Thursday, September 2, 2010

Maswali na Majibu

Honourable Dr. Wilbrod Peter Slaa [CHADEMA]
Karatu Constituency
Session No Principal Question No To the Ministry of Sector Date Asked
8 98 FINANCE Finance/Treasury 28 June 2007
Kwa kuwa kwa muda mrefu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali amekuwa akilalamikia matumizi yenye mashaka kwa njia ya vocha zisizo sahihi au zisizo na nyaraka:-

(a) Je, tangu Julai, 2001 hadi Juni 2006 ni kiasi gani cha fedha kimepotea wakati ukaguzi au wakati wa matumizi kutokana na vocha zisizo sahihi kwa Hesabu za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na kati ya fedha hizo ni kiasi gani cha fedha kimethibitika kutumika kwa taratibu za matunzo ya fedha za Serikali na ni kwa sababu gani zemefanya hati zisionekane kabla wakati wa ukaguzi na kupatikana baadaye?

(b) Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya upoteaji wa hati hizo za kutotunzwa vizuri wakti wote wa uandishi, ukaguzi na uhifadhi?

(c) Je, watu wangapi kati ya wahusika wamepoteza hati hizo kwa makusudi au uzembe na wangapi kati ya hao wamechukuliwa hatua kutokana na makosa hayo katika kipindi cha kati ya mwaka 2001 hadi 30 Juni, 2006.

ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #98 SESSION # 8
Answer From Hon. Khatib, Abdisalaam Issa
FINANCE
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Wilbrod Peter Slaa, Mbunge wa Karatu, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu Julai, 2001 hadi Juni, 2005 hoja zilizohusu malipo yasiyo na nyaraka (unvouched expenditure) zilikuwa zenye jumla ya shilingi 13,718,996,927.95 na sasa kiwango hiki kimepungua na kufikia shilingi 43,485,351.00 (sawa na asilimia 0.003 ya kiwango cha awali) baada ya nyaraka husika kuwasilishwa kwa wakaguzi.

Malipo yenye nyaraka pungufu (improperly vouched expenditure) yalikuwa shilingi 80,734,216,390.64 na sasa kiwango hiki kimepungua kufikia shilingi 1,550,059,502.42 sawa na asilimia 0.019 ya kiwango cha awali.

Aidha kuanzia Julai 2005 hadi Juni 2006; malipo yasiyokuwa na nyaraka yalikuwa shilingi 1,319,857,934.00, na malipo yenye nyaraka pungufu yalikuwa shilingi 56,511,145,057.00 ikiwa ni pamoja na kiasi hiki kinahusu bakaa ya shilingi 1,550,059,502.42 ya miaka ya 2001 hadi 2005. Nyaraka zenye jumla ya shilingi 33,709,476,043.00 zimekwishahakikiwa na hoja kufungwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Serikali za Mitaa, hoja zinazohusu vocha zisizo na nyaraka au zenye nyaraka pungufu zimekuwa zikipungua kutoka shilingi 11.66 bilioni mwaka 2000/2001 hadi shilingi 5.26 bilioni mwaka 2005/2006.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kufafanua kuwa malipo haya si malipo yenye hati zisizo sahihi bali ni zenye nyaraka pungufu kutokana na sababu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vocha zisizo na nyarala (unvouched expenditure) zinahusisha malipo yote ambayo hukosa viambatanisho vinavyotakuwa katika kukamilisha malipo husika; kwa upande mwingine vocha zenye nyaraka pungufu (improperly vouched expenditure) zinahusisha malipo yote ambayo huwa na viambatanisho pungufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu kubwa ya mapungufu haya kwa miaka kadhaa sasa ni kutokana na mawasiliano sahihi kati ya Wakaguzi na wakaguliwa. Kwa mfano fedha zinazohusu Maendeleo ya Halmashauri huwa ndani ya Bajeti za Mikoa.

Lakini fedha halisi (funds transfers) kutoka Hazina hupelekwa moja kwa moja kwenye Halmashauri husika bila kupitia mikoani na hivyo Halmashauri hupeleka Hazina stakabadhi ya kukiri kupokea fedha hizo. Nyaraka pekee inayopelekwa Mikoani ni Exchequer Issue Notification inayohusisha fedha za maendeleo zilizopelekwa kwenye Halmashauri.

Hivyo Mkaguzi anapofanya ukaguzi kwenye Mkoa husika akihitaji kuona stakabadhi ya kukiri kupokea fedha hizo ni wazi hataipata na hivyo huandika hoja chini ya malipo yasiyokuwa na nyaraka.

(b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua hatua za makusudi za kuajiri Wahasibu na Wakaguzi wa ndani wenye sifa na uelewa mzuri katika uandishi na uhifadhi wa nyaraka za Serikali.

Aidha Serikali inazidi kuimarisha Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kwani ndivyo venye majukumu ya kuhakikisha mapungufu kama hata hayatokei. Vile vile Serikali itaendelea kutoa adhabu kwa Afisa yeyote atakayebainika kupoteza fedha na mali za umma zikiwemo nyaraka za malipo kama Kanuni za fedha zinavyoelekeza.

(c) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka ya 2001 hadi 30 Juni, 2006 hakuna kumbukumbu ya Afisa yeyote aliyepoteza nyaraka za malipo kwa makusudi au uzembe.

0 comments:

Post a Comment