Wana FOS wote,
Napenda kuwataarifu wote kuwa  tunapendekeza kufanya kikao cha wana FOS wote siku ya Iddi Pili (Kwa  maana hiyo itategema na muandamo wa mwezi, lakini ni Iddi Pili, hivyo  Iddi pili yaweza kuwa ni Friday au Saturday kutegemeana na na muandamo  wa mwezi) saa kumi kamili bila kuchelewa. Mkutano utafanyika Landmark.  Nelson Mandela Road. Kutakuwa na agenda muhimu sana.
Tunaendelea  kupokea michango. Napenda kuwashukuru wote mnaochangia. Kwa wale ambao  bado kwa heshima na taadhima naomba tukamilishe michango yetu. Ndugu  zangu vitu hivi viwili vinahitajika sana; tunahitaji finances ili tuweze  ku implement activities tulizokubaliana. Lakini pia tunahitaji manpwer  au volunteers kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinahitaji  nguvu kazi, moja ya kazi muhimu ni kulinda kura, kuwa mawakala na  kuhamasisha vijana, kina mama na wengine wote ili tumpigie kura Dr Slaa  aweze kurejesha Tunu za Taifa na hili ni kwa maslahi ya wanyonge wote  wakiwamo wana CCM. Hili halina maslahi kwa mafisadi tu.
Hivyo  naomba, mnipe mawazo yenu iwapo mnaafiki siku, mahali na saa ya kufanya  mkutano huu. Pia iwapo mngependa nifafanue au nieleze agenda ingawa  naona ni vizuri tukazijadili katika kikao. Kwani wakati mwingine jukwaa  hili linaweza lisiwe zuri sana kueleza hayo. Naomba mawazo yenu.
Naomba  pia mjiunge na group email ya frinds of Slaa kama inavyoonekana hapo  juu. Muhimu naomba mumtumie Yona taarifa za wapi mnatoka, na contacts  zenu ili tuweze kuratibu masuala mbalimbali. Tunataka kujua eneo  unalotoka, email na namba yako ya simu.
Njooni tuje tupange ili tuweze kufanikisha mikakati yetu.
Wasiliana kupitia friendsofslaa@gmail.com
 
1 comments:
Ingefaa msaidie kupatikana kwa vipande vya video ya mikutano ya Dr. Slaa kwani wengi hatuioni na vilevile ingetumika kampeni nyenzo ya kampeni. Hii ni pamoja za mikutano yake yote. Kingine ni kuwa tovuti yake haiboreshwi kila siku na haifunguki, je mnaweza kusaidia kurekebisha hilo?
Post a Comment