Tuesday, September 28, 2010

"Tumieni kura kupinga rushwa"

0diggsdigg

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Media,Reginald Mengi

Elizabeth Suleyman na Pill Shaban

VIJANA na Wanafunzi nchini, wametakiwa kutumia silaha yao ambayo ni ‘kupiga kura’ na kuhakikisha wanapambana na viongozi wanaotaka kuingia madarakani kwa kupitia mianya ya kutoa rushwa.

Aidha, wametakiwa kuitumia silaha hiyo, kama chachu ya kutokukubali kurubuniwa na viongozi wala rushwa ambao hawataleta maendeleo ya kweli katika Taifa.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Media, Reginald Mengi wakati akikabidhi hundi ya Sh13 milioni kwa wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri kwenye mitihani yao na kupata daraja la kwanza katika Sekondari Azania.

“Usije ukathubutu kutumia kura yako kuchagua kiongozi mla rushwa.. na baadae akashindwa kuleta maendeleo ukaanza kumlaumu,” alisema Mengi.

Alifafanua kuwa, watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kuangaliana ni nani atakayebeba mzigo wa kutokomezo rushwa, bila kujua kwamba kazi hiyo ni ya wote inayoweza kufanywa kwa kutumia silaha ambayo ni kupiga kura na kuleta mabadiliko.

“Rushwa imekuwa ikiwasumbua Watanzania walio wengi hapa nchini, kila mmoja anasuburi mwingine atokomeze rushwa bila kujua kwamba na yeye anaweza,” alisema Mengi.

Alisema kijana au mwanafunzi endapo atashindwa kuitumia silaha hiyo, kupambana na adui rushwa..na kuchagua Kiongozi anayekula rushwa ..atakuwa ni sehemu ya wanaotoa rushwa na kupokea na ataandikwa kwenye orodha ya daftari la wala rushwa nchini, jambo ambalo ni aibu.

Mengi aliwasisitizia wanafunzi hao kuwa, hata akija mtu kununua kura yako mfukuze na usikubali.. kumpa itakugharimu.

GAZETI MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment