Wednesday, November 10, 2010

WABUNGE WATEULE VITI MAALUMU WA CHADEMA

Tume ya Uchaguzi imetangaza nafasi 104 ya wabunge wa viti maalumu kwa mgawanyo wake wa kuweza kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge. Hivyo baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo CCM imejizolea viti 65, CHADEMA kimepata viti 23 na CUF kimepewa viti 10.

Katika bunge lililopita kulikuwa na Viti maalumu 75 ambapo CCM ilikuwa ina viti 58, CUF viti 11 na CHADEMA viti 6. Viti vingine 6 vimeachwa wazi vikisubiri matokeo ya majimbo 7 ambayo uchaguzi wake haukufanyika.

Yafuatayo ni majina ya wanaopewa nafasi kutajwa kuwa wabunge wateule kutoka CHADEMA.

MAJINA YA WABUNGE WATEULE 23
WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NI:

Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza, Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.

Wengine ni Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha na Rachel Mashishanga.

0 comments:

Post a Comment