Thursday, November 25, 2010

Mdahalo - Freeman Mbowe na Hamad Rashid Mohamed

Napenda kuchukua nafasi hii, kwa niaba ya Vox Media kuwatangazia kwamba Jumamosi hii, yaanii Novemba 27, 2010, kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku, tutakuwa na mdahalo kati ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohamed, Mbunge wa Wawi (CUF), kuhusu masuala yahusianayo na kambi hiyo bungeni.

Mdahalo huo utarushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV (saa moja mpaka tatu usiku). Kwa kuwa kadi zilizopo ni chache, wengi wenu mnashauriwa kuwa kando ya televisheni zenu kwa ajili ya kushuhudia.
Karibuni na ahsanteni.

Serikali mpya isimamiwe

MOJA ya habari kubwa leo ni Baraza jipya la Mawaziri lililotangazwa jana na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Baraza la Mawaziri lenye jumla ya mawaziri 50 huku likiwa limefanyiwa mabadiliko ya kimuundo katika wizara mbalimbali zilizokuwepo awali, lilifafanuliwa jana na Rais Kikwete kuwa linalenga kurahisisha ufanisi wa utendaji kazi wa serikali yake.

Izingatiwe kuwa katika idadi hiyo mawaziri ni 29 na manaibu waziri ni 21, na baraza hilo limezidi kuwa kubwa zaidi kuliko lile lililopita ambalo lilikuwa na mawaziri 47.

Ikumbukwe kuwa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, alikuwa akilalamikia sana ukubwa wa baraza la mawaziri lililopita huku akianisha takwimu mbalimbali zilizoonyesha kuwa lilikuwa likiongeza gharama kubwa zisizo za lazima katika uendeshaji wa serikali.

Aidha, hoja hiyo ya Dk. Slaa ilikuwa ikiungwa mkono pia na wasomi, wanaharakati na watu wa kada mbalimbali huku wakisisitiza kuwa ni muhimu kuwa na serikali ndogo yenye tija na inayobana matumizi.

Kinyume cha kilio hicho cha wadau wa siasa na masuala ya kiutawala, tunasikitika kuona Rais Kikwete ameshindwa kuwa msikivu na kurudia kuunda baraza kubwa tena kuzidi hata lile la awali.

Tunajua kuwa hoja ya Rais Kikwete kuongeza wizara na mawaziri ni kurahisisha utendaji na ufanisi wa serikali yake kama alivyoeleza jana wakati anafafanua sababu za kuigawa wizara ya miundombinu kuwa wizara mbili za Ujenzi na Miundombinu.

Hata hivyo bado tunachelea kushawishiwa na hoja hizo za rais, kwani ukweli ni kwamba mawaziri si watendaji bali ni wanasiasa wanaofanya zaidi kazi ya kuratibu na kusimamia sera ambayo inaweza kufanywa na mawaziri wachache ili mradi kuwe na watendaji bora.

Kwa mantiki hiyo, tulitegemea badala ya Rais Kikwete kuongeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, angefanya mabadiliko ya mfumo wa utendaji na watendaji wenyewe ili kuwarahisishia kazi mawaziri wachache na kuokoa fedha za walipa kodi kwa manufaa ya wananchi.

Kwa dosari hiyo kubwa, ni matumaini yetu kuwa wadau mbalimbali na taifa zima, kila mmoja kwa wakati wake na kwa nafasi yake ataendelea kutimiza wajibu wa kumsihi mkuu huyo wa nchi kupunguza ukubwa wa baraza lake. Bado tunaamini ni msikivu na ataitikia kilio hiki mbele ya safari.

Pamoja na dosari hiyo, bado tunawasihi Watanzania wote kuipa ushirikiano mzuri serikali hiyo mpya iliyotangazwa jana kwani ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi na tofauti zetu mbalimbali.

Hivyo basi, tunatoa rai kwa chombo kikuu cha kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali (Bunge) kuhakikisha kuwa linashauri, kuifuatilia na kuisimamia serikali hiyo mpya ili iwajibike vizuri na kwa uadilifu wa hali ya juu kwa masilahi ya vizazi vya leo na vya kesho vya taifa hili.

Tunahitimisha kwa kuwataka wananchi wa kawaida na vikundi shinikizi, zikiwamo asasi zisizo za kiserikali (NG’Os na CSO’s) pamoja na asasi za kidini kuunga mkono rai hii ya kuipa ushirikiano serikali yetu pamoja na kuisimamia.

source : tanzania daima

Shitambala ajibu agizo la Dk. Slaa

WAKATI uongozi wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukikataa ombi la kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, kwa kutokidhi vigezo vya katiba ya chama, mwenyekiti huyo amesisitiza hatakuwa tayari kurudi katika nafasi hiyo kwa sasa hadi hapo chama hicho kitakapomaliza kabisa uchunguzi wake.

Shitambala ambaye ni wakili wa kujitegemea alisema ataendelea kukaa nje ya cheo hicho ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma za rushwa zinazoelekezwa kwake lakini pia kulinda hadhi ya kazi yake ya kutetea haki za raia kupitia kada ya sheria.

Msimamo huo aliutoa jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kujibu maagizo ya chama chake, ikiwa ni siku moja tu baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Dk. Willibrod Slaa, kulikataa ombi lake na kumsihi aendelee na uenyekiti.

Kwa mujibu wa barua ya Shitambala aliyokiandikia chama hicho na Tanzania Daima kupata nakala yake, sababu kuu nne ndizo zilizomfikisha kwenye uamuzi wa kujiuzulu wadhifa huo.

Miongoni mwa sababu hizo ni yeye kutupiwa lawama za kupokea rushwa kwenye uchaguzi wa ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini pamoja na mkoa kukosa mgawo wa wabunge wa viti maalumu.

Alisema mbali na ukweli ulivyo juu ya mfumo uliotumika kupata nafasi za wabunge wa viti maalumu, wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho mkoa wamekuwa wakitaka majibu, hali ambayo imekuwa ikimuweka katika wakati mgumu kwani hakuhusika katika mchakato huo.

Alisema katika hali ya kushangaza uongozi huo wa juu wa chama badala ya kufikiria kwa kina hoja hizo nzito na kuzitafutia majibu yanayoweza kuwatuliza wanachama wenye hasira wao wameendelea kutoa majibu mepesi.

“Hoja iliyopo mbele ni nzito, haiingii akilini Mkoa wa Mbeya kukosa nafasi ya viti maalumu wakati tumefanya kazi kubwa ya kukiinua chama tena kwa muda mfupi, walipaswa kutoa tiba kwanza kwa hili ndipo waamuru mimi nirudi kwenye nafasi yangu,” alifafanua Shitambala.

Aliongeza kuwa baada ya kupata nafasi ya kuwa mwenyekiti maisha yake yalitengenezwa katika sura mbili hivyo kitendo chake cha kuamua kujiuzulu kutokana na tuhuma za rushwa zinazotokana na mambo ya siasa kina lengo la kuokoa hadhi ya maisha ya upande wa pili wa taaluma yake ya sheria.

“Si rahisi mimi kuona maisha ya siasa yanaharibu maisha yangu ya kawaida na wala maisha yangu ya kawaida yakiharibu maisha ya siasa, ni vizuri nikaeleweka hivyo. Mimi bado ni mwanachama mwaminifu na punde yote haya yakishughulikiwa na mimi kuonekana sikuhusika basi nitarudi kuwatumikia wananchi,” alisisitiza Shitambala.

source : tanzania daima

Dk Slaa anena: Sitta akikubali, nitamshangaa

Fidelis Butahe
VIONGOZI wa vyama vya upinzani wameponda uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa Baraza la Mawaziri, huku katibu mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa akisema atashangaa kama Samuel Sitta ataridhia uteuzi wake wa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao amesema utamshushia hadhi.

Sitta alikuwa amechukua fomu za kutaka achaguliwe tena kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano lakini CCM ikamuengua kwa kile ilichoeleza kuwa ni kutaka wanawake waongoze moja ya mihimili ya nchi.
Kuenguliwa kwake kulifanya wengi wabashiri kuwa Rais Kikwete angempa wizara nyeti kama ya Katiba na Sheria ili aongoze mabadiliko ya katiba baada ya Zanzibar, lakini jana alitangazwa kushika wizara hiyo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dk Slaa, ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema, alisema kuwa uteuzi wa Sitta umelenga kuendeleza ufisadi na kwamba iwapo spika huyo wa zamani ataikubali kushika nafasi hiyo, atakuwa amejishushia hadhi.
Dk Slaa, ambaye aligomea matokeo ya kura za uchaguzi wa rais na baadaye chama chake kutangaza kutotambua matokeo hayo, alisema: “Nilitegemea kusikia Baraza la Mawaziri 20 hadi 25. Sasa hawa mawaziri wote wanakwenda wapi, watapewa nyumba na magari ya Sh200 milioni, hivyo fedha nyingi zitatumika kwa matumizi yasiyo na ulazima.”
“Hili baraza limeundwa kujenga utawala wa kifisadi, kazi ya Baraza la Mawaziri si kumlinda rais ni kuwahudumia Watanzania; hizi si sura sahihi.”

Dk Slaa alisema kwa kiongozi makini kama Sitta kupelekwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mwendelezo wa ufisadi na kusisitiza kuwa atamshangaa kama atakubaliana na uteuzi huo.
“Naelewa kilichomkumba Sitta... kila siku nasema hii kauli na sitachoka kuisema kwa kuwa naipenda nchi yangu. Inakuwaje unatoa nafasi za uwaziri kwa ajili ya kulipa fadhira? Hii si sahihi hata kidogo,” alisema Dk Slaa.
“Uteuzi wa Sitta kwenye wizara hiyo ndio utatudhihirishia kama kweli yeye ni mpambanaji wa ufisadi au la.”
Dk Slaa pia aliponda uteuzi wa William Ngeleja kuwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Makongoro Mahanga kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi na Ajira kuwa hauna mantiki.

Hata hivyo hakufafanua zaidi sababu za kauli yake hiyo kuponda mawaziri hao.
Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema kuwa baraza hilo halina jipya na akamshangaa Rais Kikwete kutumia siku nyingi kabla ya kutangaza baraza wakati hakuna jipya alilolifanya katika uteuzi wake.
“Watanzania wategemee maisha yaleyale tu, hakuna mabadiliko yoyote... labda kikubwa ni uteuzi wa (Waziri mpya wa Ujenzi, John) Magufuli na waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna) Tibaijuka. Lakini, Tibaijuka naye hatakuwa na kazi rahisi kwa kuwa ndio mara yake ya kwanza anakuwa waziri na alikuwa ameshazoea kazi za kimataifa ambazo ni tofauti na za wizara,” alisema Mziray.

Alisema kwamba kuona baraza dogo lenye mawaziri wasiozidi 30 na kusisitiza kuwa uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete unaendeleza mfumo wa CCM wa kupeana ulaji.
“Ili Watanzania waondokane na karaha hii, suluhisho ni kuwachagua wapinzani. Siku wapinzani wakiingia madarakani haya yote yatakwisha,” alisema Mziray.
Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alisema kuwa uteuzi huo umewapa watu ambao ni wagumu wa kufikiri matatizo na shida za Watanzania akipinga uteuzi wa Wazanzibar katika baraza hilo.
“Haiwezekani; Zanzibar wamevunja Muungano inakuwaje nao wanaingizwa katika baraza la mawaziri. Huku ni kujipendekeza kwa namna ya kipekee,” alisema Mtikila.

Mchungaji Mtikila ambaye alienguliwa katika kinyang’anyiro cha urais kwa madai ya kutokuwa na wadhamini katika mikoa 10 ya Tanzania Bara, alidai kuwa alichokifanya Rais Kikwete ni kuwafurahisha watu fulani ambao hakuwataja watu hao.

“Uteuzi huu si kwa ajili ya maslahi ya Watanzania; baraza hili la mawaziri ni maafa makubwa. Nchi ya Ujerumani ina mawaziri 14, Marekani hawazidi 30, lakini sisi ndio tunaendeleza kufurahishana. Nakwambia baada ya miaka mitano nchi hii itakuwa imekwisha kabisa,” alisema Mchungaji Mtikila.
Naye mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema Kikwete anatakiwa kuwa mkali kwa baraza hilo ili mawaziri wake wasifanye mzaha.

“Yaani hawa mawaziri naona wangekuwa na barua za kujiuzuru mkononi ili watakapovurunda iwe ni kukabidhi barua hizo na kuachia ngazi. Ni kweli baraza ni kubwa, lakini kama kutakuwa na uwajibikaji, sidhani kama kutakuwa na tatizo, ila kama wakilala, hapo ndio mambo yatakapoanza kuwaharibikia,” alisema Mrema.
Mrema alimpongeza Rais Kikwete kwa kuwateua Magufuli na Anna Tibaijuka akisema kuwa ni watendaji wazuri.

SOURCE : MWANANCHI

Monday, November 22, 2010

Dk Bana: Chadema wana hoja ya msingi

Sadick Mtulya
MKUU wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, amesema Chadema kina hoja ya msingi kushinikiza uundaji katiba mpya na kwamba, tatizo lipo njia wanayotumia.
Kauli ya Dk Bana inakuja ikiwa ni siku chache, baada ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia, kuashiria kuzindua rasmi.

Chadema ilifaya hivyo ikiwa ni hatua yao kupinga matokeo ya urais yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kushikiza uundaji wa katiba mpya, Nec na uundaji Tume ya uchunguzi wa yaliyoajiri uchaguzi mkuu uliopita.
Kufuatia kitendo hicho, wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi waliibuka na maoni tofauti.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Siasa’ kupitia Kituo cha Televisheni cha Star Tv jana, Dk Bana alisema madai ya chama hicho yana msingi.
“Madai ya Chadema ni ya msingi, lakini tatizo ni njia waliyotumia kutozingatia utamaduni wa Watanzania katika kudai haki,’’ alisema.

Dk Bana alisema Chadema imetumia njia hasi ambayo kimantiki itajenga tabia kwa wananchi wa kada tofauti kususia vikao au mikutano itakayokuwa inaitishwa na viongozi.
“Kama njia hii itakubalika katika jamii, itafikia hatua hata wanafunzi watatoka nje ya darasa wakati mwalimu akiwa anafundisha, kwa hoja kwamba hawamtaki jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Watanzania na hatari kwa mustakabali wa baadaye wa taifa,’’ alisema.

Kuhusu Katiba, alifafanua kwamba kulingana na mabadiliko ya wakati, Katiba ya sasa ambayo ilitungwa mwaka 1977, haikidhi haja na tija ya Watanzania inastahili kutungwa upya.

“Kulingana na wakati, inahitajika katiba mpya itakayokidhi haja na tija kwa Watanzania wote, Katiba ambayo itatoa fursa zaidi kwa wananchi kuweza kuwajibisha viongozi,” alisema na kuongeza:
“Itatoa fursa ya kujadiliwa zaidi kwa masuala ya muundo wa muungano, uteuzi wa mawaziri, uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi za serikali, uwepo wa tume huru ya uchaguzi, rais kupunguziwa madaraka na mambo mengine.’’

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amenukuliwa akisema uamuzi wao ulizingiatia demokrasia na kwamba, ulipeleka ujumbe mzito kwa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa ili kuibua mjadala wa kitaifa juu ya umuhimu wa masuala hayo matatu.

chanzo : gazeti mwananchi

Chadema: Tuko tayari kukaa mezani na serikali

Sunday, 21 November 2010


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Mwandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kipo tayari kukutana na serikali, chama au taasisi nyingine yoyote itakayotaka kujadiliana kuhusu hatua yao ya kutoyatambua matokeo ya uchaguzi wa urais na madai yao ya katiba mpya.

Katika tamko ambalo halijawahi kutokea kwenye siasa za Tanzania, Chadema ilitangaza kuwa haitambui matokeo ya uchaguzi wa rais kwa madai kuwa taratibu nyingi zilivurugwa kwa lengo la kumbeba mgombea wa chama tawala na ilidhihirisha msimamo wao wakati wabunge wa chama hicho walipotoka kwenye ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kuanza kuhutubia.

Lakini jana mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliiambia Mwananchi kuwa wako tayari kukaa meza moja na serikali au taasisi ambayo wataiona kuwa inaweka mbele maslahi ya taifa ili kujadiliana nayo kuhusu msimamo huo wa kwanza kuweka dhidi ya rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Msimamo wa Chadema umetolewa wakati mwandishi msaidizi wa rais, Premi Kibanga akikitaka chama hicho au Mbowe kufuata taratibu zilizopo iwapo wana lengo la kweli la kutaka majadiliano.

Kibanga alisema kuwa Mbowe, kama mwanasiasa na kiongozi wa kitaifa, anazifahamu taratibu na njia za kutumia iwapo anataka kukutana na serikali. Lakini mbunge huyo wa Hai alisisitiza kuwa hawangependa majadiliano yao ya serikali yachukue sura ya kisiasa kwa kuwa kufanya hivyo hakutafanikisha kufikiwa kwa lengo wanalolikusudia. “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunalifikisha taifa hili mahali ambapo amani na utulivu utaendelea kuwepo.


Kati ya madai yetu yote hakuna jambo ambalo ni kwa ajili ya Chadema... tunayoyadai yatainufaisha CUF, CCM, vyama vingine vya siasa na wananchi wote,” alisema. Hata hivyo, Mbowe alionya kuwa mazungumzo hayo yasitawaliwe na aina ya maoni yanayotolewa na viongozi kadhaa wa CCM, yakiwemo ya katibu mkuu wa chama hicho tawala, Yusuf Makamba na katibu wa itikadi na uenezi, John Chiligati. “Hawa wameonekana kuzungumzia suala hili kisiasa zaidi wakati lengo letu sisi si kupiga siasa. Angalia hata mambo wanayosema eti tutaleta hoja ya kuwafukuza Chadema bungeni... hoja kama hiyo haina msingi kwa sababu hawana ubavu kisheria wa kufanya hivyo,” alisisitiza.

Alisema mazungumzo wanayoyalenga ni yale yatakayohakikisha kuwa madai yao yanafikiriwa kwa kina huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele. Alisema wanafurahi kuona kuwa kitendo chao cha kutoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Kikwete kimesaidia kuibua mjadala mzito nchini ambao iwapo utapewa nafasi ya kujadiliwa bila kuweka ushabiki wa kisiasa, nchi inaweza kupata mabadiliko makubwa siku za usoni.

Alitoa mfano wa wa watu kama waziri mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani ambao walikaririwa wakisema kuwa suala la kuwa na katiba mpya ni muhimu. “Maoni kama haya, ambayo yanatoka kwa watu wazito kama hawa, yanaonyesha kuwa kitendo chetu kimeamsha mjadala wa maana kwa taifa hili,” alisema.

Alipoulizwa iwapo kitendo chao cha kutaka kukutana na serikali hakiathiri uamuzi wao wa kutotambua matokeo ya urais, alisema kuwa walishatamka tangu awali kuwa hawakatai kuwa kuna rais ingawa wanachopinga ni jinsi alivyopatikana. “Tunajua kuwa Kikwete ndiye ametangazwa kuwa rais, lakini tunachopingana nacho ni jinsi alivyoelezwa kuwa ameshinda katika uchaguzi... tunachokidai si kuwa uchaguzi urudiwe au kwamba Dk (Willibrod) Slaa atangazwe rais, la hasha. Tunalenga kuwa na mfumo bora siku za usoni ambao hautaacha shaka kwenye matokeo ya urais,” alisisitiza.


Alisema ni hatari sana kuwa na sheria ambayo hairuhusu watu kuhoji matokeo ya kura za urais katika mazingira ambamo watu wengi wanaingia kwenye kinyang’anyiro hicho. Alisema kuwa sheria ya kukataza kuhoji matokeo ya urais ilitungwa wakati wa mfumo wa chama kimoja wakati kukiwa hakuna mgombea wa kutoka vyama vya upinzani. “Wakati ule Mwalimu Nyerere ndiye kila mara alikuwa mgombea pekee, alikuwa hashindani na mtu yeyote kwa hiyo hakukuwa na mtu wa kuhoji. Wenzetu hawa wameichukua sheria hiyo na kuileta kwenye mfumo wa vyama vingi. Hauwezi kuitumia sheria hiyo hiyo wakati huu wa ushindani,” alisema.


Alisema iwapo matokeo ya uchaguzi wa ubunge na udiwani yanaweza kupingwa mahakamani, hakuna misingi ya kidemokrasia ya kukataza kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais. Alitaka serikali kuiga mfano wa Senegal ambayo ina mahakama ya katiba ambayo moja ya majukumu yake ni kusikiliza malalamiko yote kuhusiana na uchaguzi wa rais na kiongozi mpya wa nchi haapishwi hadi mahakama hiyo imethibitisha matokeo hayo. Alisema pamoja na madai ya katiba mpya, madai yao mengine ambayo wangependa yajadiliwe iwapo watakutana na serikali ni kuundwa kwa tume huru itakayochunguza matukio yote kuhusu uchaguzi wa rais.

Alisema kwa mazingira yaliyopo, tume hiyo inaweza kuundwa na Rais Kikwete lakini kwa kuwachagua watu makini ambao wanaheshimika nchini. “Watu kama hao wapo wengi tu,” alisema.

Alionya kuwa si vema tume hiyo ikachukua mrengo wa kisiasa kwani kufanya hivyo kunaweza kupotosha majadiliano. “Kuna nafasi ya Chadema au CCM kuunda tume hiyo, lakini itaonekana kuwa ni ya kichama zaidi. Pia kuna nafasi ya Bunge kuunda tume, lakini Bunge nalo lina wanasiasa ambao wana maslahi kutoka katika vyama vyao. Hii ndiyo maana tunashauri rais anaweza kuunda tume hiyo lakini kwa kuhakikisha kuwa anawateua watu ambao wanaheshimika katika jamii ambao kila mmoja anajua kuwa wanajali zaidi maslahi ya taifa,” alisema.

CHADEMA Special Seats MP from Kigoma Hon. Mhonga S. Ruhwanya with Malaysian ex PM Tun. Dr. Mahathir Mohamad

CHADEMA Special Seats MP from Kigoma Hon. Mhonga S. Ruhwanya with Malaysian ex PM Tun. Dr. Mahathir Mohamad after a discussion in his Office at Petronas Twin Towers, Kuala Lumpur.

MHE ZITTO KABWE ALIPOKUWA MALAYSIA



Kigoma North MP Hon. Zitto Kabwe with Malaysian ex PM Tun. Dr. Mahathir Mohamad after a discussion in his Office at Petronas Twin Towers, Kuala Lumpur. Zitto is in Malaysia on a one week long private visit at the invitation of Malaysian ex PM Tun. Dr. Mahathir Mohamad who was a very close friend of Mwalimu Nyerere, to learn more on the Malaysian development experience and the palm-oil industry.

After our meeting this is what Tun. Dr. Mahathir Mohamad said to ZITTO:

“Put your country at heart, don't destroy your country for political expediency or for fulfilling your ambition. Serve your country”

Saturday, November 20, 2010

WABUNGE WA CHADEMA WALIPOSUSIA HOTUBA YA JK

Wabunge wa CHADEMA wakitoka Bungeni

Chadema 'yaitikisa' nchi :NI KUTOKANA NA WABUNGE WAKE KUSUSIA HOTUBA YA JK

source : mwananchi

Na Waandishi Wetu

HATUA ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia, imetikisa nchi kutokana na wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi kuibuka na maoni tofauti.

Chadema wametangaza kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa kulikuwa na kasoro nyingi kwenye zoezi zima la uchaguzi na kwamba Tume ya Uchaguzi (Nec) ilikuwa imelenga kumbeba mgombea urais kutoka chama tawala.

Chadema, ambayo safari hii imeingiza watu wengi bungeni, imeamua kutumia njia hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais kushinikiza kuundwa kwa katiba mpya kutokana na katiba ya sasa kutotoa haki ya kupinga matokeo ya urais na inataka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Katika mahojiano ambayo Mwananchi iliyafanya jana katika mikoa tofauti nchini lilibaini kuwa wapo wanaoona kitendo hicho kilikuwa halali wakieleza uamuzi huo unaweka bayana msimamo wao wa kutokubaliana na mfumo uliomweka madarakani Rais Jakaya Kikwete , huku wengine wakikosoa kwa kusema kwamba hawakustahili kufanya hivyo mbele ya rais, wakitafsiri kuwa huenda hizo ni chokochoko za kuvuruga amani na utulivu nchini.

Wasomi, wanazuoni wanaounga mkono
Mhadhri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abdallah Safari alisema kitendo hicho nio cha ni aibu kwa serikali ya Kikwete na Nec na kutaka kitafsiriwe kuwa ni kiashirio cha udhaifu katika uchaguzi na mahitaji ya tume hiyo.

“Ni silaha ya haki kwa kila mwanasiasa, ndio maana hata katika historia wabunge waliokuwa kwenye mabunge aliyokuwa akihutubia Fidel Kastro walikuwa wakitoka nje. La kujitakia halina majuto,” alisema Profesa Safari.

Mhadhiri mwingine katika Chuo hicho, Dk Azaveli Lwaitama alisema kitendo cha Chadema cha kawaida kwa kuwa siasa huambatana na suala la kisheria na hisia.

“Wao wamesema kuwa hawamtambua, lakini tayari rais wetu ameshaapishwa, hivyo kinachowafanya waseme hivyo ni hisia tu. Wanataka kuwaonyesha Watanzania kuwa hawakubaliani na matokeo ya urais, lakini kisheria hawawezi kufanya lolote kwa kuwa sheria inawabana,” alisema Dk Lwaitama.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini mkoani Kilimanjaro ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema hakuna kosa lolote kwa wabunge kutumia njia hiyo kuonyesha dhamira yao ya kutokubaliana na matokeo ya Urais kwa kuwa hawana njia nyingine.

“Ibara ya 41 Ibara ndogo ya 7 ya katiba yetu inakataza matokeo ya urais kuchunguzwa baada ya kutangazwa na Nec… sasa kama umemfunga mshindani wako mikono, afanyeje kukuonyesha hakubaliani nawe,” alihoji.

"Katika hali ya kawaida ni jambo lisilowezekana kukubali goli ambalo unaamini limefungwa kwa mkono na kwamba hakuna mfumo unaomlazimisha mtu kumsikiliza Rais.”

Alisema haiwezekani Tanzania kujisifu kwa maendeleo ya kidemokrasia wakati katiba inazuia watu kuhoji uhalali wa matokeo ya urais, lakini katiba hiyo inaruhusu watu kuhoji uhalali wa matokeo ya wabunge na madiwani.

“Senegal kuna mahakama ya katiba ambayo inataka baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa, ni lazima yathibitishwe na Mahakama ya Kikatiba… kunakuwepo kipindi maalumu cha kushughulikia malalamiko kabla ya Rais kuapishwa,” alisema.

Harod Tairo, mhadhiri wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema kitendo cha Chadema hakikumfurahisha kwa sababu kilijenga taswira ya mgawanyiko na machafuko bungeni.

“Mimi nashauri CCM wakae chini na Chadema wazungumze tatizo lilikuwa wapi ili kuziba mianya itakayoweza kuleta machafuko kama yaliyotokea Zanzibar,” alisema Tairo na kuongeza kuwa kama serikali inataka kukuza demokrasia, ni lazima ikubali msimamo na kitendo kilichofanywa na Chadema.

Naye mhitimu wa shahada ya sheria wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa, Clement Kihoko alisema kitendo hicho ni kabisa japokuwa wanaweza kueleweka tofauti.

“Ni utaalamu wa kifalsafa na ni mambo ya kuangalia kwa umakini zaidi kwa sababu kama walivyosema awali kwamba hawamtambui Kikwete kama rais ,wangebaki kumsikiliza bungeni wangeonyesha kumuunga mkono na kumkubali,” alisema Kihoko.

Kihoko alibainisha kuwa katika tafsiri ya kifalsafa na hata falsafa ya sheria, kitendo walichokifanya chadema ni sahihi kabisa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM), Ali Nassor alisema kitendo cha Chadema ni kuwaonyesha wananchi kwamba wako makini na wanatambua jukumu walilokabidhiwa na wananchi bungeni.
“Kwa kitendo hiki Chadema wanajiweka hadharani ili kupata wanachama wengi,” alisema Nassor.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Dk Fairles Ilomo alielezea Chadema kuwa ni wapigania makabadiliko wachache waliojitoa kuwambwa msalabani kwa manufaa ya wananchi wengi.

Hata hivyo Dk Ilomo hakuunga mkono njia waliyotumia kupigania mabadiliko kwa kusema kuwa hawakupaswa kususia hotuba ya rais bali walipaswa kuwa wavumilivu na kutumia Bunge kufanya mabadiliko.

“Ni kitendo kilichoonyesha ujasiri kwa sababu kukiwa na viongozi ambao ni waoga watupu itachukua muda mrefu kufanya mabadiliko,” alisema Dk ILomo.

“Hayati Baba wa taifa Julias Nyerere alipoanza kupigania uhuru wakoloni walisema ni mvurugaji wa amani na kumweka rumande kwa saa kadhaa, lakini sasa tunafaidi matunda ya uhuru aliopigania. Vivyo hivyo wananchi watakuja kufaidi matunda ya mgomo Chadema."

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walisema kitendo cha wabunge wa Chadema kinastahili kupongezwa kwa kuwa wameonyesha kwa vitendo kuwa uchaguzi ulikuwa na dosari.

Wanafunzi hao ambao wapo Jijini Tanga kwa ajili ya mazoezi walisema wabunge hao hawakutaka kuwa wanafiki mbele ya Rais Kikwete na badala yake wakaonyesha kilichokuwa mioyoni mwao.

“Walichofanya ni kupaza sauti ili dunia ielewe kwamba kulikuwa na dosari kubwa katika zoezi zima la kutangaza matokeo na hilo linaegemea kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema Saida Hamis mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

Mawakili na Wanasheria
Mwanasheria wa Ngorongoro mkoani Arusha, Imanuel Saringe alisema: "Kisheria jambo hili halina tatizo na binafsi ninaaamini ujumbe wao umefika kwa walengwa bila vurugu au damu kumwagika."

Hata hivyo, alisema hutuba ya Rais Kikwete imekuwa ya ujumla sana na hivyo ni vigumu kuitathimini katika utekelezaji wa aliyosema.

Naye wakili mashuhuri mjini Moshi (jina limehifadhiwa) alisema kwa mtu mwenye mawazo finyu anaweza kusema kitendo cha Wabunge hao ni usanii fulani, lakini mtu upeo mpana atagundua Tanzania ina mgogoro wa kikatiba.

“Tuna tatizo la ubovu wa sheria nzima ya uchaguzi na kwa bahati nzuri sana wabunge hawa wameishia tu kutoka nje lakini tukiendelea na mfumo huu wa katiba unaokataza kuhoji matokeo ya rais, iko siku tutamwaga damu.”

Alisema: ”Tukiendelea na katiba hii tutajikuta tunakuwa na kiongozi aliyetangazwa kuwa ni rais, lakini si kiongozi aliyeshinda urais... kisheria anakuwa Ikulu, lakini kiuhalali hastahili na hapa ndipo mgogoro unapoanzia.”

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
Mkurugenzi mtendaji wa wanaharakati wa Agenda 2000, Moses Malaba alisema kitendo kilichofanywa na Chadema, kimefikisha ujumbe uliokusudiwa.

“Kisiasa walichofanya Chadema ni sawa; wamefanikiwa kufikisha ujumbe wa kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi kama walivyokusudia,” alisema Malaba lakini akaonyesha wasiwasi kama wananchi wataelewa lengo la chama hicho.

“Lakini wameenda mbali sana... wanachotaka wananchi waliowachangua ni kupata uwakilishi bungeni. Kwa sasa wanataka kujivunia kuwa na wabunge wengi.”

Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Fred Njama alisema haoni kosa lolote kwa wabunge hao kufanya kitendo hicho.

“Kwa maoni yangu walichokifanya ni sahihi kwa sababu usipokubaliana na mtu huwezi kumsikiliza... ni vizuri hisia zako usizifanye ni siri ni vizuri ukazionyesha badala ya unafiki; mimi sioni tatizo hapa,” alisema.

Vyama vya siasa
Aliyekuwa mgombea urais wa TLP, Mutamwega Mugahwa alisema kitendo cha Chadema kinampasa Rais Kikwete kukaa chini na kutafakari tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.

“Ningekuwa mimi ndio nimesusiwa Bunge, kiukweli nisingeweza kuchukulia kirahisi; lazima ningekaa na wahusika na kujua tatizo lililopo na kutafuta njia ya kulitatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Mugahwa.
Alisema kwa mujibu wa katiba mtu ana uhuru wa kusikiliza na kutosikiliza ili mradi tu katika maamuzi yake asiingilie uhuru wa mtu mwingine.

Muasisi wa Chadema, Edwin Mtei alisema kitendo hicho binafsi kimempa faraja na kwamba huo ni mwendelezo wa kupinga katiba na kutaka ibadilishwe.

Mtei ambaye pia aliwahi kuwa gavana wa Benki Kuu nchini pia alimuunga mkono mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, Jaji Amir Manento kuwa sasa ni muda wa kulilia katiba mpya.

Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Iringa
Baadhi ya wananchi wamewapongeza wabunge wa Chadema kwa hatua yao wakieleza kuwa msimamo huo unaweza kumfanya rais ajue kwamba wapo Watanzania wengi ambao hawana imani na utendaji kazi wa Nec.

Walisema Chadema wangeweza kuitisha maandamano na kufanya fujo kama ilivyowahi kutokea nchini Kenya, lakini kwa busara wametumia njia ya kususia hotuba kuonyesha kuwa hawamtambui rais kama alivyotamka katibu mkuu wa Chadema, Dr Willibrod Slaa.

Enock Mwasondole ambaye ni mkazi wa Mtwivila alisema umefika wakati ambao Nec inapaswa kuwa huru ili malalamiko yatokanayo na uchaguzi yapungue.

“Ni bora kususia kuliko wangeitisha mgomo na maandamano makubwa kama yaliyotokea Kenya. Rais asipuuzie hali ile badala yake anapaswa kuhakikisha Tume ya Uchaguzi inakuwa huru na kutenda haki,” alisema Mwasondole.

Mkazi mwingine wa Gangiolonga, Anania Mlelwa alisema huu ni wakati wa Tanzania kubadilisha katiba ambayo Iliandaliwa wakati wa chama kimoja na hivyo kusababisha tume hiyo kuwa mikononi mwa rais ambaye ni mwanachama wa chama kimoja.

“Katiba ndiyo tatizo kubwa; kama katiba ingelingana na wakati wa vyama vingi, tume isingekuwa ikilalamikiwa kwa kuwa isingekuwa chini ya rais,” alisema.

Naye rais wa Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari, Keneth Simbaya alisema suala hilo ni la kiitikadi zaidi la kwamba wabunge hao wanapaswa kusikilizwa kwa kuwa yawezekana wana madai sahihi,

"Mara nyingi tuhuma za wanasiasa zinatakiwa kuangaliwa pande mbili kwa kuwa upande mmoja inaweza kuwa ni kweli na kwa upande wa pili inaweza kuwa si kweli, hivyo wabunge hao wasikilizwe ili kubaini wanachokilalamikia," alisema mwanahabari huyo.

Mkoa wa Mwanza
Uamuzi wa Chadema pia uliungwa mkono mkoani Mwanza ambako walisema unalenga kurejesha thamani ya kura.
Yohana Kagenzi, mkazi wa jijini Mwanza, alisema Chadema wameanzisha njia ya amani na ya kiungwana ya kudai katiba na tume huru ya uchaguzi ambayo haiwezi kusababisha umwagaji wa damu na kuzusha vurugu.

“Walisema kuwa hawayatambui matokeo, lakini serikali iliona ni jambo la kawaida nadhani njia hii sasa itamkera rais na kuamua kuwasikiliza. Kama hakuchakachua kura kwa nini asisikilize malalamiko yao,” alihoji Kagenzi.

Mkazi mwingine, Saida Mbwana alisema kitendo hicho kisipuuzwe kwa kuwa kinaweza kuwa na athari kubwa.
"Kama hawamtambua Rais Kikwete, basi hata serikali atakayoiunda hawataitambua, jambo ambalo litawakosesha maendeleo katika majimbo," alisema.

Mkoa wa Arusha
Arnold Kamde, Gervas Mgonja pamoja na Prosper Mfinanga ambao ni wakazi wa Arusha walidai ya kuwa kitendo hicho si tu kwamba kimeonyesha dalili za kukua kwa demokrasia nchini, bali pia kinatoa ujumbe kwa serikali ya Rais Kikwete kuwa Chadema hawakubaliani na matokeo ya urais kwa kuwa yalichakachuliwa.

"Sheria ya nchi inasema kuwa mara matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna mtu wa kuyapinga mahakamani. Sasa hiki kitendo si tu kwamba kinaonyesha kukua kwa hali ya demokrasia nchini bali pia ni ujumbe tosha kwa serikali ya Kikwete," alisema Mgonja.

Mfanyabiashara John Lyimo wa soko kuu la Arusha alipongeza wapinzani kwa kuonyesha hasira zao za kupinga matokeo na pia alimpongeza Rais Kikwete kwa kutoa hutuba nzuri.

"Mimi sina chama ila naona Chadema wamefanya vizuri tu na wamefanikiwa kufikisha ujumbe... rais aliongea vizuri na ameonyesha ameupata ujumbe," alisema Lyimo.

Mkoa wa Mbeya
Watu wengi walioongea na Mwananchi mkoani Mbeya waliunga mkono kitendo cha Chadema wakisema ujumbe waliotaka kumfikishia rais ulifika.

“Chadema wana ujumbe ambao wamewasilisha kwa serikali ya Rais Kikwete na ni haki yao kufanya hivyo,” alisema Jeremiah Osward ambaye ni mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi.

"Kutokana na tamko lao la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, isingekuwa ni rahisi kwao kumsikiliza."

Mkazi wa Mwanjelwa, Zawadi Pangani alisema wabunge hao walikuwa sahihi kwa kuwa wanajua wanachokifanya ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kwamba bila kufanya hivyo, haki haitaweza kupatikana.

Alisema inawezekana Chadema wana uhakika kuwa mgombea wao wa urais, Dk Slaa alishinda, lakini matokeo yakatangazwa kuwa ameshindwa, hivyo wana haki ya haki yao kufanya hivyo.

Mkoa wa Morogoro
Mmoja wa wakazi wa Morogoro, Anthony Chalamila alisema tukio hilo lilitarajiwa kwa sababu mgombea wao alitamka wazi kuwa hakubaliani na matokeo yaliyomtangaza Kikwete kuwa rais kwa madai yana walakin.

“Ni lazmima wasimamie na kuyatetea maamuzi yao, hivyo haingewezekani mtu ambaye walisema hawamtambui, wakae kumsikiliza,” alisema.

"Kama wangekubali kukaa na kumsikiliza rais akihutubia, ingeonyesha wazi kuwa hawana msimamo."
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Naye Simon alisema ni haki yao kufanya hivyo kwa kuwa walishatoa sababu za msingi za kutomtambua rais.

Wanaopinga kitendo cha Chadema
Wasomi na wanazuoni
Mbali na wengi kuunga mkono kitendo hicho, wapo ambao wanakipinga wakiongozwa na kiongozi wa zamani wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Profesa Ernest Wamba dia Wamba ambaye alisema si cha kiungwana.

Akizungumza katika mkutano wa wanafalsafa ulioandaliwa na Chama wa Falsafa Tanzania (Phata) uliofanyika jijini Dar es Salaam, Wamba alisema ni vizuri kama chama hicho kingekubaliana na matokeo hayo.

“Kawaida katika siasa changamoto ni jambo la kawaida, lakini kwa jinsi ulivyoniuliza kuhusu uchaguzi wa hapa Tanzania ni kweli umefanyika na mshindi kapatikana, lakini ingekuwa vizuri kama walioshindwa wangekubali tu matokeo,” alisema Profesa Wamba.

“Wabunge wameshakula kiapo, lakini wanasema hawatambui ushindi wa rais. Wana haki ya kuzungumza kwa kuwa hiyo ndio maana ya falsafa, lakini kwa hili la kiapo litawabana. Wangekubaliana na matokeo.”

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali......

Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limeelezea kutofurahshwa na kitendo kilichofanywa na Chadema na kukitaka kutafuta njia mbadala ya kutoa dukuduku lao.

Katibu wa TEC, Padri Antony Mkunde alisema vyama vya siasa na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kutambua kuwa amani iliyopo haikushuka kutoka mahali popote bali ni mshikamano na busara katika uongozi.

"Mahali penye vurugu hata viongozi wa dini hawawezi kuhubiri; kinachotakiwa ni busara za viongozi wa nchi katika kuhakikisha amani na utulivu vinakuwapo," alisema Makunde.

Kwa upande wake Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISATAN) imekielezea kitendo cha Chadema kuwa ni utovu wa nidhamu.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Rose Haji alisema viongozi wa Chadema ni kati ya viongozi waliokula kiapo walipoapishwa hivyo wasingepaswa kususia hotuba ya rais.

"Chadema wanatakiwa kumheshimu rais kama baba mzazi kwa sababu baba anapokosea huwezi kumdhalilisha mbele ya kadamnasi hivyo heshima inatakiwa pia katika suala la uongozi," alisema Haji.

Naye mwenyekiti wa taasisi ya kiislamu ya Imam Bukhary, Sheikh Khaliha Khamis alisema uamuzi wa Chadema utasababisha chuki dhidi ya chama hicho na wananchi waliowachagua.

Alisema kitendo hicho kinaonyesha dhahiri kuwa chama hicho hakiko tayari kukubali misingi ya demokrasia nchini na kuwatumikia wananchi.

Vyama vya siasa....

CCM imewataka wabunge wote waliokiri kutomtambua rais kujitoa haraka bungeni vinginevyo wataondolewa na azimio la bunge hadi watakapotambua uwepo wa rais.

Katibu wa kamati kuu ya CCM, John Chiligati alisema kuwa kila mbunge amekula kiapo cha kutii na kulinda katiba na kitendo cha kutomtambua rais ni uvunjaji wa katiba na hivyo wabunge hao wanatakiwa kujiondoa bungeni.

Chiligati alisema kitendo cha Chadema kuruhusu wabunge na madiwani wake kuendelea na kazi wakati hawamtambui rais na serikali ni unafiki wa hali ya juu.

Chiligati aliwataka wananchi kukataa tabia za viongozi wanaokataa matokeo kwa kuwa ni tabia inayoweza kusababisha matatizo na kuchochea vurugu nchini.

Katibu mwenezi wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila alisema kitendo hicho hakikuwa cha kiungwana huku akikielezea kuwa ni sanaa ya maigizo.

Wananchi na makundi mengine
Mkoa wa Kagera
Aliyewahi kuwa waziri kwa nyakati tofauti katika awamu ya kwanza na pili Balozi Joseph Rwegasira amewaponda wabunge wa Chadema kwa kususia hotuba hiyo.

Mwanasiasa huyo alisema kitendo hicho kilikosa hekima kwa madai kuwa hawakujua sheria na taratibu.

Balozi Rwegasira, ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, alisema rais hawezi kususiwa na wabunge kwa kuwa kwa mujibu wa taratibu hata yeye ni sehemu ya Bunge na kuhoji iweje wasisusie Bunge zima.

Mkoa wa Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashar Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kilichofanywa na wabunge hao wa Chadema hakikuwa cha uungwana na si mfano mzuri wa kuigwa.

“Kama hawataki kutambua matokeo yaliyompa Kikwete urais ina maana kwa miaka yote mitano hakuna siku watashiriki kutunga sheria Bungeni kwa sababu ni lazima mwisho wa siku iidhinishwe na Rais wanayemkataa,” alisema.

Alisema anachokiona ni ubinafsi wa Chadema kwamba kionekane ndicho chama kikuu cha upinzani nchini kama ilivyo CUF kwa Zanzibar ili siku za usoni wapate nafasi ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Bendera Isinika, ambaye mkazi wa Kaloleni anayefanya kazi ya uchoraji, alipinga kitendo cha wabunge wa Chadema kususia hotoba ya Rais Kikwete kwa madai kuwa hawakuwatendea haki wananchi waliowachagua kwa kuwa walipaswa kuwashirikisha kwanza kabla ya kufanya tukio hilo.

"Kama kuna tatizo la uchakachuaji wa kura wao walipaswa kutumia njia bora na sio kususia hotuba ya Rais Kikwete kwa kuwa wao tumewachagua sisi hivyo wangetuambia kwanza kama wanataka kutoka nje ya Bunge na si kuchukua maamuzi yao," alisema Isinika.

Mkoa wa Mbeya
Mkazi wa wilayani Mbozi, Imelda Ngarawa alisema kuwa hayo ndiyo matokeo ya upinzani kwa kuwa wanafikiri bungeni ni mahali pa kufanya sanaa, hivyo wameenda huko si kwa ajili ya kuwatetea wananchi bali kufanya sanaa.

Naye mkazi wa Tukuyu wilayani Rungwe, Fadhili Sikumoja alisema kuwa wabunge hao hawajafanya vizuri kwani rais Kikwetye bado ni rais wao kwani yupo madarakani na kwamba ilikuwa vizuri wangemsikiliza hotuba yake na kama wanahopja za msingi wangewasilisha wakati wa bunge lijalo.

Mkoa wa Morogoro
Mkazi wa Morogoro Leonard Mtete alisema kuwa hatua iliyoonyeshwa na wabunge wa chama cha Chadema haikuwa nzuri kwa vile inaweza kuwashushia umaarufu ulioanza kujijenga katika chama hicho.

Alisema kuwa hali hiyo pia inaweza kuionyesha jamii kuwa chama hicho ni chama cha washari na wagomvi tofauti na jinsi ambavyo watu walinavyokichukulia kuwa mapambano yake ni kidemokrasia na ya amani.

“Mimi nafikiri wabunge wa chadema wangetumia fursa waliyonayo bungeni kupambana kwa hoja na siyo kutoka kama walivyofanya wao” alisema mkazi huyo wa Morogoro.

Mkoa wa Iringa
Mkazi wa Iringa, Fanuel Kagambo alisema haoni kama msimamo huo unaweza kuwa na manufaa zaidi ya kuwaumiza Chadema na akawashauri kuanzisha njia nyingine ya kudai madai yao kwa vile kumkataa rais na kushiriki kupiga kura za kumthibitisha waziri mkuu aliyeteuliwa naye kuonaonyesha kumtambua.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe anasemaje...
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Mbowe alisema wanaowapinga au kuwa na mawazo tofauti na uamuzi huo, wasilitazame suala hilo juu juu na badala yake waangalia hoja wanazozitoa.

Alisema Chadema haikuamka tu na kutangaza kutomtambua rais, bali inazo sababu za msingi ambazo imeziweka bayana na imekuwa ikizieleza kila kukicha na kulaumu vyombo vya habari vinavyoshindwa kuainisha malalamiko au hoja zao kwa wananchi.

Mbowe alisema, msingi wa madai na malalamiko ya Chadema ni kutaka mazingira mazuri katika chaguzi zijazo wananchi wapate viongozi waliowachagua.

“Harakati ni kitu endelevu, michakato huzaa tunda la haki, miaka 19 sasa tangu siasa za vyama vingi ziruhusiwe, kumekuwa na vilio vingi toka kambi ya upinzani na kwa wananchi, lakini wenzetu walioko madarakani hawaonekani kusikia, tunatafuta lugha mbadala baada ya lugha ya upole kusikia” alisema.

Alisema, jambo wanalopigia kelele sio kilio cha Chadema pekee, bali ni kilio cha watanzania wote na akasema wanachofanya ni kutengeneza mazingira mazuri ya uchaguzi wa mwaka 2015.

“Yapo matatizo ya msingi na ni lazima yafanyike mabadiliko ya haraka na ya msingi, kwanza ni suala la katiba, tutahitaji kuangalia katiba kama chombo muhimu kinachoweza kumkomboa mtanzania na kupunguza vilio vya watu wengi” anasema.

Akizungumza kwanini wanayakubali matokeo ya wabunge na kuyakataa yale ya rais, Mbowe anasema, “Hili ni muhimu likawa wazi, sheria iko wazi kabisa, kwamba Rais akishatangazwa na Tume ya Uchaguzi hakuna anayeweza kubadilisha wala kwenda mahakamani, lakini ukiwa huridhiki na ushindi kwa wabunge au madiwani, sheria inaruhusu kwenda mahakamani kupinga” anasema.

Anasema, kutokana na sheria hizo ambazo anasema ni miongoni mwa mambo wanayoyapigia kelele wameamua kutumia njia hiyo ya kutomtambua rais ikiwa ni katika hatarakati za kutaka marekebisho katika sheria kandamizi kama hiyo ya kutokuwa na haki ya kupinga endapo wagombea wengine watakuwa hawajaridhishwa na ushindi wa mgombea mwingine.

Hata hivyo Mbowe alisema, Chadema inatambua kuwa kwa kufanya hivyo hakuwezi kubadilisha matokeo na hakuwezi kuzuia Kikwete kuwa rais au kuongoza serikali isipokuwa kwa kufanya hivyo kutafikisha ujumbe wao kwake Kikwete na serikali yake pamoja na dunia nzima.

Habari hii imeandaliwa na Joyce Mmasi, Nora Damian, Tumsifu Sanga, Fidelis Butahe, Hussein Kauli, Minael Msuya, Fredy Azzah, Michael Matemanga, Petro Tumaini, Hussein Issa, Aziza Masoud, Hidaya omary, Burhani Yakub,Tanga, Daniel Mjema, Moshi, Moses Mashalla na Mussa Juma,Arusha, Brandy Nelson, Mbeya, Tumaini Msowoya na Habel Chidawali,Iringa,Venance George, Morogoro, Phinias Bashaya,Bukoba, Geroda Mabumo na Masoud Masasi Dodoma na Frederick Katulanda, Mwanza.

Friday, November 19, 2010

Tanzania opposition says to push for electoral reform

Fri Nov 19, 2010

By Fumbuka Ng'wanakilala

DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzania's main opposition party said on Friday it would push for reforms of the country's electoral system after walking out of parliament during the president's speech to protest disputed elections.

The opposition said the October 31 vote was heavily rigged in favour of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party and want an independent electoral commission and constitutional amendments to allow presidential election results challenged in court.

President Jakaya Kikwete, who won re-election for a second and final term in office by 61 percent, delayed his speech for a few minutes on Thursday as lawmakers from Chadema party, which makes up the official opposition camp, marched out.

"The decision to walk out was made in line with our decision not to recognise results of the presidential election," Chadema's parliamentary chief whip, Tundu Lissu, told Reuters.

"We have reasons to believe that the results of the presidential vote were heavily rigged in favour of the incumbent president."

Chadema, whose presidential candidate Willibrod Slaa garnered 26 percent of the vote, said it would snub meetings officiated by the president.

Under the constitution, parliamentary and local council results can be challenged in the courts but final presidential results as announced by the National Electoral Commission cannot be challenged.

"The only legal recourse left is to register our displeasure and walk out. We know our action may not have any legal consequences, but we will not give legitimacy to the deeply flawed election process," Lissu said.

"We will hit the road and streets of Tanzania. We will explain to the people of Tanzania what happened."

ELECTORAL REFORM

Independent election observers said the electoral commission and government officials openly favoured the ruling party during the election process.

Lawmakers from the ruling CCM party, which has a two-third majority in the 335-seat parliament, heckled Chadema legislators as they walked out of parliament.

Members of parliament from other opposition parties did not join Chadema in the walk out.

One analyst said Tanzania's constitution, which was written more than three decades ago when the east African country was under one-party rule, had become obsolete.

"I think the need for a new constitution is more scaled up now than at any other time in the country's history," political commentator Deus Kibamba said in a phone interview with Reuters.

"To avoid a political crisis, the government should start the process of writing a new constitution that will take into consideration all the major changes that have occurred in Tanzania, including the introduction of multi-party politics in 1992."

In his speech on Thursday, Kikwete urged political leaders to work together to heal wounds that emerged after the election.

He outlined priorities of his government in the next five years, which include boosting economic growth, investing in agriculture, infrastructure and improving access to social services such as education, water and electricity.

He said his government would add 640 MW of electricity to the national power grid by 2015.

East Africa's second largest economy has energy demand close to 900 MW capacity, but produces less than 800 MW. Only 14 percent of its 40 million people are hooked to the grid, while demand grows by 10 to 15 percent annually.

Source: Tanzania opposition says to push for electoral reform | Top News | Reuters

UFAFANUZI ZAIDI TOKA KWA DR SLAA

Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kui spin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomb kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.

i) Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Ni kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa.Hata hivyo,baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:

i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari. ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724 = Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450(iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252 hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 ( Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445 = Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 ( iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137. Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.

Hivyo basi kutokana na Dosari hiyo kubwa mgombea yeyote anayekubali kupokea matokeo atakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana nikakataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo hayo.

2:Tarehe 15 November, katika Press Conference iliyofanyika Dodoma, Dr. Slaa, alikabidhi rasmi majukumu kwa Chama kwa kuwa kazi ya Mgombea Urais imefikia mwisho wake Baada ya Rais kutangazwa kwa mujibu wa Katiba (Mbovu) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa chombo ambacho kilikasimiwa madaraka na Kamati Kuu ya Chama ( Sekretariat) mbele ya Wabunge wa Chama. Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo. Ni dhahiri basi, i) Wabunge wetu wala Dr. Slaa, hawakuhitaji kurudia madia ya msingi ikiwa ni pamoja na kurudia uchaguzi. Madai ya Mabadiliko ya Katiba au Katiba ya Wananchi na kudai Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kujiuzulu na Kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ni madai yaliyotolewa katika Press Conference ya Tarehe 15/11. Hata hivyo, msisitizo wa awali ni kwa kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo inaweza kutupelekea kwenye yote hayo. Mtu yeyote asiyemakini kufuatilia mtiririko huo anaweza kupotosha na kusababisha vurugu na uchochezi ambao Chadema, pamoja na jitihada zake za kudai haki zake na za wananchi waliochakachuliwa kura zao inapenda kufuata njia za kistaarabu na za amani. Ni vema yeyote anayetaka kufanya analysis ya hatua za Chadema kwanza akajielimisha vizuri badala ya kuweka hisia zake ( hakuna sababu ya kuandika na mate wakati wino upo), na wakati wowote Chadema tuko tayari kutoa ufafanuzi utakao hitajika, isipokuwa ule unaopaswa kupitia kwenye vyombo vyetu vya maamuzi kama chama cha kidemokrasia.

Mtizamo wa Bloga: Uamuzi wa Chadema Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni

Suala ambalo limetawala maongezi ya Watanzania wengi kwenye social media kwa leo ni kitendo cha wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua Bunge jipya mjini Dodoma.Kwanza niweke wazi msimamo wangu kuwa naunga mkono uamuzi huo wa Chadema.Sifanyi hivyo kwa minajiki ya kukipenda chama hicho bali ni katika kuzingatia ukweli kuwa Chadema wametumia HAKI yao ya Kikatiba na kidemokrasia kuonyesha upinzani wak kwa vitendo.Nimeandika HAKI kwa herufi kubwa kwa vile neno hilo ni muhimu katika "kuwahukumu" Chadema.

Baadhi ya wenzetu wamekishutumu vikali kitendo hicho huku wengine wakikiita "utovu wa nidhamu wa hali ya juu".Lakini wakati wenzetu hao wanatumia HAKI zao za Kikatiba na kidemokrasia kuwalaumu Chadema,hawataki kutafakari japo kidogo kuhusu HAKI kama hizo kwa chama hicho,yaani HAKI yao ku-protest kwa amani dhidi ya mwenendo mzima wa uchaguzi uliopelekea Jakaya Kikwete kuwa Rais tena.

Inawezekana tukio hilo linaonekana sio la kawaida kwa vile ni mara ya kwanza kutokea nchini.Lakini kwa wanaojishughulisha kufahamu kinachoendelea sehemu nyingine duniani watafahaku kuwa hali hiyo imeshatokea kwenye mabunge mbalimbali,kwa mfano nchini Afrika Kusini,Gambia,Sudan, India,Pakistan na Iraki,to mention only a few.

Kwa namna moja au nyingine,vipengere dhalimu vya Katiba yetu vimewaacha Chadema na alternatives chache zaidi ya hatua kama hiyo ya leo kwa vile Katiba yetu inanyima uhuru wa kupinga matokeo ya ushindi wa Rais mahakamani hata kama ushindi huo umepatikana kwa njia zisizo halali.Leo mapungufu hayo makubwa kwenye Katiba yetu yanaweza kuonekana kama jambo dogo.Lakini yayumkinika kuamini kuwa inaweza tokea tukapata Rais dikteta ambaye ameshindwa kwa mabavu lakini tukajikuta hatuna njia ya kupinga "ushindi" wake kwa vile Katiba inamlinda.

Tatizo la Katiba nyingi katika "Nchi za Dunia ya Tatu" na hususan barani Afrika ni ile tabia hatari ya katiba hizo kutumika kwa mahitaji na maslahi ya watawala walio madarakani.Na kwa vile wengi wa watawala hao ni walafi na waroho wa madaraka,na kwa vile madaraka makubwa waliyonayo yanawapa uhuru wa kufanya lolote wapendalo,katiba hizo huwekwa viraka hapa na pale sio kwa minajili ya ustawi wa taifa husika bali kikundi kidogo cha watawala.

Laiti Katiba ingekuwa inaruhusu ushindi wa Rais kupingwa mahakamani basi ni dhahiri Chadema wangeshafungua kesi.Kuna wanaosema "sasa wakitoka nje ya Bunge ndio inasaidia nini?"Majibu ni mengi ila hapa nitatoa machache tu.Kwanza,ikumbukwe kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani bungeni.Pamoja na uchache wa idadi ya wabunge wao ukilinganisha na wale wa CCM,hadhi ya chama kikuu cha upinzani ni kubwa na muhimu ndani na nje ya nchi.Pamoja na mazingira na sheria kandamizi dhidi ya vyama vya upinzani,kwa nchi masikini kama Tanzania kuna kila sababu ya sote kuonekana tumeshikamana hata kama mshikamano huo ni wa kinafiki na unawanufaisha zaidi mafisadi.Ndio maana basi nchi wafadhili zilikuwa zikiwakalia kooni watawala wetu kuhusu upatikanaji wa suluhisho la kudumu huko Zanzibar,ambapo hatimaye CCM kwa shingo upande (na licha ya ngebe za akina Makamba) leo hii tunashuhudia serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar.

Of course,hali ya kutoelewana huko Zanzibar ilikuwa serious sana hasa kutokana na vurugu za uchaguzi zilizopelekea mauaji ya watu kadhaa,ukweli unabaki kuwa msimamo thabiti wa chama kikuu cha upinzani visiwani humo,yaani CUF,kutotambua matokeo ya chaguzi mbalimbali,sambamba na kelele walizopiga kwa jumuiya ya kimataifa ndivyo vilivyopeleka leo hii kuwepo serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwahiyo wanaohoji umuhimu wa wabunge wa Chadema kususia hotuba ya Kikwete wanapaswa kuelewa kuea msimamo imara sambamba na matendo yanayothibitisha msimamo huo yanasaidia kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.Leo pale Dodoma kulikuwa na wawakilishi wa nchi na jumuiya mbalinbali za kimataifa.Vyovyote itavyokuwa,wameguswa na tukio hilo ambalo kwa hakika limetia dola utawala wa Kikwete.Baadhi ya nchi hizo ni wafadhili ambao bila wao basi mambo yanakuwa si mambo.

Lakini jingine la muhimu ni kufikisha ujumbe kwa Kikwete na serikali yake (including vyombo vya dola na Tume ya Uchaguzi) kuwa zama za "ndiyo mzee" zimefika kikomo.Hata kama Katiba inaendelea kuhalalisha sheria dhalimu (kama hiyo inayonyima fursa ya kupinga ushindi wa rais mahakamani) mwanya mdogo wa uhuru wa kidemokrasia kupingana pasipo kupigana unawezesha Chadema kuzalisha harakati mpya za mapambano dhidi ya udhalimu lakini pasipo vurugu au umwagaji damu.Kwa tunaotaka kuona Tanzania yenye kuheshimu na kuzingatia haki na stahili za Watanzania,kitendo cha leo cha Chadema kinafungua ukurasa mpya wa matumaini.Kadhalika,kitendo hicho ni hatua kubwa na muhimu ya kukua kwa demokrasia yetu kutoka vyama vinavyokubali yaishe hata pale penye uthibitisho kuwa vimejumiwa kwenye chaguzi,kwenda kwenye zama ambapo uchakachuaji wa chaguzi unaharamishwa hadharani tena kwenye live tv.Message delivered!

Ni wazi kuwa tukio la leo limemgusa Kikwete na serikali yake kama ambavyo limewagusa Watanzania wengi na jumuiya ya kimataifa.Yayumkinika kuwa inawezekana nguvu kubwa iliyotumika kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita sasa itaelekezwa katika kuihujumu Chadema ili idhoofike na hatimaye kuachana na msimamo wake wa kukataa kumtambua Kikwete.Zitafanyika jitihada za kuwqgombanisha viongozi wa chama hicho kama ilivyokuww kww NCCR-Mageuzi ya Mrema.Kuna uwezekano pia wa Dokta Wilbroad Slaa kuzushiwa zengwe zaidi ya lile ya maisha yake binafsi.Lakini hayo yanaweza kupita pasipo madhara makubwa kwani hata Baba wa Taifa na wenzake walipokuwa wanahangaikia ukombozi wa Tanzania kutoka himaya ya mkoloni walikumbana na vizingiti hivyo.Haya ni mapambano kati ya wenye uchungu na nchi yao dhidi ya wale wanaotaka kuigeuza nchi yetu kuwa "shamba la bibi" na makao makuu ya ufisadi.

Sie Wakristo tunaamini kuwa mwenye haki ataanguka saba mara sabini ( hapa simaanishi kuanguka kama kule kwa Kikwete pale Jangwani) lakini mwishowe atasimama.Kukubali uchakachuaji wa kura kutapelekea matokeo ya ain moja tu: uchakachuaji zaidi.Historia inatufundisha bayana kuwa kukubali kitu kibaya hakusaidii hata chembe kitu hicho kibaya kugeuka kizuri au athari zake kupungua.Wanaoshauri Dkt Slaa na Chadema "wakubali matokeo" hawana tofauti na wanaoweza kusema tuache mapambano dhidi ya malaria au ukimwi kwa vile magonjwa hayo yamekuwepo miaka nenda miaka rudi.

Laiti Nyerere na mashujaa wengine wa mapambano dhidi ya mkoloni wangepatwa na mawazo hayo ya "kukubali yaishe" leo hii tungeendelea kuwa chini ya mkoloni ( I know kuna watakaosema bora mkoloni kuliko fisadi.Mie nasema ukoloni na ufisadi ni mbaya kama ilivyo kwa kansa na ukimwi.Hakuna cha nafuu,wote ni maadui wanaostahili kuangamizwa).Na laiti Nyerere "angekubali yaishe pale Nduli Idi Amini alipotuvamia,basi huends leo tungekuwa sehemu ya Uganda chini ya dikteta Idi Amini au mrithi wake.

Giving up is not an alternative.Mapambano ya kudai haki (kwa amani) lazima yaendelee.Waingereza wana msemo kwamba kukubali kitu pungufu kwa minajili ya bora liende hatimaye hupelekea kupata kilicho pungufu zaidi ya kilichostahili kupatikana.Kadhalika,hatua zote za mabadiliko huanza kwa hatua chache na pengine ndogo lakini zenye impact na hatimaye kutengenrza mazingita mazuri kwa hatua kubwa zenye impact kubwa zaidi na pengine zenye kuweza kuandika historia mpya.Vilevile,actions speak louder than words.Na hiyo imethibitka leo kwani japo Chadema walishatangaza kuwa hawatomtambua Kikwete uzito wa tamko hilo haukuwagusa wengi kulinganisha na tukio la leo la kususia hotuba ya Kikwete.

And by the way,hotuba hiyo ilikuwa na tofauti gani na hotuba lukuki alizotoa wakati wa utawala wake 2005-2010?Hivyo vipaumbele sijui 13 (or were they 19) tulishavisikia kwenye kampeni za 2005 na zikarudufiwa kwenye kampeni za mwaka huu.Kama kuna yeyote aliyechukulia vimpaumbele hivyo seriously all I can say asubiri muda si mtefu atabaini "imekula kwake" as they say in the streets.

KULIKONI UGHAIBUNI: Uamuzi wa Chadema Kususia Hotuba ya Kikwete Bungeni Dodoma

Thursday, November 18, 2010

Kwanini wabunge wetu wamesusia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete

SOURCE : http://www.facebook.com/WilbrodSlaa

Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.

Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.


Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.

Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.

Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.

Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.

Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.

WABUNGE WA CHADEMA NA KUAPISHWA MIZENGO PINDA.

CHADEMA hawatahudhuria hafla ya kumwapisha Mh. Pinda na pia hawatahudhuria hotuba ya Jakaya Kikwete.

Ufafanuzi zaidi umetolewa kuwa CHADEMA haijatamka kuwa haimtambui Kikwete kama Rais wa Tanzania bali HAWAYATAMBUI MATOKEO YA UCHAGUZI YALIYOMPA KIKWETE MAMLAKA YA KUWA RAIS. Kwa tafsiri rahisi ni kuwa Kikwete hana tofauti na wale marais wanaotumia mbinu mbalimbali kuupata urais bila ridhaa ya wananchi wanaowaongeza, amewekwa madarakani na tume ya uchaguzi lakini siyo wapiga kura.

CHADEMA haiongelei matokeo ya kura za ubunge kwa vile sheria inaruhusu kuhoji matokeo ya ubunge kwenye vyombo vya kisheria, kwa hiyo CHADEMA inategemea kuhoji matokeo ya kura za ubunge katika majimbo kadhaa. Kwa upande wa Urais ni tofauti kwa vile sheria hairuhusu kuhoji matokeo ya Urais mara tume ya uchaguzi ikishayatangaza. Kwa hiyo jitihada pekee inayoweza kutumika ni ya kisiasa.

CHADEMA hawatahudhuria matukio yote mawili kama njia mojawapo ya kuonesha kutokuridhika na kile kilichofanywa na tume ya uchaguzi ya kuhujumu demokrasia.

WABUNGE WA CHADEMA NA KUAPISHWA MIZENGO PINDA.

Mfumo wa uchaguzi unawabana wanawake

na Datus Boniface

WANAWAKE waliokuwa wagombea ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, wamesema mazingira na mfumo wa uchaguzi nchini haumruhusu mwanamke kushiriki na kushindana na wanaume katika kugombea nafasi za uongozi nchini.

Wakizungumza katika kongamano la kutathmini ushiriki wa wanawake katika Uchaguzi Mkuu, lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika Mabibo, Dar es Salaam juzi, walisema wanawake wanapaswa kujipanga upya ili kuubomoa mfumo kandamizi wa kibepari unaohitaji kutumia fedha kwa kila kitu, ili waweze kushiriki vema katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Mwakilishi wa kamati ya wanawake wanaotoka katika vyama visivyo na wabunge, Eliana Mshana, alisema serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilipaswa kuwawezesha wagombea kwa kuwalipia mawakala wa kusimamia kura, lakini haikufanya hivyo.

“UNDP ilitupa taarifa za kimaandishi kuwa wao na mashirika ya kiraia wasingeweza kutuwezesha nyenzo za kugombea bali wangetoa mafunzo ya kutujengea uwezo, ili tuwe jasiri na kujiamini katika kugombea. Serikali ilipaswa kutuwezesha wanawake lakini haikufanya hivyo,” alisema Mshana.

Wakizungumzia changamoto zilizowakumba wanawake katika Uchaguzi Mkuu uliopita, walisema tatizo kubwa lilikuwa ni kuwalipa mawakala ambapo kila mmoja alipaswa kulipwa sh 10,000 kwa siku na kwamba wanawake wengi walishindwa kuzilipa.

Nuru Kimwaga kutoka Chama cha Demokrasia Makini, aliyegombea ubunge Jimbo la Gairo, mkoani Morogoro, alisema changamoto kubwa aliyokumbana nayo ni matumizi makubwa ya rasilimali fedha na vyombo vya usafiri ambavyo yeye hakuwa navyo.

Akizungumzia changamoto hizo, Ofisa Programu Mwandamizi wa TGNP, Anna Mushi, alisema kuna haja ya kujipanga mapema kuhakikisha raslimali zinatafutwa za kutosha kwa ajili ya kuweka mawakala katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Wanawake hao wametoka katika vyama 17 ambavyo ni CHADEMA, NCCR Mageuzi, CUF, TLP, SAU, CHAUSTA, UPDP, UDP, SAU, APPT-Maendeleo, DP, Jahazi Asilia NRA, Demokrasia Makini, UMD na TADEA wakati Chama cha Mapinduzi pekee hakikuwa na muwakilishi katika kongamano hilo.

Jumla ya wanawake 190 waligombea ubunge majimboni mwaka huu wakiwepo 25 CHADEMA, 24 CCM, 15 NCCR-Mageuzi, 14 CUF , 14 UDP, 14 UPDP, 12 TADEA, 11 DP na 10 UMD. Wanawake 557 waligombea udiwani majimboni.

CHADEMA kumsusa Kikwete

Mbowe akataa kuzungumzia msimamo wao

na Mwandishi wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinatarajiwa kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, pamoja na uzinduzi wa Bunge la 10 utakaofanywa na Rais Jakaya Kikwete.

Sababu za CHADEMA kutohudhuria uzinduzi wa Bunge na kuapishwa kwa Pinda, kunatokana na msimamo wao walioutangaza wiki iliyopita kuwa hawamtambui kiongozi huyo kwa sababu matokeo yaliyompa ushindi yalichakachuliwa.

Habari ambazo zilizagaa maeneo mbalimbali mkoani hapa zilibainisha kuwa CHADEMA hawatohudhuria uzinduzi huo wa Bunge, ili kushibisha hoja yao ya kutomtambua Rais Kikwete ambaye alipata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Tanzania Daima, limedokezwa kuwa msimamo huo wa CHADEMA, unamaanisha kuwa chama hicho hakitahudhuria shughuli zozote ambazo Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi.

Msimamo kama huo uliwahi kutolewa na Chama cha Wananchi (CUF), ambacho kiliwahi kutoyatambua matokeo yaliyowaingiza madarakani waliokuwa marais wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour na Dk. Amani Abeid Karume.

CUF ilikataa kuhudhuria mikutano ya Baraza la Wawakilishi pamoja na ile ya Bunge sambamba na kutoshiriki kwenye shughuli mbalimbali za kitaifa zilizokuwa zikiongozwa na marais hao.

Tofauti na CUF, CHADEMA imetoa msimamo wa kutomtambua Rais Kikwete, lakini kimeweka wazi kuwa wawakilishi wake wataendelea kuwatumikia wananchi kulingana na sheria na Katiba za nchi.

Tanzania Daima, lilizungumza na msemaji wa kambi ya upinzani bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuhusu tetesi hizo na kusema hayuko tayari kuzungumzia tetesi bali aliwataka wananchi wavute subira, ili waone kama watahudhuria au hawatohudhuria.

Alibainisha kuwa hawezi kuzuia mawazo ya watu au maneno yao, lakini ukweli utajulikana wakati ukifika kama wabunge wa CHADEMA wataingia bungeni wakati Rais Kikwete akilizindua na kulihutubia Bunge.

“Taarifa za CHADEMA kutohudhuria sherehe hizo umezipata wapi?....mimi naomba uvute subira ili kujua ukweli wa tetesi hizo, wanaozieneza wanajua walikozipata...muda utaamua,” alisema Mbowe.

Tanzania Daima, lilidokezwa na watu walio karibu na wabunge wa CHADEMA kuwa msimamo wao ni kutohudhuria sherehe hizo, kwani wakifanya hivyo ni sawa na kwenda kinyume na msimamo wao walioutoa mwanzoni mwa wiki hii wa kukataa kumtambua Rais Kikwete.

CHADEMA inadai kuwa Kikwete alipata madaraka kwa sababu ya uchakachuaji wa kura uliofanywa na Usalama wa Taifa kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kumuwezesha Kikwete kuibuka na ushindi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, leo asubuhi katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, anatarajia kuapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuidhinishwa na Bunge juzi.

CHADEMA yamwadhiri Ndugai

Yamtuhumu kumbeba Sophia Simba

na Salehe Mohamed, Dodoma

NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai, juzi alianza kuonja machungu ya kiti chake baada ya kukaliwa kooni na wabunge wa CHADEMA kwa madai anakipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, na John Mnyika wa Ubungo, walipinga kitendo cha mbunge wa viti maalum kupitishwa bila kupingwa kuwakilisha Tanzania katika Bunge la nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).

Mnyika aliomba mwongozo wa Naibu Spika kuhoji ni kanuni ipi iliyotumika kumpitisha Simba ilhali wenzake walijieleza kwa lugha ya Kiingereza na baadaye kupigiwa kura.

Alisema kanuni za uchaguzi wa wabunge wanaokwenda kwenye vyombo vingine vya uwakilishi kifungu cha 5(2)c kinasema mgombea mmoja wa nafasi inayohusika wabunge watampigia kura za ndiyo au hapana.

“Mimi napinga Sophia Simba, kutoitwa kujieleza, kuulizwa maswali na kupigiwa kura, kinyume na kanuni ametangazwa na amepita bila kupigwa,” alisema Mnyika.

Akitoa mwangozo, juu ya jambo hilo Naibu Spika Ndugai, alisema Mnyika yuko sahihi, lakini alichelewa kutoa hoja na Spika wa Bunge, Anne Makinda ndiye aliyeanza mchakato wa uchaguzi kabla ya kumuachia kiti hicho.

Jibu hilo lilimfanya Zitto na Mnyika kupinga hoja hiyo na kuzua mjadala ambao ulimfanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Federick Werema kuingilia kati.

Werema, alisema hoja iliyotolewa na Mnyika ni sahihi lakini haitoweza kujadiliwa au kubadili utaratibu uliofanyika kwa sababu ilichelewa kutolewa.

Alisema kuwa makundi mengine yalishafanya uchaguzi huo hivyo haitokuwa rahisi kwa Sophia Simba kuitwa kujieleza, kuulizwa maswali na hatimaye kupigiwa kura.

Maelezo hayo, yalipingwa na Zitto kwa madai kuwa kanuni zimekiukwa na Bunge haliwezi kuendeshwa kwa ukiukaji kanuni au upendeleo kwa chama fulani.

Mjadala wa kupinga jambo hilo ulizidi kushika kasi na kumfanya Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM), kusimama kutoa taarifa kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) inayohusu mamlaka ya Spika.

Alisema kanuni hiyo, inamtaka mbunge ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika kuwasilisha sababu za kutoridhika kwake kwa katibu wa Bunge, ambaye atawasilisha malalamiko hayo kwa Spika.

Chenge alibainisha kuwa vifungu vidogo vya (5) na (6) vinaeleza Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na kamati.

Aliongeza kuwa Spika au Naibu wake hawatakuwa wenyeviti wa kikao hicho, ili kutoa nafasi na haki kwa shauri husika kusikilizwa.

Aliongeza kuwa majibizano kati ya kiti (Spika au Naibu Spika) na baadhi ya wabunge kutokana na uamuzi wa Spika hayana nguvu.

Zitto aliinuka na kumjibu Chenge kuwa Kamati ya Kanuni za Bunge bado haijaundwa, hivyo hawawezi kuwasilisha taarifa ya kutoridhishwa kwake.

Akizungumzia kuhusu uadilifu kwa kiongozi wa Bunge (Spika, Naibu wake au wenyeviti wa Bunge), kwa kutumia kanuni ya nane, inayozuia upendeleo, Zitto alitaka Sophia ajieleze na apigiwe kura.

Mjadala huo ulihitishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, ambaye aliwaonya wabunge wanaotaka kucheza na mamlaka ya Spika au Naibu Spika kujirekebisha mara moja, ili kuepuka adhabu.

Mjadala huo, ulisababishwa na uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la SADC.

Aliongeza kuwa mabishano hayo yanapaswa yachukuliwe na wabunge wapya kwa umakini mkubwa hasa kwa kusoma sheria na kanuni za kudumu za Bunge.

Pamoja na Sophia, wajumbe wengine wa Bunge la SADC-PF ni Mohammed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF), ambaye baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 275 dhidi ya kura 47 za mgombea wa CHADEMA, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Mwingine ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (CCM) aliyepata kura 180. Waliopiga kura walikuwa wabunge 324.

Wednesday, November 17, 2010

Unabii wa kuanguka kwa CCM utatimia hivi

19 Septemba 2007

Unabii wa kuanguka kwa CCM utatimia hivi
na
Samson Mwigamba

ITAKUWA ni mwishoni mwishoni mwa utawala wa rais wa awamu ya nne kutoka CCM. Utawala uliowapa matumaini makubwa hewa wananchi wa jamhuri hii.

Sauti zao wananchi zitapaza na kusikika kila pembe ya nchi hii kama sauti za matarumbeta yatakayopigwa na malaika watakaoambatana na Bwana Yesu wakati akirudi mara ya pili duniani kuchukua wateule, yatakavyosikika kila pembe ya dunia hata kuamsha waliolala makaburini kama inavyosimuliwa ndani ya Biblia takatifu. Wananchi watakumbuka jinsi “walivyouziwa mbuzi kwenye gunia”.

Mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, CCM iliunda kamati iliyoongozwa na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wakati huo), Pius Chipanda Msekwa kwa ajili ya kupitia na kupendekeza utaratibu bora zaidi wa kupata wagombea wa chama hicho wa nafasi mbalimbali za serikali, ikiwamo urais.

Moja ya mapendekezo kadhaa ya kamati hiyo ilikuwa ni kwamba, mgombea urais kupitia CCM awe amepatikana kufikia Mei ya mwaka wa uchaguzi.

Bila shaka ni ili kujipa nafasi ya kutosha kumtambulisha mgombea wao kwa wananchi yasije yakawakumba yale ya mwaka 1995, ambako walipata tabu ya kumtambulisha mgombea asiyefahamika kwa kipindi kifupi hadi wakalazimika kumtumia Baba wa Taifa kuzunguka nchi nzima, akimnadi Benjamin Mkapa ambaye hadi leo wengi wanaamini kwamba wakati akipitishwa na chama kugombea urais, alikuwa hafahamiki kiasi cha baadhi ya watu kudhani aliyepitishwa alikuwa Kenneth Mkapa, mchezaji beki namba tatu wa timu ya Yanga wakati huo.

Hata kabla ya mwaka wa uchaguzi mkuu uliofuata, yaani 2005, pilikapilika zilikuwa zimeshaanza ndani ya chama hicho kikongwe Afrika. Kukawa na kupakana matope kwingi miongoni mwa wanachama walioonekana kuwa na nafasi na nia ya kugombea urais kupitia chama hicho.

Aghalabu kila aliyepakwa matope alisikika akisema “waliofanya hivyo ni kwa malengo ya 2005”. Ni katika wakati huu tulipoanza kuona kalamu ikitumika kwenye magazeti kuchafua baadhi ya watu na kusifia wengine. “Wenye akili” wakang’amua kuwa makusudi ya maandishi kama hayo yalikuwa ni mkakati.

Hatimaye 2005 ikawadia na muda wa kuchukua fomu za kugombea urais kupitia CCM ukawadia. Wanaume 11 waliokamilisha timu ya mpira wa miguu wakajitosa kuchukua fomu.

Wakati huu ndipo tuliposhuhudia kiwango cha juu cha kutumia magazeti kuchafuana. Katika hali ambayo binafsi sikuitarajia, mwandishi maarufu niliyemheshimu na kumpenda kwa makala zake, wa gazeti maarufu la Kiswahili ambalo nilikuwa silikosi kila Alhamisi, alitoa makala mfululizo za kumchambua kila mgombea aliyeomba kupitishwa na chama hicho kuutafuta urais.

Kama kujihami akatoa sababu ya kufanya hivyo tangu mwanzo kabisa wa makala zake, eti ilikuwa ni kwa sababu CCM ndicho chama tawala na hivyo kikipata mgombea mbovu taifa litaathirika.

Mwandishi huyo hakupima hata utetezi wake butu kwa sababu wakati huo kulikuwa na vyama vingine vipatavyo kumi na tano ambavyo vyote vilikuwa na nafasi ya kusimamisha wagombea urais.

Hivyo kama Watanzania wangeona CCM wamesimamisha mgombea mbovu, bila kujali sababu za kufanya hivyo, wangechagua mgombea wa chama kingine. Na hili ndilo lengo hasa la demokrasia ya vyama vingi.

Sasa mwandishi alijuaje kwamba lazima CCM ndiyo ishinde na nani alimwambia kwamba wajumbe wa vikao husika vya uteuzi ndani ya chama hicho hawana uwezo wa kumtambua na kumpitisha mgombea bora kati ya hao kumi na moja mpaka yeye awape wasifu wa kila mgombea?

Waandishi wa namna hii hawakuwa mmoja wala wawili, walikuwa ni wengi, tena ambao hatukuwatarajia. Jitihada zao zilizaa matunda pale ambapo mgombea wao ndiye hatimaye alipitishwa.

Siku ile alipopitishwa, hakuna atakayenibishia nikisema kwamba nchi ililipuka kwa kelele za shangwe na vifijo, maana shangwe haikuwa ndani ya Ukumbi wa Chimwaga pekee, bali kila kona nchi ilizizima, watu wakikokodolea macho kwenye TV.

Wakati Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo, Spika Msekwa akisimama kusoma matokeo, nilikatiza mtaa mmoja hapa Arusha na kuona watu wamerundikana kwenye pharmacy moja.

Niliposogea, ndipo nikaelewa kilichokuwa kinaendelea. Tukio hilo liliniachia mshangao na maswali mengi, hasa nikijiuliza Jakaya Kikwete alikuwa na umaarufu gani kiasi cha kushangiliwa vile kwa kuteuliwa kwake kugombea urais.

Ni kweli kwamba hakuwa hata na robo tatu ya umaarufu wa Augustine Mrema mwaka 1995. Hakukaribia hata umaarufu wa Pombe Magufuli, mjenga barabara ambaye alihifadhi kichwani mtandao wote wa barabara zilizo chini ya TANROADS nchi nzima ikiwa ni pamoja na makandarasi wanao/walio – zijenga, wafadhili wanao/walio – toa pesa na hatua zilizofikia.

Huwezi kulinganisha umaarufu wake na ule wa Dk. Salim Ahmed Salim, aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na aliyeukosa Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa tundu la sindano.

Kampeni zilipoanza ndipo nikaelewa kilichofanyika, ambacho sasa ni dhahiri kwa wananchi wote. Kwamba kulikuwa na mtandao uliojumuisha wafanyabiashara, waandishi wa habari, wasanii na watendaji wakuu wa chama na serikali, ulioanza kutengenezwa tangu mwaka 1995 kwa lengo la “kumkuza” na “kumtangaza” mteule wao, hata aonekane maarufu kuliko marais wengine waliopita, isipokuwa tu Mwalimu Nyerere, ambaye ndiye aliyekuwa analinganishwa naye. Kazi hiyo ilifanywa kwa ustadi hadi akaonekana ni “chaguo la Mungu” na wengi wakaaminishwa hivyo.

Utawala wa huyu mteule ulipoanza kwa ari, kasi na nguvu ya soda, kila mtu alikubali kwamba huyu ndiye rais. Hata wanasiasa wa kambi ya upinzani walionyesha kumkubali, hata baadhi yao kufikia kusema “anafanya kazi ya upinzani”.

Watu wakamkubali kwa maneno yake na kwa baadhi ya hatua zilizochukuliwa mwanzoni mwa utawala wake. Kila kukicha kukawa na kauli mbalimbali kwenye magazeti kama; “Awamu ya nne spidi 120”, “Kasi ya Kikwete yamkumba kigogo”, “Sumaye aonja shubiri ya ari na kasi mpya”, “Lowassa hatari, asafiri Arusha – Dar – Arusha kwa siku moja, asimamisha mhandisi wa wilaya”, n.k.

Muda si muda, wananchi wakang’amua kwamba matendo hayo yote yalikuwa nguvu ya soda, walikuwa “wameuziwa mbuzi kwenye gunia”. Kumbe waliotabiri kwamba Kikwete alikuwa ni chaguo la Mungu na wale waliosema ni tumaini lililorejea, walikuwa ni manabii wa uongo. Ukweli ni kwamba alikuwa ni chaguo la wanamtandao na si tumaini lililorejea, bali ni kukata tamaa kulikorejea.

Safari za rais nje ya nchi zikatumbua zaidi ya sh bilioni 24 ndani ya mwaka mmoja wa fedha wakati nchi ikiwa gizani bila umeme, thamani ya shilingi yetu haikushuka bali iliporomoka, mfumuko wa bei ukaongezeka, akiba ya fedha za kigeni aliyoacha mzee Ben ikanywea, mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ikakatwa kwa asilimia 40 kinyume cha sheria iliyoanzisha mikopo hiyo, rushwa na ufisadi vikaongezeka, mikataba mibovu ikazidi kusainiwa huku watuhumiwa wakifichwa na kulindwa, kodi za mafuta zikapanda na kuongeza ugumu wa maisha huku mishahara ikiongezeka kiduchu.

Lakini katikati ya shida hizo za wananchi, ofisi ya waziri mkuu ikinunua gari mbili tu kwa shilingi milioni 400, posho za wabunge zikipanda hadi sh 100,000 kwa kikao kimoja tu cha siku moja, matumizi ya serikali yenye mawaziri na manaibu wao wapatao 60 zikazidi kuliliza taifa huku kazi wanayoifanya haionekani.

Ndipo kuelekea mwishoni mwa utawala huu, wananchi watapiga kelele. Baadhi ya vyombo vya habari vilivyoupigia debe utawala huu vitajiona viliwasaliti Watanzania. Vitaungana na vyombo vya habari makini kupiga kelele itakayosikika kila kona ya nchi kwamba uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli bado yanahitajika.

Wanafunzi wa vyuo na sekondari watapaza sauti, watumishi wa umma na binafsi watapiga kelele kila kona wakiambiana “hakuna njia ya kuleta mabadiliko nchi hii bila kuipiga chini CCM”.

Baada ya “chaguo la Mungu” kushindwa kuleta mabadiliko, sasa itakuwa ni dhahiri kwamba hata malaika ndiye awe rais wa Tanzania kupitia CCM kwa mfumo uliopo, hakuna mabadiliko yoyote.

Kule vijijini, walimu wa shule za msingi na sekondari watageuka na kuwa walimu wa wananchi wa vijijini wasio na uelewa mpana na mwamko wa mambo ya kisiasa. Watawaelewesha kuwa mabalozi wa nyumba kumi ni viongozi wa CCM tu, na hawana haki wala uwezo wa kuwatisha wananchi hata waichague CCM bila ridhaa yao.

Watawaelimisha kwamba Tanzania itaendelea kuwa nchi ya amani tena amani ya kweli (si ya uongo) bila CCM. Wala anguko la CCM halitaifanya nchi iwe na vita kama Rwanda na Burundi.

Watawaelimisha wananchi nao watayapuuza madai hayo ya kutungwa na CCM, wasiwe na wasiwasi maana chama cha upinzani kikishinda majeshi yote yataitii serikali mpya na kama CCM wana mpango wa kushika silaha na kuingia msituni watakamatwa hata kabla hawajafika ukumbi wa Chimwaga kupanga mipango hiyo.

Ni katika wakati huo ambako walimu hawa watawaonyesha wananchi kodi zote wanazolipa wanaponunua viberiti, chumvi, sukari, sabuni, n.k kutokana na vipesa wapatavyo kwa kutembea kilometa 30 kwa miguu isiyo hata na kandambili kwenda kuuza vitu kama kuni, ndizi, viazi, mbogamboga, n.k. watagundua kwamba kumbe kodi si tu ile waliyokuwa wanalipa ikiitwa ya maendeleo iliyofutwa.

Watatambua kuwa kumbe kuna kodi za moja kwa moja (Direct – taxes) na za mlango wa nyuma (Indirect taxes), ambazo ndizo zinaathiri sana maisha yao ya kila siku.

Watagundua kwamba kumbe wao ni watu wakubwa sana na wanaopaswa kuheshimiwa ndani ya nchi hii. Maana wao ndio waajiri wa serikali.

Ndio wanaowaajiri wabunge, rais na mawaziri wake. Watatambua kuwa wao walio vijijini ndio wanapaswa kuheshimiwa zaidi maana kwa wingi wao ndio wanashikilia cheo cha juu zaidi katika ofisi ya ajira ya wabunge na rais. Wao ndio hutia saini ya mwisho ya ajira ya vigogo baada ya kupata mapendekezo toka kwa wasaidizi wao (wananchi wa mijini).

Watasema sasa tunaitumia vema sahihi yetu, kwa kuheshimu mapendekezo ya wasaidizi wetu walio mijini, na ambao ndio huwafanyia usahili viongozi kwa kupima vitendo vyao, maisha yao ya ukwasi na umaskini wa Watanzania. Wataazimia kuinyima CCM kura.

Wakati huu ndipo vyama vya upinzani vitajiona vina deni. Wananchi watavilazimisha viunganishe nguvu zao na kumsimamisha mgombea mmoja wa urais hata kama CCM haitakuwa imebadilisha sheria ya vyama vya siasa ili kuruhusu vyama kuungana.

CHADEMA, TLP, CUF, NCCR – Mageuzi, UDP na vyama vingine makini vitakaa pamoja na kumpitisha mgombea mmoja na mgombea mwenza wake wa urais. Kila jimbo la uchaguzi atakuwapo mgombea mmoja tu anayekubalika wa upinzani anayewakilisha vyama vitakavyokuwa vimesaini mkataba wa ushirikiano.

Kauli za hamasa kama “hakuna kulala mpaka kieleweke”, “haki sawa kwa wote”, “wananchi tujazwe mapesa”, “nguvu ya umma” nk, zitasikika kila mahali, wakati wa kampeni.

Viongozi wa upinzani watajigawa kila pembe ya nchi na kusambaa, huku wote wakimpigia debe mgombea mmoja tu wa urais na mgombea mmoja wa ubunge katika kila jimbo.

Tukumbuke kuwa kabla ya kampeni, vyama vilivyoamua kushirikiana vitakuwa vimekaa chini na kukubaliana juu ya sera murua za kuiongoza nchi yetu, zitakazotokana na muunganiko wa sera za vyama mbalimbali vya upinzani.

Kubwa likiwa ni kuunda katiba mpya baada ya uchaguzi na kubadili mfumo wa utawala wa nchi hii kubwa ili kuanzisha serikali za majimbo na kufuta kabisa cheo cha waziri mkuu, mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.

Naam, wakati wa kura utawadia. Kura zitapigwa na ingawa CCM itajitahidi kuiba kura kama kawaida yake, lakini bado zitakazobaki zitatosha kuupa upinzani ushindi mzito na kuuwezesha kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Mara tu baada ya rais kuapishwa atalihutubia Bunge na kutangaza mchakato wa kukusanya maoni ya kuunda katiba mpya kwa kutumia tume maalum itakayoongozwa na jaji maarufu kama Robert Kissanga.

Wakati mchakato huo ukiendelea, mali zilizohodhiwa na CCM wakati zikiwa ni za wananchi wote, kama viwanja vya mpira, zitarejeshwa serikalini. Wakati huo huo nyumba zote za serikali walizojiuzia vigogo zitarudishwa serikalini.

Mikataba mibovu ya madini, IPTL, Richmond, ATCLM, TTCL n.k itapitiwa upya sambamba na kuwafikisha mawaziri wote wa zamani kama kina Nazir Karamagi na watendaji wakuu mbele ya jopo maalum la majaji ili kujieleza kwa nini walisaini mikataba isiyo na masilahi kwa taifa.

Watumishi wote wa umma watalishwa yamini kuhakikisha hakuna hata shilingi moja ya serikali inayopotea kwa njia yoyote ile bila kunufaisha Watanzania wote.

Hata hivyo kima cha chini cha mshahara kitapanda hadi sh 275,000 bila kugusa kodi za vitu ‘sensitive’ kama mafuta, ili kuepuka mfumuko wa bei na hivyo ongezeko la mshahara kumnufaisha mfanyakazi wa kawaida. Hii itakuwa motisha kwa watumishi wa umma kuachana na rushwa na ubadhirifu.

Muda si muda serikali itakuwa na pesa nyingi, kwani TRA watakusanya si chini ya sh bilioni 300 kwa mwezi, utalii na maliasili zingine zitamwaga trilioni za shilingi ndani ya hazina kufuatia udhibiti wa maliasili zetu na kurekebisha mikataba mibovu ambayo hata hivyo itasitishwa kila inapofikia mwisho wa kipindi cha mkataba.

Pesa hizi zitatumika kutoa elimu bure hadi chuo kikuu, matibabu bure, kuleta mapinduzi ya kweli ya kilimo na ujenzi wa miundombinu kama barabara za lami, viwanja vya ndege vya kisasa, umeme wa uhakika na mawasiliano.

Katiba itakapokamilika na kuruhusu uanzishwaji wa serikali za majimbo, italeta ushindani baina ya majimbo huku kila jimbo kikiongozwa na viongozi wazawa ndani ya jimbo husika, wenye uchungu na maliasili zao na nia ya kuleta maendeleo majimboni mwao kwa msaada wa karibu wa serikali kuu.

Hii itaongeza kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi na hapo ndipo Tanzania itakuwa tayari KUPAA!!!

Barua kwa Rais Kikwete - Wagombea Binafsi

31 Mei 2006

Barua kwa Rais Kikwete - Wagombea Binafsi

MAAMUZI YA MAHAKAMA KUHUSU WAGOMBEA BINAFSI NA UMUHIMU WA KUBADILI MFUMO WETU WA UCHAGUZI

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ikulu,
Dar es Salaam.


Ndugu Rais,

Kwanza naomba nikupe pongezi kwa kuchaguliwa kwako kuwa Kiongozi wa nchi yetu. Inawezekana kuwa tayari nimeshakupa hongera tulipokutana pale Dodoma siku uliyomwapisha Waziri Mkuu Ndg. Edward Lowassa au vile vile tayari umekwisha pongezwa na Mwenyekiti wangu wa chama cha CHADEMA ndg. Freeman Mbowe pale Diamond Jubilee. Hata hivyo, kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na wewe kama Rais kwa barua, nimeona ni bora nikupe hongera zangu tena.

Vile vile nikutie moyo kwa kazi unayofanya. Umeanza kazi kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya ili kuleta Mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli kwa jamii ya Watanzania.

Kwamba timu yako nzima ya uongozi inafanya kama wewe ni suala la mjadala mwingine. Sina shaka hata kidogo kuwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge letu tukufu wanaendana na ari yako. Ninaamini watakusaidia vya kutosha. Nina imani kubwa sana na viongozi hawa licha ya changamoto kadhaa ambazo ninaamini ni matatizo ya kimfumo (systematic inherent problems) tu ambayo hata sisi tungefanikiwa kupata ridhaa ya Watanzania na kuongoza taifa letu tungekutana na changamoto hizo. Nikisema sisi, ndugu Rais, nina maana CHADEMA.

Ndugu Rais, barua hii ni yangu binafsi kama kijana mwenye kulipenda taifa langu na bara langu la Afrika. Kwa kuwa nina ofisi ya kitaifa, kama Mbunge, nakuomba uchukulie barua hii kama inatoka kwa Mbunge kwenda Rais wa nchi ambae ni sehemu ya pili ya Bunge.

Barua hii ina mawazo ya kujaribu kusaidia kutokana na changamoto iliyopo mbele yetu kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu kuruhusu wagombea binafsi wa uongozi wa nchi yetu. Wagombea binafsi maana yake ni wagombea wasio na vyama vya siasa. Wanaweza kuwa ni wanachama wa vyama, lakini hawana dhamana ya vyama vyao wanapogombea na kisha kuchaguliwa kuwa viongozi.

Ndugu Rais, kuwa na mgombea binafsi haina maana kuwa mgombea huyu hatakuwa na udhamini wa aina fulani. Mfano, Kikundi cha Wafanya biashara wa zao fulani (mfano Tumbaku kule Urambo) wanaweza kudhamini watu kadhaa, wakagombea udiwani, wakashika “majority” ya Halmashauri ya Wilaya. Maana yake ni kuwa maamuzi yote ya Halmashauri ya Wilaya Urambo yatakuwa chini ya kundi hili. Hii inawezekana. Inawezekana pia hata kwa ngazi ya Ubunge. Sina uhakika katika ngazi ya Urais. Lakini sina haja ya kukuhadithia alichofanya Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi.

Ndugu Rais, Vyama vya siasa vimewekewa masharti ya kuandikishwa. Kuna sheria inayopelekea vyama kusajiliwa na kuna ofisi ya Msajili wa vyama anaeratibu vyama vyote ikiwemo chama chako, CCM. Hata kama mmoja wa wajumbe wa secretariat ya chama chako alinukuliwa akisema Msajili wa vyama ni karani tu, lakini ofisi hii ina majukumu makubwa sana ya kuhakikisha taifa halimeguki kisiasa. Ingawa nina mawazo tofauti, kwamba ofisi hii ingeweza kuwekwa chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya muundo wa sasa. Lakini hii sio hoja kwa sasa.

Kiufupi ni kwamba vyama vinaratibiwa. Katiba zao na hata kanuni zao za uteuzi wa wagombea wa nafasi zote zipo kwa Msajili. Msajili aweza kufuatilia kuona kama chama kinafuata taratibu zake na anao uwezo wa kuonya.

Ndugu Rais, nchi haiwezi kuwa na ofisi ya kuratibu wagombea binafsi. Nidhamu yao Bungeni na hata katika Mabaraza ya madiwani haitaweza kushughulikiwa na vyama. Hawa hawana vyama!

Ndugu Rais, sio nia yangu hata kidogo kushauri kuwa tusiruhusu wagombea binafsi. Hii itakuwa ni kuzuia uhuru wa Mtanzania kushiriki katika uongozi wa nchi. Mahakama imesema ni kinyume na Katiba. Katiba ambayo sote tumeapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea. Kiapo tulichokula ni kikubwa sana na lazima tuheshimu kiapo. Hata hivyo, suala hili ni lazima tuliangalie kwa mapana yake.

Mara baada ya mahakama kutoa hukumu nilinukuliwa na magazeti ya hapa nyumbani na moja na Ghuba (Gulf Times) na lingine na Marekani (The Herald Tribune). Nilisema kuwa maamuzi ya mahakama yanatutaka tufanye mabadiliko makubwa ya mfumo wetu wa siasa. Maamuzi ya mahakama yanaweza kuudhoofisha mfumo wa vyama nchini kwetu.

Uzoefu wangu unaonesha kuwa Watanzania hawapendi vyama. Sio manazi wa vyama vya siasa. Hawaoni kama vyama vinawawakilisha. Wanaona vyama kama vikundi tu vya watu wenye madhumuni ya kutawala. Hawaoni vyama kama Asasi muhimu za kujenga demokrasia na kutoa sera mbadala. Ndio maana kati ya Watanzania milioni 16 waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2005, ni Watanzania milioni tano tu ndio wanachama wa vyama. Hata wewe ndugu Rais, umechaguliwa na Watanzania milioni 9 wakati chama chako kina wanachama milioni tatu tu!

Kwa hali hii ya udhoofu wa vyama kutokukonga nyoyo za Watanzania, wagombea binafsi wanaweza kuvuruga kabisa mfumo wa vyama. Hii ni hatari ninayoiona. Ni hatari kweli kweli. Ni hatari kwa sababu, nchi inaweza kukatika kwa matamshi tu ya mtu ambae hana chombo cha kumdhibiti. Vyama vinadhibiti wanachama wake.

Ndugu Rais, mimi binafsi nina maoni yafuatayo ili kuimarisha Demokrasia katika nchi yetu kufuatia hukumu ya mahakama kuu. Mapendekezo yangu haya yanaweza kuwa sehemu ya mjadala wa kitaifa uliouahidi wakati ulipolihutubia Bunge mwishoni mwa Disemba 2005.

* Serikali ikubaliane na maamuzi ya Mahakama:

Mabadiliko ya Katiba yapelekwe Bungeni na kuondoa vizuizi vya Watanzania kugombea uongozi kwa kudhaminiwa na vyama. Sheria ya Uchaguzi ifanyiwe marekebisho na kuweka masharti kadhaa ya kufuata kwa mgombea binafsi. Mfano, mgombea mtarajiwa kupata wadhamini 50 kutoka kila kata iliyopo katika Jimbo, kama anagombea Ubunge na wadhamini 20 kutoka kila Mtaa/Kijiji katika Kata kama anagombea Udiwani. Kama anagombea Urais, apate wadhamini 1000 kutoka kila Mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

* Mfumo wa Uchaguzi urekebishwe na kuruhusu mfumo mchanyato wa uwiano wa kura na mfumo wa “first-past-the-post”:

Ndugu Rais, mfumo wetu wa uchaguzi unataka Wabunge na Madiwani kupatikana kutoka katika majimbo na kata tu. Wabunge wanawake hupatikana kwa uwiano wa kura za Wabunge nchi nzima na Madiwani wa wanawake kutokana na uwiano wa viti vya udiwani ambao kila chama kimepata.

Lakini Wabunge Wanawake hawana mamlaka ya kisheria kwa eneo maalumu. Kwa sasa ni rahisi kusema kuwa wanatoka mikoani, lakini hii ni kwa sababu tuna chama kimoja kikubwa na hivyo kupata kura za kuenea mikoa yote. Huko mbele, tena na hawa wagombea binafsi, itatokea mikoa ambayo haitapata wabunge wanawake kwa sababu kura hazitotosha kwa chama kimoja kugawa wabunge kila mkoa. Umefikia wakati sasa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchaguzi ili kuingiza uwakilishi wa uwiano.

Napendekeza kama nchi tutafakari mambo yafuatayo yanayohusu mabadiliko ya mfumo wa kisiasa wa nchi yetu:

1. Wabunge wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi watokane na Halmashauri za Wilaya za sasa. Mfano, badala ya Wilaya ya Manispaa ya Kinondoni kuwa na Wabunge watatu, iwe na Mbunge mmoja tu. Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji ndio iwe Jimbo la Uchaguzi. Katika ngazi hii wagombea wasio na vyama waruhusiwe pamoja na wale wenye vyama.

Kwa hali ya sasa tutapata Wabunge 119 kutoka kundi hili. Idadi yao itaongezeka kutokana na kuongezeka kwa Halmashauri zitakazoundwa pindi mahitaji yanapotokea. Haitakuwa tena kazi ya Tume za Uchaguzi kuunda Majimbo ya uchaguzi bali vile vigezo vya kuunda Halmashauri (Baraza la Madiwani) vilivyopo kisheria (Local Government Authorities Acts) ndio vitatumika.

2. Wabunge 231 watokane na kura za uwiano. Vyama vya siasa vitapata viti kutokana na uwiano wa kura ambao kila chama kimepata katika Mkoa. Chama cha siasa ni lazima kiwe kimepata kwanza asilimia tano ya kura zote zilizopigwa katika Mkoa husika ili kigawiwe viti. Kwa hiyo kila chama kitatengeneza orodha ya wagombea wake kwa kila Mkoa na kuipeleka Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Orodha hii iwe katika hali ambayo kama jina la kwanza ni Mwanaume la pili awe Mwanamke, hali kadhalika kama jina la kwanza ni Mwanamke katika orodha la pili liwe la mwanaume. Mikoa itapata idadi ya Wabunge kutokana na vigezo maalumu, mfano idadi ya watu n.k. Jambo la kuzingatia tu ni kwamba idadi ya sasa ya Wabunge katika mikoa isishuke baada ya mabadiliko haya (no region shall be left worse off).

Mfano Mkoa wa Kigoma una Jumla ya Wabunge saba wa Majimbo. Iwapo tukibadili mfumo kama ninavyopendekeza hapa, kutakuwa na wabunge wanne wa kuchaguliwa, kutoka Halmashauri za Wilaya Kasulu, Kibondo na Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji. Hivyo wabunge watatu watagawiwa kwa vyama kutokana na uwiano wa kura ambao kila chama kitapata.

Kwa mapendekezo haya tuna uhakika wa kuwa na Wabunge wanawake zaidi ya theluthi moja katika Bunge. Lakini pia tutakuwa na uhakika kwamba kila Mkoa utakuwa na Mbunge au Wabunge wanawake.


Ndugu Rais, mabadiliko haya ya mfumo wetu wa Uchaguzi yana faida nyingi sana. Moja ya faida ni kuvigeuza vyama vyetu vya siasa kutoka katika kushindanisha watu tu, bali pia kushindanisha sera. Kwa sababu wananchi watakuwa wanapiga kura mbili. Kura moja ya chama na kura nyingine ya ama diwani au Mbunge na Rais. Kura ya chama ndio itatufanya kupata wabunge wa uwiano. Wala hatutatumia mfumo mmoja kuzalisha mfumo mwingine. Bali kila mfumo utazalisha Wabunge kuunda Bunge letu.

Vyama vikianza kushindanisha sera tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana kama nchi katika kuimarisha mfumo wa demokrasia na kwa kweli hatutokuwa na wasiwasi wa vyama kudhoofika kutokana na wagombea Binafsi kuruhusiwa.

Demokrasia ndani ya vyama itaimarika kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi itahakikisha vyama vinapata wawakilishi wake katika Orodha ya Mikoa kidemokrasia. Pia pale Bungeni uliahidi kutengenezwa kwa “code of conduct” ambazo zitakuwa binding kwa kila chama ili kuimarisha demokrasia ndani ya vyama.

Ndugu Rais, najua una majukumu mengi ya Kitaifa. Sitaki nikuchoshe na barua yangu hii.

Hata hivyo, sisi hatutokuwa wa kwanza kufuata mfumo huu wa uwiano. Ndugu zetu wa Msumbiji wanafanya hivi. Pia Afrika ya Kusini, Ujerumani, Uswidi na hata India.

Mfumo huu, pia unaweza kumaliza matatizo ya kisiasa ya Zanzibar kwani kila kura itakuwa na thamani. Wawakilishi wa Zanzibar watatokana na kura za kila chama. Kura za Wapemba walio CCM na za Waunguja walio CUF zitahesabika. Hivyo, ile hali ya Pemba yote kutoa Wawakilishi au Wabunge wa CUF tu au Unguja yote kutoa Wawakilishi au Wabunge wa CCM tu itaondoka. Hali hii pia inaweza pelekea kupatikana kwa vyama vingine vyenye wawakilishi au Wabunge kutoka Zanzibar, kwani ushindani utakuwa ni wa sera za vyama na sio watu.

Ndugu Rais, naomba utafakari mawazo yangu haya. Ninaamini kuwa ni muhimu kufanya mabadiliko ya mfumo wa siasa. Kesi ya Mtikila sio sababu pekee ya mabadiliko, bali tunakokwenda hatuwezi kukwepa mabadiliko kwa faida ya demokrasia ya nchi yetu.

Kwa leo naomba niishie hapa. Nakutakia kila la kheri katika kazi.

Kwa ruhusa yako nina nakili barua hii kwa Spika wa Bunge letu Tukufu na pia kwa wasaidizi wako muhimu. Pia nina nakili barua hii kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala.

Wako mtiifu,

Zitto Z. Kabwe (Mb)
Kigoma Kaskazini.

Nakala:
Ndg. Samuel Sitta (Mb)
Spika wa Bunge.

Ndg. Edward Lowassa (Mb)
Waziri Mkuu.

Ndg. Kingunge Ngombale Mwiru (Mb)
Waziri (OR) Siasa na Uhusiano wa Jamii.

Ndg. Mary Nagu (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria.

Ndg. Willibrod P. Slaa (Mb)
Katibu Mkuu, CHADEMA.