Monday, September 27, 2010

CHANGIA HALIMA MDEE CHAGUA CHADEMA JIMBO LA KAWE

Mgombea Ubunge wa jimbo la kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mheshimwa Halima Mdee,aliendelea na mlolongo wa kampeni zake za Ubunge wa Jimbo hilo jumapili tarehe 26,kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara uliojaza umati mkubwa wa watu katika eneo la Tanki bovu,mkabala na baranbara ya Bagamoyo.
Kama kawaida yake Mheshimiwa Mdee,aliwaeleza wakazi hao kuhusu matokeo ya Ufisadi katika manispaa ya Kinondoni na jinsi alivyojitoa muhanga kupambana nayo na kwa ajili ya mustakabali wa wakazi wa jimbo la kawe,hususani kata ya mbezi juu.
Kamanda Halima Mdee ataendelea na kampeni zake katika mbio za ubunge katikati ya wiki kwa kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote kumi na moja za jimbo la Kawe.

Kamnda Halima Mdee akimtambulisha mama yake mzazi kwa wapiga kura wake.

Shughuri zote zilisimama kwa muda,ili kumsikiliza mpiganaji na mkombozi wa wakazi wa Kawe,Mh Halima mdee.

Wapiga Kura wakifuatilia kwa karibu mkutano huu,hii ni sehemu tu ya mwamko wa wakazi wa Mbezi juu na tanki bovu.

Wake kwa waume 2010,Hakuna kulala mpaka kieleweke!

0 comments:

Post a Comment