Sunday, September 5, 2010

Muunge Mkono Dr Slaa

Jiunge na Harakati!

Mabadiliko yanawezekana. Tunaamini mabadiliko ya kweli yanaanzia ndani. Wanasosholojia wanasema “Mabadiliko huanzia kwangu”. Huu ndio ujumbe ambao tunamwambia kila Mtanzania - ‘badilika, tuibadili nchi yetu’.

Ewe mwanaCHADEMA, usihoji CHADEMA inafanya nini. Jiulize wewe umefanya nini kama mwanachama wa CHADEMA. Chama ni cha wanachama, jumla ya maneno na matendo ya wanachama ndio matokeo ya chama.

Ewe Mtanzania, usiulize mfumo wa vyama vingi uko wapi. Jiulize wewe umechangia nini kufanya vyama vya siasa hususani vyama mbadala kama CHADEMA kuendeleza yale unayoyaamini. Kama Mahatma Ghandi alivyosema, “Kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona”.

Ewe mdau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi, usiulize demokrasia ina hali gani Tanzania. Jiulize, wewe umetoa ushikirikano gani kuwaunga mkono Watanzania wenye kutetea, kuendeleza na kutekeleza demokrasia. Michango ya kimaendeleo unayoitoa haitaleta matokeo unayoyataka kama taifa halitakuwa na mifumo ya udhibiti thabiti ikiwemo upinzani makini na wenye nguvu.

Mabadiliko yanawezekana kama kila mmoja akitimiza wajibu. Na tuanze sasa.

Sasa nini tufanye?

 1. Kuwa mwanachama wa CHADEMA na kipigie kura CHADEMA. Lengo letu la muda mfupi ni kutoa fikra na sera mbadala na la muda mrefu ni kuchukua dola na kutekeleza misingi na mipango mbadala. Sera zetu makini mpaka sasa zimekuwa mchango mkubwa kwa Serikali. Kuna maamuzi ya kisera ambayo yamefanyika kutokana na hoja ambazo tumeziibua kama chama cha upinzani. Hata katika utawala wa awamu ya nne, kuna mambo kadhaa ambayo serikali imeyachukua kutoka kwetu ambayo tulikuwa tunayahubiri wakati wa kampeni. Hii ni sababu tosha ya raia makini kutaka CHADEMA iendelee kushamiri kama chanzo cha sera mbadala.  Usisubiri jiunge leo! jiunge sasa! 2. Tuchangie kwa hali na mali. Chama ni wanachama na uhai wa chama unategemea wanachama. Hivyo kila mwanachama anawajibu wa kutoa mchango wake wa hali na mali katika kutekeleza malengo ya chama. Tunalazimika kuwaomba hata wasio wanachama watuchangie kwa kuwa tunapambana na chama tawala kilichohodhi mali nyingi za Serikali bila ridhaa ya wananchi wake. Tunapambana na chama kinachochangisha kwa nguvu wafanyabiashara matajiri na kuwatishia mambo yao hayatanyooka kama hawatawaunga mkono. Tunapambana na chama chenye viongozi walioshutumiwa kupokea mabilioni ya fedha kutoka nje na wameshindwa kutoa ushahidi utakaokanusha madai hayo. Kazi ni kubwa lakini tunaimani kwamba upepo wa mabadiliko umeanza kuvuma na misaada yenu itatufikisha tunapokwenda kwa kuwa Mungu yupo upande wetu.  Unawezaje kutuchangia? soma zaidi... 3. Jiandikishe na Upige Kura. Kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni haki na wajibu wako. Ni uthibitisho wa uraia wako! Huhitaji kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa ili kuandikishwa. Sifa muhimu ni kuwa raia wa Tanzania na umri wa miaka 18.  Jitokeze upige kura kwenye chaguzi zoke zinazokuhusu, usikubali kuchaguliwa viongozi wabovu. Wakati wa kampeni za uchaguzi, wenye uchu na madaraka wakikupa takrima chukua, hiyo pesa ilistahili kuwa yako, lakini kura usiwape kwani hawastahili kupata. 4. Jielimishe uifahamu CHADEMA. Soma na uzifahamu Sera zetu makini. Vilevile soma Falsafa, Itikadi na Katiba yetu. Ni muhimu sana kujua CHADEMA inasimamia nini. 5. Kuwa chimbuko la CHADEMA. Si lazima kuwa na ofisi! Hata nyumbani kwako au kazini kwako kunatosha kuanzisha Msingi wa CHADEMA. Pata maelezo zaidi 6. Gombea uongozi. Mtaalamu wa siasa UDSM, Profesa Baregu alisema hivi karibuni, “Ari, Nguvu na Kasi mpya haiwezi kuwa na maana kama hakuna Fikra Mpya”. Wote tunatambua kuwa CCM wameishiwa fikra na ndio maana bado tupo gizani miaka 45 tangu tupate uhuru! Fikra mpya mnazo nyinyi Watanzania wenye uchungu na nchi yenu. Fikra hizo zitaweza kuleta maendeleo kama tu tutagombea uongozi katika ngazi mbalimbali za Serikali kuanzia vitongoji hadi Taifa. Pata maelezo zaidi. 7. Unganisha nguvu za ushindani. Wanaharakati wengine, mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi wote kwa ujumla tuondoe tofauti zetu, tushikamane kuing'oa CCM. Makosa ya chaguzi tatu zilizopita kamwe tusiyarudie. 8. Eneza ujumbe kwenye mtandao. Watumie wenzako taarifa kuhusu tovuti hii. Vilevile tuunge mkono kwa kututangaza kwenye tovuti yako. Hali kadhalika kama una habari zozote nyeti tafadhali This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it " style="margin-top: 0px; margin-right: 0px; margin-bottom: 30px; margin-left: 0px; padding-top: 0px; padding-right: 0px; padding-bottom: 0px; padding-left: 0px; border-top-width: 0px; border-right-width: 0px; border-bottom-width: 0px; border-left-width: 0px; border-style: initial; border-color: initial; outline-width: 0px; outline-style: initial; outline-color: initial; font-size: 11px; background-image: initial; background-attachment: initial; background-origin: initial; background-clip: initial; background-color: transparent; text-decoration: none; font-family: Verdana; color: rgb(34, 34, 34); font-weight: bold; background-position: initial initial; background-repeat: initial initial; ">tutumie.

Katika ngao na wimbo wa Taifa ipo ndoto yetu Watanzania: “Uhuru na Umoja”. Hii ni ndoto ya pamoja bila kujali itikadi. Ni ndoto tuliyorithi toka kwa waasisi wa Taifa letu. Wakati wa kudai uhuru, viongozi wetu waliweka bayana kwamba tunataka uhuru ili tuondokane na umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi ambavyo mkoloni alishindwa kuviondoa. Hatuwezi kusema tuna umoja katika taifa lenye pengo kubwa baina ya maskini na matajiri. Hatuwezi kusema tuna umoja katika ubaguzi. Nia ya kudai uhuru ilikuwa ni kuondoa maadui hawa na matokeo ya uhuru ni taifa lenye elimu, afya, utajiri na uongozi bora. Bado hatujafika. Ndio maana tunasema, ni wakati wa kuendeleza na kutekeleza Mabadiliko ya Kweli na Uhuru wa Kweli. Katika hali hii, nawakumbusha tena, “Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke.” Hakuna kulala, tuendeleze Mabadiliko ya Kweli. Mpaka kieleweke! Kikieleweka tutakuwa na Uhuru wa Kweli. Huwezi kulala kwa furaha katika ujinga, huwezi kulala kwa raha katika umaskini, utalala kwa karaha katika maradhi, huwezi kulala katika ufisadi. Hivyo basi unapojiunga na CHADEMA lazima uelewe kwamba huku kwetu Hakuna kulala Mpaka kieleweke!

Karibu.

0 comments:

Post a Comment