Tuesday, September 7, 2010

Propaganda za CCM kumpa chati Dr. Slaa

Hoja za maisha binafsi ambazo ni dhahiri zimepikwa na CCM, Makamba ndio alianzisha, akafuatwa na makada wengine, zitaijenga Chadema na mgombea wake wa urais. Kwa nini hizi hoja zitajenga badala ya kubomoa.
Zimekuja mapema sana na muda upo wa kutosha watu kujadili na kasha kuzipuuzia. Kwani zaidi ya kusema mtu kachukua mke wa mtu kuna lipi jipya watakalosema tena kuonyesha mabaya ya Dr. Slaa?
Sababu huyo aliyekuwa Mume ndio kajitokeza baada ya CCM kuanzisha hizi hoja, na kwa sababu kuna ushahidi kuwa Mkewe alishaondoka nyumbani hata kabla ya kukutana na Dr. Dlaa, jamii ya watu wenye uelewa watawapuuza CCM na kuwapunguzia umashuhuri wao kwa kuwa wataonekana wanawanyanyasa wananchi wao kwa kuangalia maisha binafsi. Wasomi na watu wenye uelewa zaidi ni dhahiri wataona CCM ni chama cha wahuni na kisichofaa kuongoza nchi kwa kuweka mbele UDAKU kuliko ukweli.
Jamii ilitegemea CCM ijibu shutuma mbalimbali zikiwemo za ufujaji madaraka, RUSHWA, udini, ukabila na upendeleo kwa watoto wa viongozi; lakini hawajaweza kujibu, hata kwa kukanusha au kukubali, na badala yake wameanzisha mjadala wa maisha ya Dr. Slaa. Wapiga kura wataamini shutuma dhidi ya CCM ni za kweli mana Dr. Slaa alishajieleza kuhusu maisha yake binafsi na bila shaka wananchi wameshajua ukweli.
Ni wazi CCM itakosa kura za watu wasiopenda mambo ya kuingilia maisha binafsi kwa kuwa hawatafurahia hilo. Ukitaka kujua kuwa watu wengi hawapendi maisha kuingilia maisha binafsi fuatilia kwa week Magazeti ya Udaku wanauza kopi ngapi? Halafu ulinganishe na magazeti makini kama Mwananchi. Hivyo hii issue itakuwa na faida kwa Dr. Slaa.
Kwa kuchapisha, tena kwenye ukurasa wa mbele, masuala ya Dr. Slaa, CCM inamuongezea umashuhuri kwa kuwa watu watapenda kujua huyu ni nani na ni kwanini anashambuliwa sana. Siku zote inatokea mnyonge kupendwa na watu wengi, na CCM hapa wamekosea step.
Kumpeleka mahakani mume wa zamani kudai fidia ya 1bn ni kuongeza elimu kwa wapiga kura kuwa CCM na wana propaganda wake wanazusha mambo. Hii itadhihirika pale mlalamikaji atakaposhindwa case na jamii ya kitanzania itajenga uaminifu zaidi kwa Dr. Slaa na kuidharau CCM.
CCM inapoteza nguvu na mali nyingi kutumia magazeti na njia nyingine kumchafua mtu kwa issue binafsi, wangeweka hizo nguvu kuwavutia watu kwa sera ingefaa zaidi kuliko kuwaelimisha watu na kuwafanya wamjue vizuri Dr. Slaa. Siku zote binadamu humfuata mtu wanayemjua kiundani, yote mapungufu na mazuri yake.
Kumebaki zaidi ya mwezi na nusu kufufikia uchaguzi, hii STORY ya CCM juu ya maisha ya Dr. Slaa itaisha tu ndani ya week chache zijazo, CCM watakauwa na lipi? Itakuwa ni zamu yao sasa kutakiwa kujibu shutuma za Ufisadi na ubadhirifu katika uongozi na mambo ya ahadi zisizotimilika.
Mwisho Namwonea huruma huyo Mume wake wa Zamani mana kaingia mkenge. CCM watamtumia tu wakati wa kampeni na zitakapoisha atajijua mwenyewe. Kama atakuwa na kesi mahakamani itabidi ajilipie gharama, na aibu nyingine zitakuwa juu yake. Watu wanajiuliza Tangu Dr. Slaa aweke hadharani mahusiano yake na huyu bibi alikuwa wapi? Tulitegemea siku ile ile angelalamika. Sasa kakubali kutumika kisiasa atayaona matokeo yake baada ya 31 Oct. Na kuna siku ukweli utawekwa hadharani hapo ndio itakuwa mwisho.

0 comments:

Post a Comment