Monday, September 6, 2010

FOS - MARAFIKI WA SLAA MIKOANI

Napenda kuwakaribisha kuwa sehemu ya FOS popote ulipo Tanzania hata nje ya Tanzania .Ukiwa Mwana FOS kazi yako itakuwa kutupatia habari na nini kinachotakiwa mkoani mwako na utaweza kukutana na FOS wenzako mkoani humo kwa ajili ya kutangaza habari njema kuhusu FOS na kile kilichokusudiwa tokea mwanzoMnaweza kujikusanya hata kikundi kimoja mkawa na Simu inayofikiwa muda wote angalau yenye uwezo wa kupiga picha na kurekodi kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu ya matukio na habari zingine zinazoendelea mkoani mwako au kijijini mwako na sehemu zingine ambazo upo .Kazi hii inaweza kuwa ngumu na gharama kidogo tunaweza kusaidiana katika kuhakikisha jamii inapata habari kuhusu DR SLAA na jamii hiyo inaweza kuleta changamoto mpya pia kwa DR SLAA .Kwa habari zaidi wasiliana na friendsofslaa@gmail.com tembelea blogu yetu katika www.marafikiwaslaa.blogspot.com na unaweza kujiunga na http://groups.google.com/group/friendsofslaa kwa kubadilishana habari na FOS wenzako Duniani

0 comments:

Post a Comment