Wednesday, September 15, 2010

DR. SLAA alivyounguruma mjini musoma

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wahadhara wa kampeni, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini Musoma
Mgombea urais wa Tanzaia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akikumbatiana na mbunge wa zamani wa Musoma kupitia CCM, Paul Ndobo, mara baada ya mkutano wa kampeni za mgombea huyo mjini Musoma .
Mgombea ubunge katika jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Vincent Nyerere, akihutubia katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini humo .
Mgombea wa ubunge katika jimbo la Maswa Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Musoma, katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa Tanzaia kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo
Vijana wa kikosi cha ulinzi cha Red Brigade wakisindikiza gari lililombeba mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya mkutano wake wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mukendo mjini Musoma .(picha zote kwa hisani ya Joseph Senga mpiga picha mkuu wa gazeti la Tanzania Daima).

0 comments:

Post a Comment