Quote: Akizungumza wakati wa kutangaza majina ya wagombea wa nafasi ya ubunge na uwakilishi yaliyopitishwa na Baraza Kuu la Uongozi, Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema pamoja na umakini wa Dk. Slaa, lakini amechelewa kutangaza nia yake hiyo na kuwa yeye yuko tayari kupambana na wanaoitafuna nchi.
“Awali Slaa, (Freeman) Mbowe, Dk. (Sengodo) Mvungi, (Augustino) Mrema, wote waliweka bayana kuwa hawatagombea, na sisi kupitia mchakato wetu tukaamua kugombea tukijua kuwa kuna mambo mengi ambayo tunayadai bado hayajatekelezeka na watu wamechoka hususan vijijini ambako sisi ndio tutakwenda,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Slaa ana haki ya kufanya hivyo na Chadema kina haki kumsimamisha.
Slaa ni rafiki yangu, na ninajua kuwa ni mtu makini na aliyefanya mambo mengi mazuri hususan katika Bunge kwa kushirikiana na wabunge wa vyama vingine vya Upinzani, lakini amechelewa kutangaza nia yake.
Namtakia kila la heri. Ila mimi nitasimama kupambana na mapapa, sangara na nyangumi wa rushwa.”
Source: Habari Leo Kwakweli kauli hii imetoka mdomoni kwa mtu makini anayeelewa ni nini anafanya kwa maslahi ya taifa. Kauli ya Lipumba inaashiria kwamba endapo Dr. Slaa angetangaza nia mapema, basi yeye Lipumba angeweza kujitoa ili kumpisha Slaa. Natamani akina MS KN na Tumain waseme lolote kuhusu hili.
WE HAVE MOVED TO/TUMEHAMIA WWW.UDADISI.COM
3 years ago
0 comments:
Post a Comment