Wednesday, September 8, 2010

John Mnyika



Katika kampeni hizo, nashukuru niliweza kuungana na kiongozi wa kitaifa wa chama changu, CHADEMA. Katibu Mkuu, Dr. Wilbrod. Slaa. Yeye kwa unyenyekevu alisema maneno mazito sana kwa wananchi wa Taifa letu na hususan wana wa jimbo la Ubungo.

"Tupeni MNYIKA, ni mdogo kwa muonekano lakini sisi tunaithamini na kutambua sana kazi yake. Ana mchango mkubwa sana katika demokrasia ya nchi hii. Tupeni kijana wetu huyu aingie bungeni".

Kwa kina maneno mengine ya Rais wetu mtarajiwa waweza fatilia tutakapo weka video ya uzinduzi wa kampeni zangu humu katika blogu siku chache zijazo.



Katika harakati hizo niliungwa mkono na wagombea na wanaharakati wengi sana. Natambua mchango wa Mpendazoe (Mgombea Ubunge, Jimbo la Ukonga), Joseph Mbilinyi aka Sugu (Mgombea Ubunge, Jimbo la Mbeya Mjini).

0 comments:

Post a Comment