya Ernst & Young.Unadhani kuna umuhimu gani kwa serikali kuiweka ripoti hiyo hadharani?

WS: Kuweka au kutoweka hadharani kwa Ripoti hiyo siyo hisani ya Rais wala ya Serikali. Jambo lolote lililofanyika kwa Kodi ya Wananchi linapaswa kufikishwa kwa wananchi hasa kama linahusu Tuhuma.

Kwanza serikali yenyewe ilitoa ahadi Bungeni kuwa itawekwa hadharani, kwa wananchi na kwa Wabunge. Itakuwa ajabu kama hata Wabunge hawatapewa. Itakuwa Serikali ya ajabu ambayo haiheshimu ahadi na kauli zake. Waziri Meghji naye pia aliahidi mara nyingi kuwa Taarifa ya Ernst and Young itatolewa hadharani leo kulikoni? Hii hatua ya sasa inazua utata mkubwa, kuna nini kinafichwa?

Pili taarifa hiyo ni muhimu kwa umma wa Watanzania kuona hasa nini kimeandikwa na nani anahusika. Nina sababu nzito ya kuamini kuwa viongozi wa Serikali waliosemwa katika Taarifa hiyo wameachwa nje, na ndiyo maana Serikali inapata kigugumizi katika kuweka Taarifa nzima hadharani. Hili haiisaidii Serikali bali inazidi kuichafua.

Ningependa kuamini Serikali imepata fundisho kwa jinsi ilivyoshughulikia suala hili, na sasa itakuwa makini zaidi, lakini inaelekea wenzetu hawa fundisho bado halijawaingia hata kidogo, na bado wana mawazo ya zamani kuwa Serikali inaweza kufanya inavyotaka. Serikali inayowajibika kwa Wananchi, inapaswa kuwa wazi (Transparent and Accountable). Tuko mbali sana na mambo hayo mawili ambayo ni msingi mkubwa sana wa Good Governance.

BC: Tofauti na hapo zamani,siku hizi taarifa zinasambaa kwa haraka sana.Shukrani kwa maendeleo ya kisayansi na kitekinolojia.Unadhani nini kitatokea katika miaka kumi ijayo kama kasi ya kupeana habari na kuwasiliana itaendelea kukua kwa kasi hii.Wewe binafsi unadhani tekinolojia imekusaidia vipi katika kufanikisha shughuli zako za kisiasa mpaka hivi sasa?

WS: Ni kweli teknolojia imesaidia sana. Hata hili unalofanya wewe ni msingi mkubwa sana katika kupeleka Taarifa kwa watu wengi zaidi. Hili lisingeliwezekana miaka takriban 10 iliyopita. Ninafurahi sana kwa maendeleo haya. Bunge la Tanzania lilipitisha, kupitia Miscellaneous Ammendement sheria kutambua Taarifa zinazopatikana katika Internet, lakini hatimaye Spika wa Bunge akapinga. Nadhani kuna haja kubwa viongozi wetu au kusoma na kupitia maamuzi ya nyuma. Viongozi wengi wanakosa Consistency kwa kusahau waliyoaumua wenyewe, au kupindisha tu sheria makusudi. Kama tunahitaji kwenda mbele ni lazima tuwe jamii yenye principles zisizoyumba na kubadilika badilika kama kinyonga.

BC: Sasa tungependa kukuuliza kuhusu chama cha CHADEMA.Wewe ukiwa kama katibu mkuu wa CHADEMA,unaweza kutueleza chama chenu kina visheni gani kwa taifa? Kama CCM imeshindwa, CHADEMA kinaweza kuwa chama mbadala? Kwa vipi?

WS: Misimao ya Chadema inajulikana wazi katika maswali mbalimbali. Ni dhahiri kuwa CCM imeshindwa kabisa kupiga vita Rushwa, Taifa kwa dhahiri limekosa mwelekeo katika mambo mengi, na CCM na Serikali yake hawataki kusikia, ili kujipongeza tu na miradi kama MMEM na MMES, ambayo kimsingi wala si sera yao ( imetokana na maamuzi ya Kimataifa ya kama vile MMEM na MMES ambayo yalifanyika Jomtien, Thailand, mwaka 1990). Hata hivyo, hatujatekeleza maamuzi hayo kama yalivyokubaliwa yaani EFA. Lakini CCM na Serikali zake kila siku wamekuwa wakijisifu bila kueleza chimbuko halisi la maamuzi hayo. Ndiyo maana hata upatikanaji wa fedha umekuwa rahisi kwa kiasi kikubwa. Mimi nimekuwa Makamu Mwenyekiti wa Afrika wa Wabunge wanaojishughulisha na Elimu, hivyo ninayafahamu kwa undani masuala haya.

Dr.Willibrod Slaa(katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wake,Freeman Mbowe(kushoto) na Zitto Kabwe,mbunge machachari wa Kigoma Kaskazini kupitia CHADEMA.

BC: Kumekuwepo na habari ambazo zimesambaa mtandaoni zikidai kwamba ndani ya CHADEMA pia kuna kashfa za ufisadi. Shutuma hizo zimekuwa zikielekezwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA na pia wewe mwenyewe.Unasemaje kuhusiana na shutuma hizi?

WS: Ni kweli kumekuwepo na taarifa kama hizo. Siwezi kumjibia Mhe. Mbowe, japo ninamfahamu Mwenyekiti wangu sasa kwa kiasi kikubwa. Na sijawahi kuona wala kushuhudia kinachosemwa. Hata hivyo:

Kwanza kusema au kutoa maoni ni haki ya watu wote. Tofauti ni kuwa hao wanaotoa maoni yao ni ya umbeya, au yanaushahidi kama sisi tunavyofanya? Mimi sina tatizo kama kuna tuhuma dhidi yangu ningelifurahi tu, zitolewe hadharani bila kificho na kwa ushahidi kamili.

Tuhuma zingine zinazoelekezwa Chadema kama za matumizi ya Helicopter, msingi wake tunaufahamu, na tusingelipenda kuwanufaisha watani zetu. Yatosha tu niseme hapa ni kweli, sisi tulikopa fedha kwa Mwenyekiti Mbowe kufanya kampeni zetu. Tuliweka taarifa zetu hadharani. Tukatoa changamoto kwa CCM watoe walipata wapi fedha zao hawajasema hadi leo. Swali la kujieleza, sisi tumekopa kwa Mwenyekiti wetu fedha za Helikopta, na tunamlipa kwa utaratibu uliokubalika kwa mujibu wa taratibu zetu.

Kwa ushahidi uliopo CCM kampeni wamefanya kwa fedha zetu, za Watanzania zilizochotwa BOT, Tangold, Meremeta kupitia DEEP GREEN, sasa nani bora? Nadhani mengine ni propaganda, na watu walidhani hatuna details ya tunayosema. Ninaendelea kui challenge CCM imepata wapi fedha za Kampeni na sources zao zilikuwa nini? Fedha zote zilizochotwa kupitia Deep Green Serikali na CCM lazima wazieleze zilienda wapi? Isitoshe, tulipoanza kutoa tuhuma, ni kwanini CCM walianza kuwakingia kifua watuhumiwa badala ya kuwaacha wajibu wao na au Serikali, lakini Katibu wa CCM anahusika vipi na tuhuma, kama dhamira yake haimsuti kuwa amegunduliwa na ndiyo taharuki ya kujibu hata yasiyomhusu na mwisho kuishia kwenye porojo na propaganda badala ya kujibu hoja?

BC: Ni kiongozi gani duniani anayekuvutia kutoka na jinsi anavyoongoza taifa au jamii yake?Kwanini?

WS: Kwa kuwa sijalifanyia utafiti naomba nisilijibu suali hili.

BC: Tukiachana kidogo na masuala ya siasa,unapokuwa mapumzikoni(tunaamini kwamba hufikia wakati ukahitaji mapumziko)huwa unapendelea kufanya nini?

WS: Nikiwa mapumzikoni mimi hupenda

1) Napenda sana kusoma vitabu mbalimbali vya Sheria, Siasa, maendeleo na hata Novels za kawaida.

2) Kujikumbusha lugha mbalimbali nilizojifunza nikiwa masomoni kama vile Kiitaliano, kijerumani, ili nisije nikazisahau.

3) Kutazama TV.

4) Kufanya shughuli za kawaida na kuzungumza na wapiga kura wangu jimboni.

BC: Mwisho una ujumbe gani kwa watanzania?

WS: Ningependa Watanzania watambue kuwa nchi ni yetu sote. Watanzania katika ujumla wetu ndio wenye nchi, Rasilimali zote za nchi ni zetu sote, na viongozi tumewapa tu dhamana ya kuzilinda kwa niaba yetu. Hivyo, tusiruhusu kabisa wakati sisi tunatumbukia kwenye lindi la umasikini wengine wananufaika kwenye migongo yetu. Kulinda mali zetu, ni jukumu la kila mmoja wetu pale alipo, kwa uwezo alionao na ufahamu wake. Ufisadi uko ngazi zote hadi vijijini tuukatae katakata popote pale. Rushwa tuikatae sote, na Mtanzania hata siku mmoja asikubali kununua haki yake iwe mahakamani, polisi, au hospitalini au popote pale ambapo huduma ni haki yake.

BC: Dr.Slaa,asante sana kwa muda wako.Tunakutakia kila la kheri katika shughuli zako.

WS: Shukrani sana,mimi pia nawatakieni kila la kheri.