Monday, September 13, 2010

TUNAHITAJI MDAHALO KABLA YA UCHAGUZI MKUU 2010

Nalileta kwenye jukwaa suala la mdahalo wa viongozi wa vyama vya siasa katika ngazi ya rais kwa mwaka huu wa uchaguzi. Tuliona mara ya mwisho mwaka 2000 wakati BBC walipoanda mdahalo kati ya maalim seif wa CUF na Mheshimiwa Karume (CCM).

Mdahalo unawapa fursa wananchi kusikia moja kwa moja toka kwa wagombea katika kunadi sera zao lakini pia kujibu maswali ya wananchi moja kwa moja, tofauti na ziara za viongozi hawa mikoani ambako huwa hawamfikii kila mlengwa ama kukata kiu ya wananchi ambao ndio wapiga kura wakubwa.

Wananchi wakati mwingine hawapati hata nafasi ya kuwaona ama kuwasikia viongozi na wagombea katika nafasi mbali mbali za uchaguzi zaidi ya wawakilishi wao ambao mara nyingi wanakwenda kwa minajiri ya kuwashawishi kuwapigia kura bila kuwaeleza ni namna gani watatua matatizo ya taifa ama wamefanikiwa kwa kiasi gani katika mipango iliyopo.

Mdahalo ni njia mbadala ya kuongea na wananchi kwa kujibu mawali yao na kuwapa nafasi ya kupima sera za vyama vyote kupitia mahojiano ya moja kwa moja. Ni njia pia ya kuwakosoa viongozi moja kwa moja pale wanapotoa ahadi ambazo hazitekelezeki.

Naomba tuchangie hili na namna gani tunaweza kuinfluence lifanyike kwa mwaka huu. Kumbuka kuwa mwaka 2005 Hamza Kasongo akishirikiana na Channel Ten waliamndaa mdahalo ambao ulikuwa ufanyike Agosti 27, 2005 ambapo CUF, TLP, CHADEMA, na NCCR-Mageuzi walikuwa wamekubali kushiriki lakini CCM walikataa kushiriki na hivyo kufanya mdahalo huo kuota mbawa.

Kama kuna chama kinakataa ama kitakataa kushiriki mdahalo huu basi kitatoa nafasi kwa wananchi kuamua kutokana na sababu zitakazokuwa zimetolewa.

NAWAKILISHA

TUNAHITAJI MDAHALO KABLA YA UCHAGUZI MKUU 2010

0 comments:

Post a Comment