Thursday, September 9, 2010

KUSAMBAZWA WARAKA FEKI WA KATOLIKI KUMCHAFUA DR SLAA.

N\dugu zangu wana bidii kwa taharuku kubwa asubuhi nimekutana na matusi
mazito hata kuitwa kafiri na mzee mmoja kwenye kijiwe kikoja cha kiwi hapa
Moshi maeneo ya stendi.

Mzee huyo alikuwa anamsomea jamaa mmoja waraka anaosema umetoka kwenye kikao
kilichofanyika Dodoma ukiwasihi wakikristo wakatoliki kumchagua Dr Slaa ili
kurejesha hadhi ya kanisa, nikavutika kumsikiliza na baada ya hapo
nikamuuliza anieleze waraka huo ambao anasema unasambazwa kwa waislamu
kautoa wapi ndio akanivurumishia matusi kuwa mimi ni KAFIRI

Haraka nikagundua kuwa ni mzee lakini uzee wake umetawaliwa na ukame wa
fikra, nikaona nisinyamze kimya niwasirikishe wanajukwaa wenzangu na
kuwauliza kama mmeshakutana na waraka huo? kwa jinsi nilivyokuwa namsikiliza
waraka huo umebeba mambo mazito yenye kuhamasisha waumini wa kiislamu
kutomchagua Dr Slaa.

Nikiwa miongoni mwa waumini hao nathubutu kusema waraka huo si tu utaendela
kuturudisha nyuma kule tuliko toka kwenye enzi za chama cha CUF kuhusishwa
na uislamu lakini pia fikra potofu zilizo tawaliwa na ulewa mdogo. waislamu
wenye uelewa mdogo wanaweza kuamini kilichoko kwenye waraka huo.

Naomba kuwasilisha.

FUATILIA MJADALA HUU HAPA

KUSAMBAZWA WARAKA FEKI WA KATOLIKI KUMCHAFUA DR SLAA.

0 comments:

Post a Comment