Saturday, August 28, 2010

UZINDUZI WA KAMPENI ZA CHADEMA

Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani. Dr Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.

Mgombea Mwenza wa Dr. Willbrod Slaa,Said Mzee akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika katika viwanja vya Jangwani leo.

Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa akimtambulisha rasmi mke wake mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya jangwani,jijini Dar.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akikabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho Mh Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akionesha vitabu vya Ilani ya chama chao mara baada kuizindua leo katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.

Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi waliofika katika viwanja vya jangwani leo.Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.

Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya nyimbo zake ujulikanao kwa jina la ‘Sugu’ ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lisu akiwahutubia wanachama wa Chadema waliofika katika viwanja vya jangwani jioni ya leo huku akiwa ameshika kitabu alichokisema kuwa ni moja ya mikataba ya migodi.

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akijaribu kuwatuliza baadhi Wananchi kuwa wawe na utulivu hakuna kitakachoharibika,Mbowe ilibidi awatulize Wananchi mara baada kubaini kuwa shirika la utangazaji la TBC1 lilikatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kutaka kumpiga mmoja wa watangazaji wa kituo hicho, na baadae TBC1 waliamriwa waondoke uwanjani hapo kwa usalama wao.

Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani leo jioni mara ya kushuka kwenye gari.

Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari ili kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute wakati wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio,hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa na jazba ya tukio hilo waliendelea kulalama mpaka Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe aliposimama na kuwasihii wananchi watulie na amani itawale eneo hilo la jangwani,na kweli baadae hali ikawa shwari na uzinduzi wa kampeni ukaendelea.

maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani leo.

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kawe,Halima Mdee akipitisha bakuri la kuomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali waliofika viwanjani hapo,fedha hizo ambazo imeelezwa kuwa zitatumika kwenye mbio za kampeni ambazo wamezindua leo na wanatarajia kuzianza hivi karibuni Tanzania nzima.

Msanii G- Solo akishambulia jukwaa leo.

Msanii wa Bongofleva Dani Msimamo akiimba jukwaani.

Mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mkoloni ambaye pia ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma lisala fupi kwa niaba ya Wasanii wenzake kuhusiana na mambo mbali mbali yanayoikumba anga ya muziki na wanamuziki wenyewe,Mkoloni baadae lisala hiyo aliikabidhi kwa mgombea Urais wa chama hicho Dr.Willbroa Slaa.

WanaChadema wakiwa juu ya mti ili kuweza kuona na kusikia kila kinachoendelea katika viwanja vya jangwani.

Askari Polisi wakituliza ghasia zilizotaka kuletwa na wanachama wa Chadema katika gari la kurushia matangazo la Television ya Taifa TBC.

Gari la matangazo la TBC baada ya kuwekewa uilnzi ili lisiletewe fujo na wanachama wa Chadema.

Mkutano ukiendelea.

walielekea jukwaa kuu.

gari lililommbeba mgombea urais wa Chadema likiwasili katika viwanja vya jangwani leo.

moja ya vioja vilivyokuwepo katika viwanja vya jangwani leo

umati wa wanachadema leo.


Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando, ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi,Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea wa chama cha CCM,Mh DK.Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.
Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya wimbo wake uitwao wananiita Sugu ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake.
Mwanasheria wa chama cha CHADEMA na mgombea Ubunge wa jimbo la Tabora Mjini,Tundu Lisu akiwasalimia wananchi kwa nguvu.
Baadhi ya Watu wakiwa juu ya mti huku wakisikiliza mambo kadha wa kadha yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wa juu wa chama cha CHADEMA wakati wa uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya Jangwani.
Meza kuu ikiwa katika maombi kabla ya kuanza uzinduzi wa kampeni hiyo
Mwenyekiti mstaafu wa chama cha CHADEMA,Mh Bob Makani (kulia) akiwasili kwenye uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama hicho leo jioni katika viwanja vya Jangwani.
Chadema Oyeeee...! Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho nao wakiwasalimia Wananchi
Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia Wananchi sambamba na Mgombea mwenza (kati) Said Mzee.
Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaaa akisalimiana na Mgombea Ubunge jimbo la Ubungo kwa chama hicho,John Mnyika mara baada ya kuwasili viwanjani hapo huku akilakiwa na shangwe za wananchi waliokuwa wamefika viwanjani hapo jioni ya leo.
Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani leo jioni mara ya kushuka kwenye gari.
Gari la mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa likiwasili katika viwanja vya Jangwani leo jioni huku likilakiwa na wanachama mbalimbali wa chama hicho,kwa madhumuni ya kuzindua rasmi ilani yao ya Uchaguzi mbele ya Wananchi na pia kuzindua mbio za kampeni za chama hicho.

0 comments:

Post a Comment