Tuesday, October 12, 2010

CHAGUA JOSEPH MBILINYI CHAGUA CHADEMA MBEYA

Mr II atia fora mdahalo wa uchaguzi mkuu Mbeya
Sehemu ya wakaazi wa jiji la Mbeya wakisikiliza mdahalo huo
Mgombea ubunge wa jimbo la Mbeya mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Joseph Mbilinyi a.k.a MR.II akiingia ndani ya ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya kwa ajili ya kushiriki mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Mbeya (MBENGONET) kwa ufadhili wa asasi za kiraia Tanzania,huku akishangiliwa kwa nguvu sana
Mratibu wa midahalo mikoa ya nyanda za juu kusini kutoka asasi za kiraia Tanzania Bw Sisila Ngalemwa (Kulia) akijaribu kuwatuliza wananchi waliofurika katika ukumbi wa Mkapa Mbeya kumsikiliza mgombea ubunge wa Chadema Joseph Mbilinyi a.k.a MR II katika mdahalo huo ulioandaliwa na asasi za kiraia mkoa wa Mbeya (MBENGONET) Vijana wakijitolea kumtoa nje ya ukumbi wa mdahalo mmoja kati ya mashaiki wa msanii Joseph Mbilinyi a.k.a MR II aliyeshindwa kujizuia kushangilia kwa staili ya kutaka kumshika mkono msanii huyo wakati akijinadi mbele ya wananchi katika mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Mbeya mjini. MR.II (chadema)ni mmoja kati ya wagombea watano wa ubunge jimbo hilo.
Wapenzi na mashabiki wa msanii Joseph Mbilinyi a.k.a MR II na wale wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) jijini Mbeya wakiwa wamemzunguka msanii huyu nje ya ukumbi wa Mkapa baada ya kutoka kushiriki mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Mbeya mjini
Picha zote na Francis Godwin

1 comments:

Machu said...

Nini tena mbona chadema.co.tz or chadema.net kuna kwikwi???

Post a Comment