Friday, October 15, 2010

ELIMU KWA MPIGA KURA

Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (sura ya 343) 30 Juni 2010 inatuelekeza nini?
7(5) Kila msimamizi wa uchaguzi na msaidizi wake wataapa kiapo cha kutunza siri mbele ya hakimu.
[ni siri gani hii wakati uchaguzi ni huru na wa haki?]
35C (3) Tume inawezakutoa maelekezo na kuweka masharti ambayo mtu anaweza, katika siku ya uchaguzi wa Rais, kuruhusiwa kupiga kura katika kituo cha kupiga kura mbali ya kile alichopangiwa
[wanafunzi wa vyuo ambao hawajafungua vyuo wanaruhusiwa kisheria kuchagua Rais nje ya vituo walivyopangiwa]
35F (6) Tume inaweza, kama kuna shaka kuhusu usahihi katika kujumlisha kura za Rais katika jimbo lolote kurudiwa au kwenye baadhi ya vituo au vyote
[shaka hii inatokea wapi?]
35F (8) Mshindi wa Urais ni atakayepata kura nyingi zaidi ya kura zote halali zilizopigwa.
[kigezo cha kura halali ni kipi?]
35G (1) Uchaguzi kurudiwa kama hakuna mgombea aliyepata kura nyingi zaidi ya kura halali zilizopigwa.
[kipimo cha wingi au uchache wa kura ni kipi? Mbona Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 iliyorekebishwa chini ya aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali Andrew Chenge inasema mwenye kura nyingi zaidi ndio mshindi]
Kufungana kwa kura nyingi zaidi; waliofungana kuingia kwenye uchaguzi kwa mara ya pili
[Kipimo cha wingi wa kura ni kipi?]
61 (4) Ndani ya kituo, kabla au baada ya kupiga kura, mpiga kura anaweza kutoa malalamiko yake
[wapiga kura tutumie fursa hii]
63 (2) (l); 72 (1) (e); 80 (6) (f) moja ya watu wanaoruhusiwa ndani ya kituo cha kupigia kura ni askari polisi au mtu mwingine yeyote anayehusika na usalama katika kituo cha kupigia kura
[huyu mwingine anayehusika na usalama na sio askari polisi ni nani, green guard, JWTZ, KK security, Mgambo?]
67 (1) Ghasia au vurugu, upigaji kurakuairishwa mpaka siku ya pili
[je, huu sio mwanya wa CCM kwa kutumia green guard kuvuruga uchaguzi na wizi wa kura? Nani atalinda kura ambazo zimekwisha pigwa?]
70A (2) Kama kuna ufinyu au dalili za kituo kuwa na usalama mdogo wakati wa kuhesabu kura, masanduku yatapelekwa kwenye nafasi na usalama kwa ajili ya kuhesabu kura
[hapa ndio masanduku uchanganywa na yale ya bandia?]
72 (2) Wapiga kura wakisha piga kura wanatakiwa kuwa mbali na kituo cha kuhesabu kura
[umbali gani?]

Wakala wa upigaji kura amebeba dhamana kubwa ya taifa ili kuliingiza kwenye ‘mwanga’ au ‘giza’
57 (1-4) wakala wa upigaji kura uchaguliwa na chama cha siasa kwa ridhaa ya mgombea
[Vyama pinzani mmekwisha fanya ili]
70 (1) kila wakala wa upigaji kura au wakala wa upigaji kura mbadala aliyeteuliwa na wakala wa chama cha siasa kwa mujibu wa kifungu cha 57 cha sheria hii, mwisho wa upigaji kura na wakati wa kuhesabu kura, atakuwa wakala wa kuhesabu kura wa mgombea aliyemteua.
[wakala uliyeteuliwa na chama chako unaruhusiwa kisheria kumteua wakala mbadala wakati unapoondoka kituoni aidha kwa dharura au umechoka, vyama vya siasa mtumie fursa hii ya kisheria kuwaondoa mawakala wababaishaji na wasioonekana vituoni]
61 (1) & (2); 69 (1); 70 (1); 73 (1) (a-e); 73 (1-4); 74 (1 -2), 78 (1-2); 79A (1-3); 80 (1-6) kazi za wakala ni:
1. Kutambua wapiga kura
2. Kumwakilisha na Kulinda maslahi ya mgombea au wagombea katika kituo
3. Kuhakikisha sheria za upigaji kura zinafuatwa
4. Kuwepo wakati wa maandalizi ya kufungua kituo ikiwemo kuhakiki vifaa na wakati wa kufunga kituo
5. Atakuwepo wakati wa kuhesabu kura
6. Kabla ya kuhesabu kura atashuhudia uhakiki wa kura zilizopigwa, kufungua sanduku,
7. Kukubali matokeo kwa kuweka sahihi yake na Kushuhudia matokeo yanabandikwa kwenye kituo
[mawakala wa vyama vya upinzani hasa Chadema tunawapa dhamana kubwa ya kuleta maisha bora kwa watanzania wote na vizazi vijavyo kuanzia Nov 2010 kwa kulinda kura na maslahi ya Dr. Slaa na wabunge wa vyama vya upinzani kwa kukataa rushwa kama alivyofanya Askofu Mkiwa au kulitumbukiza taifa letu la Tanzania kwenye utumwa na maisha magumu kuanzia Nov 2010 na siku zote zijazo kwa watoto, wajukuu na vitukuu vyetu kwa kupokea rushwa ambayo haitakumalizia matatizo yako na ya ukoo wako na jamaa zako na marafiki zako na kukubali kura za Dr. Slaa ziende kwa Jakaya Mrisho Kikwete: usijiangalie wewe tu na maisha ya muda mfupi bali angaliamaisha ya watanzania wote wa leo na wa miaka ijayo]
Rai ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame, ni vyama vya siasa vichague mawakala wa upigaji kura waaminifu (The Guardian 12/10/2010)!
Somo ni kwamba mustakabali wa taifa letu upo kwa mawakala wa upigaji kura

0 comments:

Post a Comment