Friday, November 12, 2010

anna makinda ndiye spika mpya wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania

Mh Anna Makinda ambaye alikuwa ni Naibu Spika wa bunge lililopita na pia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini mkoani Iringa,ameshinda nafasi ya kugombea kiti cha Uspika kupitia CCM baada ya kujizolea idadi ya kura 265 na kumbwaga mpinzani wake Mabere Marando (CHADEMA) ambaye amejinyakulia kura 55 katika uchaguzi huo uliofanyika leo asubuhi mjini Dodoma.

Idadi ya Kura zilizopigwa katika uchaguzi huo zilikuwa 307,zilizoharibika zilikuwa 9.Hivyo katika uchaguzi huo Mh Makinda anachukua nafasi ya kiti cha spika aliyepita Mh Samwel Sitta.

Pichani anaonekana Mh. Anna Makinda akiongea na waandishi wa habari jana nje ya jengo la Bunge . Picha kwa hisani ya Anna Itenda wa MAELEZO

0 comments:

Post a Comment